Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,480
- 4,775
Thanks Mkuu... haya mambo naona kama yanataka kugeuka tena!!! manyema ni watoto wa mujini wale!!!
Ngoja tuone
Hapana,mtashinda mkuu..Amini hivyo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Thanks Mkuu... haya mambo naona kama yanataka kugeuka tena!!! manyema ni watoto wa mujini wale!!!
Ngoja tuone
Mtabiri wetu-umeyapata matokeo?I gues Yanga are going to loose some points today thats very sad news
Hivi ule nao unaita uwanja? Kama mna uwanja kwa nini mnaenda kufanyia mazoezi Uhuru?
Klabu kubwa haipimwi kwa mechi za mchangani bali kwa mashindano ya kimataifa ambayo mnyama ndio mwenyewe. Yebo yebo ni michuano gani ya kimataifa ambayo wamewahi kufika japo nusu fainali?
Kutembeza bakuli yebo yebo ndio wenyewe au umesahau wakati Ngozoma Matunda alipoomba timu ichangiwe mchele na maharagwe?
Mbona matajiri Simba walidaiwa CHAPATI 20 walizo kopa kwa Kaduguda ehhh
Mbona matajiri Simba walidaiwa CHAPATI 20 walizo kopa kwa Kaduguda ehhh
Papic ajitosa rasmi kumrithi MaximoKocha wa Yanga Kostadin Papic akizungumza na katibu wa Yanga Lawrence Mwalusako nje ya ofisi za Shirikisho la soka Tanzania (TFF) jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kutoa taarifa ya kutaka kuwasilisha barua ya maombi ya kazi ya kukinoa kikosi cha Taifa StarsSosthenes Nyoni![]()
KOCHA wa Yanga, Kostadin Papic jana aliwasilisha rasmi barua ya maombi ya kazi Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuwania nafasi ya kumrithi Mbrazil Marcio Maximo anayemaliza mkataba wake wa kuifundisha Taifa Stars mwezi Julai.
Papic ambaye aliweka bayana dhamira yake hiyo ya kuwania kuifundisha Taifa Stars pale tu TFF ilipotangaza kuanza mchakato wa kumtafuta kocha mpya, aliwasili katika ofisi za shirikisho hilo majira ya saa 5:30 asubuhi akisindikizwa na katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako.
Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kukabidhi barua yake, Papic alisema amefikia uamuzi huo kutokana na kuamini kuwa ana vigezo vyote vinavyomwezesha kuwa kocha wa Taifa Stars.
"Bila shaka niliweka wazi kwamba nitaomba kazi ya kufundisha Taifa Stars na leo nimeleta rasmi maombi yangu hapa kwa kuwa najiamini kutokana na vigezo vilivyotolewa ninavyo,"alisema Mserbia huyo.
Aliongeza kuwa ameshafanya kazi ya kufundisha soka sehemu mbalimbali akiwa na timu kubwa na kuziletea mafanikio, hivyo hana wasiwasi wa kuimudu vema Taifa Stars.
Akizungumzia mustakabali wake na Yanga ikiwa atakabidhiwa nafasi ya kuifundisha Taita Stars, alisema kwa sasa hakuna tatizo hasa kwa kuwa mkataba wake na Yanga unamalizika mwezi Juni na kuongeza kuwa kama atafanikiwa pia anaweza kuwasaidia kutafuta kocha mwingine ikiwa watapenda.
"Mkataba wangu unamalizika Juni hivyo kwa sasa sioni tatizo na kama nitafanikiwa katika hili ninaweza pia kuwasaidia Yanga kutafuta kocha mwingine kama watapenda," alisema Papic maarufu kama Clinton.
Endapo Papic atafanikiwa kuchukua nafasi ya kuinoa Stars, itakuwa zamu ya Yanga kutoa kocha wao kuifundisha timu hiyo ya taifa kwa kuwa mara nyingi makocha wa Stars pindi wanapomaliza mikataba yao ndipo wanaamua kufundisha klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani na Twiga.
Makocha waliowahi kuifundisha Taifa Stars na baada ya kumaliza mkataba wao kujiunga na Yanga ni pamoja na Rudi Gutadrf mwaka 1982, Joel Bendera (1986) kwa sasa Naibu Waziri wa Habari na Utamaduni akiwa kocha wa Stars aliombwa kuisaidia klabu hiyo kwenye michuano ya Afrika mashariki na kati. Mwaka 1996, Yanga ilifanikiwa kumnasa Sunday Kayuni aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Tanzania Bara.
Katika hatua nyingine Papic alisema kuwa maandalizi ya kikosi chake kinachojiandaa na mpambano wa Michuano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya FC Eloi Limpopo yanaendelea vizuri ingawa ana majeruhi wawili.
"Tupo vizuri ingawa nina majeruhi wawili ambao tayari hawatakuwepo katika kikosi cha Jumamosi, hawa ni Obren Curkovic aliyeumia katika mchezo wetu wa mwisho na Kabongo Honore aliyefanyiwa upasuaji wa goti,ukiondoa hao wengine wako vizuri." "Ninajua itakuwa mechi ngumu siwezi kuwazungumzia sana wapinzani wetu kwa kuwa hata nilipoenda kule walichezesha kikosi cha pili,lakini pia siwezi kuwadharau kwa kutambua timu ile haijacheza mashindano haya kwa miaka mitatu, sasa huwezi kujua watakuja na nguvu kiasi gani, tutakachofanya ni kuwasoma kwanza,"alisema Papic
![]()
Sijaona update nyingi za sredi hii tangu Yanga ilipofungwa na SEFC Lupopo, ndo maana nimeamua niweke picha ya mshambuliaji Ntombo Lutete alipokuwa akiipangua ngome ya Yanga. Ni wakati wa majonzi, lakini tusifiche habari kwani kwa mtindo huo hatutajua tulipokosea.
Huku kumekuwa kuchungu, nimeona Gang Chomba ameanzisha thread ya AC Milan na Man U kule.Hili Jukwaa Limelala sana inabidi mara moja moja tuwe tunaingia kuwaamsha akina Balantanda, Gang Chomba na ndugu zao
Yule jamaa majeruhi , ila ni beki wa ukweliasalaaam aleykum kandambili wote.... ninawapa pole kwa kuwakosa wakongo lakini nategemea yule beki wa malawi hamtampanga tena..