Kama umeridhika na Yanga uliyoishuhudia mpaka sasa hongera!, lakini sio kwa Kocha Nasreddine Nabi
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc ambao Yanga iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi, Nabi alisema mpaka sasa kikosi chake kimekamilika kwa kati ya asilimia 45% na 50%, yaani ni nusu ya vile anavyotaka kuiona timu inacheza
Mwanzoni mwa msimu Nabi alisema anahitaji siku 90 kutengeneza kikosi imara ya Yanga, amesema umebaki mwezi mmoja kufikia malengo
"Naipongeza Yanga Sc na (GSM) kwa kufanya usajili mzuri, pia naipongeza timu ya wataalamu wa viungo 'Physio', wamenisaidia kuiweka timu fiti sana na leo watu wamejionea wenyewe"
"Yanga imeimarika kwa asilimia 45% hadi 50% hapo unapoiona, ila baada ya mwezi mmoja itakuwa 100%," alisema Nabi