Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Mamluki!!!!!

DUDU BLAKI nashabikia Yanga toka 1980 enzi za kina Mkwasa, Alan Shomari, Ahmed Amasha, Isiaka hassan Chukwu, kila siku ni chandimu tuuu hata hatushindi kikombe chochote cha Africa, tunajivunia nini? kumfunga simba? ndo maana Tanzania hatufiki popote ki Soka
 
Yanga inahitaji Centre half kevin n canavaro wote wachezaji aina moja no 4..

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
526587_396024170462569_1080341157_n.jpg

Huyu Bwana mdogo ni noma,changanya na goli lile kama alilotupia Abdalah Juma juzi alikuwa anaondoka na HATTRICK yake saafi,sema Refa alitubania kiaina
 
Hiyo fomesheni yenu ya kuchezesha 5-3-2 sijui mmeitoa wapi, naona jana ndo iliwaokoa inabidi muendelee nayo.
 
ukuta wa Yanga wa sasa hivi unanikumbusha Ukuta wa AC Milan wa Mwaka 1989 na 2003.

1989...
1. Galli
2. Tasotti
3. Maldini
4. Costacurta
5. Nahodha Franco Baresi


2003...
1. Dida
2. Cafu
3. Nahodha Paolo Maldini
4. Jaap Stam
5. Nesta
 
mchezo ulikua hivi;
-Ameanza Bahanuz wa yanga akapata,
na salm said wa mafunzo akapata.
-Canavaro wa yanga akapata,said msa shabaan wa mafunzo akakosa.
-Kiza wa yanga akapata,mohamed Ablahim wa mafunzo naye kapata.
-Nionzima wa yanga akapata, na juma jaku wa mafunzo akapata.
-Aliyefunga penalt ya mwisho ni Chuji na ile moja iliyobaki tukawagawia mafunzo watu weweweeeeeeeeeee.....!!!!.
Yanga inanipa raha sana.
hahahahahahahaaaaaaa.......!!!!
 
bongo hakuna mpira hata kidogo,,,,,ngoja ligi yagu ya ulaya ianze
 
YONDAN HALALI YANGA, KAMATI YA MGONGOLWA YAMALIZA UTATA





Alex Mgongolwa

Na Prince Akbar
KIKAO cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, kilichofanyika Julai 17, mwaka huu, kupitia mikataba na nyaraka zote zinazohusiana na mchezaji Kevin Yondani katika kujiridhisha juu ya hadhi yake ya usajili katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kimemhalalisha beki huyo wa kati kuchezea Yanga.
Taarifa ya Mwenyekiti Kamati hiyo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema;


“1. Kwa mujibu wa mapitio ya nyaraka zote zilizotajwa hapo juu na kufanyiwa upembuzi yakinifu, Kamati iliridhika pasi na shaka yoyote kuwa suala zima la mchezaji Kevin Yondani ni la kiutendaji, hivyo uamuzi wa Sekretarieti ya TFF kuwasiliana na Klabu ya Simba kwa suala hilo la kiutendaji kama Sekretarieti ilivyofanya katika barua yake ya Julai 14 mwaka huu ulikuwa sahihi.


2. Kamati ilibaini kuwa Mkataba wa mchezaji Kevin Yondani na Klabu ya Simba ulimalizika Mei 31 mwaka huu. Hivyo kwa taratibu za usajili mchezaji Kevin Yondani kuanzia Juni 1 mwaka huu alikuwa ni mchezaji huru.


3. Aidha Kamati ilibaini kuwa Mkataba uliowasilishwa na Klabu ya Simba TFF ukiwa na maana ya kuongeza mkataba uliokuwepo TFF baina ya mchezaji Kevin Yondani na Klabu ya Simba uliwasilishwa TFF, Juni 7 mwaka huu ambapo ni kinyume cha utaratibu wa kuongeza mikataba ya wachezaji unaozitaka klabu kuwasilisha mikataba ya kuongeza muda wa mikataba ya wachezaji wao wakati mkataba halisi haujaisha muda wake. Hivyo mkataba huo kwa jicho la kisheria haupo.


4. Hata kama kamati ingeuona mkataba huo katika jicho la sheria, bado mkataba huo una tatizo la kisheria hasa katika tarehe ambazo pande mbili husika ziliingia makubaliano hayo. Ukiuangalia mkataba huo unabainisha kuwa, wakati mchezaji Kevin Yondani aliingia makubaliano Desemba 23 mwaka jana, upande wa pili wa kimkataba ambao ni Klabu ya Simba inaonekana iliingia makubaliano hayo kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Geofrey Nyange Kaburu, Desemba 23 mwaka huu.


5. Kisheria utata huu unaweza kuondolewa na pande husika tu kwa kurekebisha dosari hiyo kwa maridhiano kuweka saini katika mabadiliko hayo ili kuthibitisha mabadiliko hayo. Hivyo katika jicho la kisheria mkataba huo hauwezi kutumika kumzuia mchezaji huyo kwenda katika klabu anayoipenda wakati akiwa huru.


Kutokana na maelezo yote hapo juu, Kamati imeridhia hatua iliyochukuliwa na Sekretarieti ya TFF ya kumruhusu mchezaji Kevin Yondani kuichezea timu ya Yanga katika mashindano ya Kombe la Kagame 2012,”
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kevin Yondan katika uzi wa klabu mpya, Yanga
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

maha-RAGE oyeeee!
 
Wana-JF;
Tukiwa bado na majonzi ya ajali ya meli iliyotokea na kuua watanzania na wasio watanzania wengi baharini majuzi, kuna hoja imekuwa ikijadiliwa kwamba ni kwanini marehemu wote walifanyiwa Ibada ya Kiislamu wakati kuna baadhi yao hawakuwa wa imani ya Kiislamu, kwani pia alikuwepo Padri wa Kanisa Katholiki.

Nikiwa nafikiria haya, kuna wazo hili la klabu ya Yanga chini ya Baraza la Wazee linaloongozwa na Mzee Akilimali na wenzake, kwamba ni kwanini wakati wa hitma ya kuwakumbuka waliofariki uliofanyika pale klabuni Jangwani wiki 1 kabla ya uchaguzi wa viongozi,taratibu zote zilifanyika kwa imani ya kiislamu?

Pia ukirejea uchaguzi uliofanyika wiki mmoja iliyopita napo pia zilifanyika sala la kiislamu kabla shughuli za uchaguzi hazijaanza. Na katika uchaguzi ule pia walikuwepo wagombea ambao siyo waumini wa Kiislamu kuanzia ngazi ya Mwenyekiti, Makamu na hata wajumbe.

Hivyo basi mimi napenda kuuliza, ni kwanini yanga inaitwa timu ya Wananchi wakati shughuli zake zinapofanyika ziwe za hitma au uchaguzi huwa zinafanywa kama taasisi ya Kiislamu? Je ni kweli kwamba katika yanga hakuna wanachama au viongozi ambao wana imani zingine au hawana dini? Kama ni kweli kwamba wapo wengine wa Imani tofauti, je logic inatoka wapi wa mambo ya Yanga Football Club kuendeshwa kama Taasisi ya Kiislamu?

Naomba tujadili kwa hoja na tuone nini mantiki ya YANGA F.C kuendesha shughuli zake kama Taasisi ya Kidini.
TELO.
 
Ngoja waanze wengine kwanza,mimi nitarudi baadaye kidogo
 
Back
Top Bottom