Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

NJE YA 18- COASTAL UNION VS YOUNG AFRICANS

Yanga wana shida kwenye eneo la Utawala, soka la kisasa huanza kuchezwa Ofisini kisha linamaliziwa uwanjani, sina uhakika kama Maboss wana watu sahihi wa mpira kwenye cycle yao, sina uhakika kama Yanga ina mikakati sahihi kwenye ofisi zao sina uhakika

Uingereza ilituletea Isaac Newton na Laws of Motions, ila Coastal Union imetuletea ERIC MSAGATI na kipaji chake, ni stori ile ile ya Yusuph Mhilu kutoka Yanga na kuwasha sehemu nyingine, leo tena ni story ya Msagati kwenye jezi ya Coastal

Ugiriki ilituletea Pythagoras na Theory zake kwenye Hesabu, ila Coastal Union imetuletea Kocha JUMA MGUNDA na ufundi wake, aliilock Coast eneo la chini na akaipa kasi ya Usain Bolt eneo la mwisho, kila alichogusa kiligeuka kuwa dhahabu pale Mkwakwani, waliubeba mzimu wa 1989 juu ya barizi la kokoni

Ujerumani ilituletea Adolph Hitler na sera zake za Nazism ila Ghana imetuletea nchini MICHAEL SARPONG na kiwango dhaifu zaidi cha mpira, mzito eneo la mwisho, hana maamuzi na anaikaba sana Yanga, inaumiza na kusikitisha sana, sio rahisi kuamini ni Professional

Kenya ilitupa Afrika David Rudisha kwenye mbio ila Coastal Union imetupa MAJIMENGI kwenye mpira wa miguu, hakuwa rahisi kukabika, hakuwa rahisi kuzuilika, aliweza kutembea vyema na chaki, aliweza kuipeleka defense ya Yanga vile anataka, mwisho wa siku at his best he is unplayable

Tuliwahi kuwa na Albert Einstein na kanuni yake na Atomic akili yake nzuri ikaipa shida dunia na bomu lake, leo tuna TUISILA KISINDA akili yake bora ikaipa Yanga bao moja na akili nyingine ikaikosesha penati muhimu sana Yanga, uzuri wa Mkakasi ndani kipande cha mti bwana

Dunia iliwahi kumiliki akili ya Muitaliano Galilei Galilei, lakini bado dunia inafeli kutumia kanuni zake, lakini Coastal Union ikatupa HANCE MASOUD alieweza vyema kutumia mbinu ngumu kumdhibiti Tuisila Kisinda, tank lake lilijaa mafuta dakika ya Kwanza mpaka ya mwisho

LONDON HAS FALLEN, Yes LAMINE AND MWAMNYETO HAVE FALLEN, game ya tano wanafungika hakuna cleansheet, sijajua sasa ni kuwa wamechoka? Sijajua ni mfumo? Sijajua ni nini ila nachojua ni kukosa watu eneo la mwisho inafanya wapinzani wafunguke muda wote
 
Msola amechaguliwa yanga kutatua shida atafute wafadhir na s kusumbua mashabiki kila siku michango tumechoka
Nadhan matajir na wafadhir wanamuona jamaa n ng'ombe aliyepata bahat ya kuongoza klabu kubwa nchini lakn UWEZO na ufanis wake hata wakisaidaia hataweza fanya Yale yaliyokusudiwa na klabu

Trust me atamaliza uongoz wake hatapata kombe lolote la ligi kuu Wala la Azam
MASHABIKI NAO WAACHE UZWAZWA WA KUPOKEA MAGARASA UWANJA WA NDEGE SIJUI HUWA WANALIPWA MTU NA AKILI ZAKE TIMAMU HAWEZ FANYA HAYA HUKU MATOKEO YANAONEKANA MABOVU
 
Kweli yanga wanaonewa.
Lile goli lililonyanyua nyavu.lina ukakasi
 
Huo mwiko haukuchubui mkuu? [emoji23][emoji23][emoji23]
YANGA NDO TIMU YA WANANCHI, YANGA NDO TANZANIA, YANGA NI NURU YA TAIFA...
JAMANI WEEE NAIPENDA YANGA KULIKO ..PIGA KELELEE KWA YANGA YAKEEEE ..
SISI TUNABEBA UBINGWA ASUBUHI TU MAPEMA SANA..
ILA HII MIKIA FC IMEKUWA TISHIO KILA GAME WANASHINDA TU ,NINGEKUWA NA UWEZO NINGEWALIPUA NA BOMU

ENEWEI #VISIT_KIDIMBWI [emoji41][emoji41][emoji41]

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…