Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Mkuu kumbe umeona eeh, yaani Calinho kapiga faulo na kona tu kawa MTM kelele nyingi
 
Mkuu kumbe umeona eeh, yaani Calinho kapiga faulo na kona tu kawa MTM kelele nyingi
Carlinho tunamuoverrate sana ila bado hajawa fiti kama anavyozungumziwa,kocha naye ni kama hana mipango pia imagine game yetu kabla ya hii ya juzi timu ilishindwa kudeliver kwa maana mipira ilikua haiwafikii strikers na tulikosa muunganiko pale kati ilibidi ilibidi tuongeze kiungo cha kati (Mauya) alikua nje badala yake akatoka kiungo wa kati akaingia sijui Kaseke....bahati ilikua tu upande wetu tukapata matokeo.

Hii game ya juzi tulijitahidi kidogo kumiliki mpira ila tulishindwa kufanya pressing ndio wakati ambao tulimuhitaji Niyonzima ili apenyeze mipira kupitia kati kwa maana wings zilikosa ubunifu hata kina Yassin hawakua na madhara ukizingatia krosi zote kutokea pembeni waliziwin kagera in short waliwin mipira karibu yote ya juu ila ni km kocha anaamka tu na mawazo yake kabisa leo kikosi kitaanza hv zen nafanya sub ya fulani na fulani bila kutumia ufundi wowote kutegemea na hali halisi ya mchezo...inatia shaka sana hususani kwa upande wa kocha na still hapo bado hatujaanza kudaiana mishahara maana timu yetu tunaijua wnyw
 
Wewe ndio definition sahihi ya shabiki halisi wa soka
 
Wewe ndio definition sahihi ya shabiki halisi wa soka
Unajua mkuu timu hata ikifungwa ila mtu unakubaliana na matokeo bila kinyongo kulingana na inavyocheza kwa malengo ila sisi tunapata ushindi lkn unashindwa kuelewa plan ya timu ilikua nini? Mfano mpira waliopiga watani jana na namna walivyokua wanaelewana hata wangefungwa ila kuna kitu unakiona.... Bado nina wasiwasi na kocha na hata Carlinhos binafsi naona anastahili kuingia kuanzia dk70 tena timu ikiwa ishapata matokeo ya kuridhisha.... Kupiga kona mipira yote iliyokufa kwa timu yako peke yako haijalishi upande upi yani kona iwe upande wa kulia au kushoto na faulo za mbali hadi karibu ukabahatisha kuhusika katika goli moja bado ni tatizo na mchezaji yeyote anaweza kufanya
 
Kwa nini hawa Simba wanapenda kututishia sisi Yanga? Kwani wangeshinda 1 wangepungukiwa nini hawa Jamaa? 😐
 
Ni ukweli mchungu yanga kwa sasa wanatakiwa kujikita katika kutengeneza timu na waondoe dhana ya kujifananisha na simba ikiwa unataka au hiutaki simba wako mbele ya yanga kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…