Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze ameeleza kuridhishwa na matokeo ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa jana uwanja wa Uhuru
Kaze amesema pamoja na ushindi huo, wataendelea kuboresha maeneo yenye mapungufu kuelekea mchezo dhidi ya KMC ambao utapigwa keshokutwa mkoani Mwanza
"Nimeridhishwa na matokeo ya ushindi leo, tulihitaji kushinda lakini bado tuna changamoto kwenye baadhi ya maeneo"
"Hatujawa na muunganiko mzuri tunapofika langoni kwa mpinzani lakini pia hatuko haraka kutafuta mpira pale tunapopoteza. Tumefanya mazoezi kwa siku tano tu, naamini mambo mengi yatakuwa sawa kadiri tunavyoendelea kujiimarisha," alisema Kaze
"Bado tuna mechi nyingi mpaka kumaliza msimu hivyo tunajipanga kukabili mchezo mmoja mmoja"
Bao la Mukoko Tomombe lilitosha kuihakikishia Yanga ushindi wa bao 1-0 ambao umewapandisha mpaka nafasi ya pili wakiwa na alama 16, alama tano nyuma ya Azam Fc inayoongoza ligi.