Ukweli ni kuwa kwa sasa timu hii ni bora sana si tu hapa nchini bali katika ukanda wetu wa Afrika mashariki,ina wachezaji mahiri karibu wawili kwa kila idara,inacheza mpira mzuri na benchi la ufundi bora.
Kasoro nyingi zinazotolewa na watu kuhusu Yanga ni jambo la asili tu; mtu,kampuni au kikundi chochote kinapofanikiwa haters huwa wanaongeza kiwango na vigezo vya mafanikio sasa wataanza kusema ili ithibitishe ubora eti ichukue ubingwa wa shirikisho,haters hawataki kukiri ubora wa Yanga..chuki chuki chuki,
Ukweli ni kuwa kadiri unavyoongeza viwango kwa mtu au kikundi unachokichukia ni sawa tu na kumpiga chura teke,Yanga wanaichukia bure tu, huu ndo muda wake,ooops nilitaka kusahau Yanga pia ina msemaji bora sana kwa sasa Afrika mashariki.