Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

kwa ligi zetu za mchangani yanga sina tabu nao....

tatizo ndege bwana.....yaani timu za nje yanga weupe weupe..ata wawe kamili namna gani....watalia tu!!

Hivi PM wenzako wamekwambia kama nimejitolea kupaka chokaa jengo lenu la simba looote?
 
Hivi PM wenzako wamekwambia kama nimejitolea kupaka chokaa jengo lenu la simba looote?

KWA nini usingemsaidia madega.....anamlamba manji miguu sasa ..ona aibu hiyo!!

NA manji [ambaye ni nazi wa simba..alienda yanga kama pr repair tu]...amechukizwa na kitendo cha yanga kumpotezea pesa yake kumdanya eti manakarabati kaunda stadium...wakati ule ni uwanja wa rede na mdako....hauna vipimo vya FIFA....Umeona wapi uwanja upana 45m kwa 75m ..alafu eti mnaita stadium....manji alipeleka wachina pale waweke kapeti.....wakamfuata wakamuuliza kama ana akili timamu....au anataka kuanzisha aina yake mwenyewe ya mpira....wakakataa wakamuambia watajivunjia heshma ..kupokea pesa wakati uwanja hauna vipimo.......

madega akapewa pesa na manji anuunue vitanda vya 6/6 pamoja na kuwa vyumba vyenjewe ndio 6/6...na televisheni wegga...akalamba...budget kila chumba furniture ilikwa 2.5m...yeye akaenda KEKO akanunua vitanda vya boarding school 3/3 na godoro 5 inch ....,[200,000] na akanunua televisheni za kichina bei ya jumla 90,000 ..pesa iliyobaki anakimbilia kugombea ubunge....
 
Dakika ya 5 Yanga 1 Toto Africa 0, Boniface Ambani pasi kutoka kwa Abdi Kassim(BABI)
 
Wadau wa Club ya Yanga ingawa tulifungwa na Lupopo, tunaomba mwenye matokeo ya mechi ya leo kati ya timu yetu ya Yanga na Toto Africa mtuletee ili tujue timu yetu imefanya nini katika mechi ya leo
Yanga kashinda 6-0,ni historia kama walivyofungwa na simba miaka hiyo.
 
Goli la Jerry Tegeta alilifunga jana zid ya Toto kwa mara ya mwisho kufungwa katika uwanja wa Uhuru(Taifa ya zamani) lilifungwa na Kassim Ramadhan Manara siku ya Taifa Stars wanacheza na Wasudan
 
Ligi ya Mabingwa Afrika


Lupopo vs Yanga
Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga leo inapeperusha bendera ya taifa huko Lumbumbashi DRC wakati itakapopambana na FC Lupopo ya huko kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Stade de Kenya jijini Lubumbashi.

Habari za hivi punde kutoka huko Lubumbashi zinaeleza kwamba Yanga imefanya mabadiliko ya kikosi chake kilichoanza katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita ambapo Kipa atakaa Obren Circkovic wakati George Owino atacheza beki namba nne huku Godfrey Bonny na Jerry Tegete wakianza.

List kamili:
1. Obren
2. Nsajigwa
3. Maftah
4. Owino
5. Nadir
6. Chuji.
7. Nurdin
8. Bonny
9. Tegete
10. Ngassa
11. Kiggi

Yanga inahitaji ushindi wa mabao 2-0 ili isonge mbele kwenye michuano hiyo. Pambano hilo linatarajiwa kuanza saa kumi na nusu kwa saa za Afrika Mashariki.
 
Inshallah leo watoto wa Jangwani watoke na ushindi wa at least 2 goals, nitakuwa nikiwaupdate matokea kadiri ninavyoyapata..
 
Leo Athumani Iddi anatandaza soka sio mchezo pale dimba la kati mpira ni kipindi cha pili dakika ya 14 bado Yanga wanaongoza 1-0
 
Leo Athumani Iddi anatandaza soka sio mchezo pale dimba la kati mpira ni kipindi cha pili dakika ya 14 bado Yanga wanaongoza 1-0

Mkuu Mfunyukuzi,

Asante kwa kutuletea taarifa. Please endelea kutujuvya kinachoendelea huko.

Tiba
 
Leo Athumani Iddi anatandaza soka sio mchezo pale dimba la kati mpira ni kipindi cha pili dakika ya 14 bado Yanga wanaongoza 1-0
Huyo mabangi kwa sasa anapiga soka ya ukweli nadhani kocha takayekuja atamrudisha
 
Watani vipi mmefanikiwa au ndo mwisho wenu hatua ya mwanzo kama kawa?
 
For how much? Nikajilie serengeti saa hizi, yanga wanaweza kunipandisha sukari
 
Back
Top Bottom