Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa taarifa kuhusu maendeleo ya kesi waliyofungua dhidi ya winga wao wa zamani Bernard Morrison
Akizungumza mapema leo kutoka jijini Mbeya, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kesi hiyo itasikilizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) na tayari imepangiwa Jaji
Mwakalebela amesema baada ya Yanga kuwasilisha malalamiko yao CAS, Morrison alitakiwa kujibu malalamiko hayo na juzi Yanga imepokea barua kutoka CAS ikiwataarifu kuwa majibu aliyotoa Morrison hayana mashiko na hivyo wanapaswa kulipia pesa za Kifaransa franc 12,000 ili kesi hiyo inze kusikilizwa
Malipo hayo yanapaswa kufanyika kabla ya Januari 12 2021 ambapo pande zote zimetakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha
"Yanga tulipeleka malalamiko Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) kupinga maamuzi ya kubatilisha mkataba wa Bernard Morisson na Yanga yaliyotolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF"
"Morrison alitakiwa kujibu malalamiko yetu na juzi tumepokea barua kutoka CAS iliyotutaarifu kuwa majibu yaliyotolewa na Morrison hayana mashiko na kwamba shauri letu litapangiwa Jaji wa kuendelea kulisikiliza"
"Hadi kufikia Leo hii, Jaji ameshapatikana, Morrison na Yanga sote kila mmoja tunapaswa kulipa Franc 12,000 tayari shauri hilo kuanza kusikilizwa"
"Tarehe ya mwisho ya fedha hizo kulipwa ni Januari 12 2021, sisi kama walalamikaji tutalipa fedha hizo ili shauri lisikilizwe", alisema Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga
Sent from my Infinix X650B using
JamiiForums mobile app