Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Wameishia kupika majungu ya mezani kwenda CAF wakiongozwa na mpishi wao mkuu Madeni maha-Rage

Ha..ha....haaaa.walishafia Lubumbashi hao,Maha-RAGE msanii anawazuga kuficha failure yake.
 
TANGAZO RASMI...
Kwa niaba ya familia yangu, napenda kuwafahamisha wapenzi wa Simba kuwa nimewanunulia zawadi ya Gagulo kila mmoja wenu kwa washabiki 10 wa mwanzo, na mtachagua wenyewe mahali pa kulivaa...kama utalivaa ukiwa umekalia kibao cha mbuzi huku unakuna nazi, au utalivaa leo ukija kuleta fitna na ushambenga ili Yanga tusimfturu Toto Africa...

Asanteni sana


Umesomeka mkuu,leo kwao tu..,huwa wanachonga sana....
 
Je wajua??

Yanga - mabingwa TZ mara 23
Simba - mabingwa TZ mara 17

Kweli Simba kumbe bado watoto sana kwa Yanga kimafanikio.....
 
No one like Dar Young Africans sports club..............................
 
Mimi ni shabiki wa Yanga, nilikua ccm kirumba jana, soka waliloonesha Yanga Jana ni la kiwango cha chini mno.

Napata hofu, huenda tukawa wasindikizaji kimataifa. They really need to pull up their socks!
 
Sidhani
Maana hata kama Okwi angefunga ile penati bado Yanga angekuwa Bingwa.
Timu zote zingekuwa na goal difference ya 25, lakin kipengele kinachofuata baada ya hicho kilikuwa ni kuangalia nani alimfunga mwenzake walipokutana.

Kwa mujibu wa website ya TFF, mpk final results, goal difference ni 2, hivyo hata Okwi angefunga wasingepata kitu.
 
Kuna ndugu yangu mmoja aliniambia kuwa shangilia wakati umeshameza si wakati unatafuna, kwani unaweza kupigwa ngumi ya shingo ukatapika huo mnofu ambao unataka kuumeza. Ndicho kilichowatokea Simba michuano hii..........
 
Mimi ni shabiki wa Yanga, nilikua ccm kirumba jana, soka waliloonesha Yanga Jana ni la kiwango cha chini mno. Napata hofu, huenda tukawa wasindikizaji kimataifa. They really need to pull up their socks!

suala la viwango duni si hoja.....cha msingi kuijaza silverware cabinet!

angalia Man U kule ulaya wanavyofukuzia mataji matatu huku wakicheza kwa kiwango duni!

au umesahau pia Kili Stars walivyochukua Challenge cup na kiwango duni kabisa?

niendelee???
 
Majuto Omary
19 April 2011

Dar Es Salaam Tanzania mainland Vodacom Premier League champions Young Africans say they are ready to recruit Azam FC and national soccer team striker Mrisho Ngassa.

Chairman of the club's Competition Committee Seif Mohamed told The Citizen that Ngassa, who emerged last season's top scorer, is fit to play for his team in both international games and the Mainland Vodacom Premier League.



Mohamed said they were ready to discuss the matter with Azam FC officials if they were prepared in order to register the player in the Yanga team.

"As you know, we have just completed the league and managed to win the trophy.
We are supposed to recruit the best players ahead of the next season as well as international competitions.

"Every team would like to sign Ngassa, and Young Africans are among these teams," said Mohamed.

However, he explained that it was very early to discuss the matter because of Tanzania Football Federation (TFF) rules and regulations governing the registration exercise.



But that was their target although they neither discussed the matter with the player nor club officials.

"We are not ready to break the rules; we are waiting for the greenlight before starting to follow the procedures.

"We are aware that Ngassa has a contract with Azam FC which is yet to expire," he said.

Mohamed also said the club has managed to extend their midfielder Nurdin Bakari's contract for one more season and dropped three foreign players, namely: Ernest Boakye, Isaac Boakye, both from Ghana, and Serbian goalkeeper, Ivan Knezevic.
"Their contracts have expired and we are not ready to continue with their services.

We informed them about the decision and they have already left the country," he said.

As for Shamte Ali and Athuman Idd Chuji, he said both have no contracts with the club, but their fate was with the team's head coach Sam Timbe, he said.
He explained that Timbe was yet to decide on the fate of the players and they were waiting to hear from him.

Meanwhile, the club is planning to hold a charity dinner to raise money for its development activities.

The gala is scheduled to take place on June 7 at a city hotel, according to the club chairman, Lloyd Nchunga.

He said they target to raise betweenm four and six billion shillings from the dinner.
 


Tuesday, 19 April 2011 19:23 newsroom


*Mwanchama mwingine ajitolea kumrejesha Ngasa

Na Mwandishi Wetu

MFADHILI wa zamani wa klabu ya Yanga,Yussuf Manji, amemwaga kitita cha sh. milioni 100 kusaidia usajili wa wachezaji msimu ujao. Habari za uhakika zilizopatikana kutoka klabu hiyo, zimesema Manji alikabidhi fedha hizo wiki iliyopita. Kwa mujibu wa habari hizo zilizothibitishwa na kiongozi moja wa Kamati ya Usajili ya Yanga, fedha hizo zimeshaanza kutumika kwa kazi iliyokusudiwa.

"Kamati ya Usajili imeanza kutumia pesa hizo kwa kuwasajili wachezaji wapya na wengine wa zamani, watakaoichezea timu hiyo msimu ujao."Habari hizo zimeeleza kati ya wachezaji ambao wametua Jangwani baada ya kutolewa pesa hizo, ni kipa wa Majimaji, Said Mohamed na Nurdin Bakari. Bakari alimaliza mkataba wake wa kwanza na Yanga na hivi karibuni ameingia mkataba mpya wa miaka miwili na klabu hiyo, na kuzima ndoto za Azam kumpata mchezaji huyo.

Manji ametoa pesa hizo akiwa mwanachama wa klabu hiyo kongwe na sio kama mfadhili, baada ya kujitoa kuifadhili hivi karibuni.

Habari zaidi zimesema mwanachama mwingine wa klabu hiyo, amejitolea kutoa pesa zote za kuilipa timu ya Azam, imwachie mshambuliaji Mrisho Ngasa arejee kuichezea timu hiyo ya Jangwani.

Mwanachama huyo (jina tunalo) ambaye hakutaka jina lake litangazwe, amekubali kutoa pesa zitakazowezesha Azam kumwacha Ngasa, aichezee tena Yanga katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mwakani.

Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, alipoulizwa jana juu ya masuala hayo, alikiri kuwepo mipango ya kutaka kumrejesha Ngasa ingawa hakuwa tayari kuzungumzia zaidi jambo hilo.

Ngasa alitua Azam mwanzoni mwa msimu uliomalizika hivi karibuni kwa uhamisho wa kitita cha karibu sh. milioni 100.

Uongozi wa Azam umeshasema iwapo Yanga inamtaka kumrejesha mchezaji huyo, uende kuzungumza nao.

Alipoulizwa jana, Mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed, alieleza klabu yake haipo tayari kumwachia mchezaji huyo, lakini amewataka viongozi wa Yanga kwenda kukutana nao kwa ajili ya majadiliano.

"Milango iko wazi, kama wanamtaka Ngasa waje tuzungumze, lakini sipendi kuzungumzia mambo katika vyombo vya habari, kwa nini wao hawaji kama kweli wana nia hiyo," alihoji kiongozi huyo wa Azam.
 
...Ngassa alipotea njia,rudi kundini fasta...
 
kwani timbe yuko wapi, au nae ni mjumbe wa kamati ya usajili?
 
Back
Top Bottom