Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20201224_070012.jpg
 
MCHEZO WA YANGA VS SINGIDA WAFUTWA

“Kufuatia klabu ya Singida United kushushwa madaraja mawili, mchezo wa Azam Sports Federation (ASFC) namba 65 kati ya Young Africans v Singida United uliokua uchezwe Jumamosi Desemba 26, 2020 hautakuwepo, hivyo Young Africans sasa wanasubiri kucheza raundi ya nne 2021” Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
 
MCHEZO WA YANGA VS SINGIDA WAFUTWA

“Kufuatia klabu ya Singida United kushushwa madaraja mawili, mchezo wa Azam Sports Federation (ASFC) namba 65 kati ya Young Africans v Singida United uliokua uchezwe Jumamosi Desemba 26, 2020 hautakuwepo, hivyo Young Africans sasa wanasubiri kucheza raundi ya nne 2021” Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Hahhaha yanga anapasua anga tu kwa njia zote....ndio bingwa anavyokua[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa taarifa kuhusu maendeleo ya kesi waliyofungua dhidi ya winga wao wa zamani Bernard Morrison

Akizungumza mapema leo kutoka jijini Mbeya, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kesi hiyo itasikilizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) na tayari imepangiwa Jaji

Mwakalebela amesema baada ya Yanga kuwasilisha malalamiko yao CAS, Morrison alitakiwa kujibu malalamiko hayo na juzi Yanga imepokea barua kutoka CAS ikiwataarifu kuwa majibu aliyotoa Morrison hayana mashiko na hivyo wanapaswa kulipia pesa za Kifaransa franc 12,000 ili kesi hiyo inze kusikilizwa

Malipo hayo yanapaswa kufanyika kabla ya Januari 12 2021 ambapo pande zote zimetakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha

"Yanga tulipeleka malalamiko Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) kupinga maamuzi ya kubatilisha mkataba wa Bernard Morisson na Yanga yaliyotolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF"

"Morrison alitakiwa kujibu malalamiko yetu na juzi tumepokea barua kutoka CAS iliyotutaarifu kuwa majibu yaliyotolewa na Morrison hayana mashiko na kwamba shauri letu litapangiwa Jaji wa kuendelea kulisikiliza"

"Hadi kufikia Leo hii, Jaji ameshapatikana, Morrison na Yanga sote kila mmoja tunapaswa kulipa Franc 12,000 tayari shauri hilo kuanza kusikilizwa"

"Tarehe ya mwisho ya fedha hizo kulipwa ni Januari 12 2021, sisi kama walalamikaji tutalipa fedha hizo ili shauri lisikilizwe", alisema Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga



Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom