Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Kama umeridhika na Yanga uliyoishuhudia mpaka sasa hongera!, lakini sio kwa Kocha Nasreddine Nabi
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc ambao Yanga iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi, Nabi alisema mpaka sasa kikosi chake kimekamilika kwa kati ya asilimia 45% na 50%, yaani ni nusu ya vile anavyotaka kuiona timu inacheza
Mwanzoni mwa msimu Nabi alisema anahitaji siku 90 kutengeneza kikosi imara ya Yanga, amesema umebaki mwezi mmoja kufikia malengo
"Naipongeza Yanga Sc na (GSM) kwa kufanya usajili mzuri, pia naipongeza timu ya wataalamu wa viungo 'Physio', wamenisaidia kuiweka timu fiti sana na leo watu wamejionea wenyewe"
"Yanga imeimarika kwa asilimia 45% hadi 50% hapo unapoiona, ila baada ya mwezi mmoja itakuwa 100%," alisema Nabi
 
Kuna kenge linasimama linasema hata mwakajana tulianza hivohivo?? Pumbavu! Wachezaji tegemeo wote wa mwakajana wanakula benchi. Mukoko , Saido, Farid, Mauya, Nchimbi, Kaseke na Adeyuni ndio walikua tegemeo letu mwakajana ...... Yaani unaona Bangala na Aucho wako ndani wewe unaleta Ndoto zako za Abunuwai
 
Huyo anaye Sema hivyo ujue bado amelala na anaota ndoto. Hii YANGA ya mwaka huu muziki mnene.
 
Mnataka Simba wajifiche sasa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kama ni ivyo basi baada ya huo mwezi mmoja nawaomba tff waiamuru Yanga iwe inapanga wachezaji 7+1 golikipa,maana hakuna timu itakayoweza kucheza na Yanga eleven kwa eleven.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…