Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Asante Sana Kwa kumkumbuka Mwamba huyu. Miezi michacbe nyuma alisikika akisema miongoni mwa mambo yanayomnyima Raha ni kuachwa na timu yenu. Apumzike Kwa Amani beki mwenye kipaji na mapenzi ya kweli Kwa Taifa lake.
🙏 Huenda aliipenda kwa dhati Timu ya Wananchi ila ndo hivyo kiwango chake hakikutosha kumshawishi kocha kumbakiza.

Ila ameniuma sana aisee. Mwisho wa siku ni kumuombea tu huku sisi wengine tukiendelea kuitafakari kesho yetu ambayo ni fumbo kubwa sana.
 
Nina imani kubwa tutakuwa mabingwa 2022....Mungu ashatupa kibari amini
 
Naomba ratiba ya mechi tatu za yanga
20220212_123446.jpg
 
Ni kweli ndugu yangu jana walitunyima nafasi ya wazi kabisa hilo halipingiki, ila bana na sisi inatupasa tutengeneze nafasi nyingi zaidi na zaidi ili hata kama imetokea tumeminywa sehemu basi zile nyingine zikave ili tupate matokeo.

Sababu waamuzi wa hapa Tz akili zao wanazijuaga wenyewe na hii yote ni ile kwamba game ikiisha imeisha hivyo hata akifungiwa matokeo yanabakia yale yale na hayaezi badilika huku yeye ameshatimiza adhma yake.
Ni ujinga mtupu yani!
 
Back
Top Bottom