Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

dar+young+african.jpg


yanga kesho watainama kama hao mstari wa mbele simba wataingiza ma goal.
 
Mie kesho nitakuwa online wakati wa halftime na baada ya mechi, nitakuwa busy utadhan mimi ndo msaidizi wa Basena na humu JF ingekuwa ni kwa sauti kesho baada ya mechi nisingeweza kuongea maana sauti inaweza isitoke ni kushangilia hadi mwisho kama mashabiki wa liverpool.

Tunataka tuwakumbushe miaka ya 2000 hadi 2009 mlipokuwa mnachezea kichapo .
 
Mnalo kesho....Chama letu litakuwa hivi hiyo kesho....1. Yaw Berko2. Shadrack Nsajigwa 'Fuso'3. Oscar Joshua4. Chacha Marwa 'Muraa'5. Nadir Haroub 'Cannavaro'6. Juma Seif 'Kijiko'7. Godfrey Taita8. Nurudin Bakari9. Davies Mwape10. Jerry Tegete11. Kigi Makassy
hahahhaha!!!! Sijaona kitu hapa.. Kesho hakuna penalt ya kupewa.
 
nyie dogo mishikaki (mnyama) ya msimbazi.... embu shikeni adabu kwa wakubwa zenu ebo!!

angalieni stats hizi hapa chini kwa mataji makubwa hapa nchini na EA:

mishikaki ya msimbazi = 23 trophies (TZ championship 17 + EA championship 6)
yanga afrika = 26 (TZ championship 23 + EA championship 3)
 
July 19, 1977 : Simba 6 Yanga 0. WAFUNGAJI: Abdallah Kibadeni (3) dk. 10, 42 na 89, Jumanne Hassan 'Masimenti' (3) dk. 60 na 73, Selemani Sanga alijifunga dk. 20. Kumbukeni hii mechi inachezwa July pia
Wakumbuke pia tar 2 July 1994...Simba 4 Yanga 1!!!
 
Yanga Daima Mbele.......Nyuma MwikoYanga Imara..........Yanga Daima
 
hahahhhahmkuu Balantanda umeiona hii?
Hahaaaaaaaaaaaa........Simba kwa Historia tu hatuwawezi.....Lol........Na hii je,Juni 01, 1968 Yanga Vs Sunderland 5-0......Wafungaji: Maulid Dilunga dk. 18 (penalti), Dilunga dk. 43, Salehe Zimbwe dk. 54, Zimbwe dk. 89, Kitwana Manara dk. 86.
 
hahahhaha!!!! Sijaona kitu hapa.. Kesho hakuna penalt ya kupewa.
Hebu nipe kikosi chenu cha kesho basi.......Btw.....Kuna tetesi kwamba Jerry Santo,Juma Kaseja na Amir Maftah hawachezi kesho sababu wana kadi mbilimbili za njano,ya kweli hayo?......Pia Mohamed Banka bado ni majeruhi,anaweza asicheze kesho.........Hahaaaaaaa.....'Maumivu ya kichwa huanza poooooooole pole'........
 
Mnalo kesho....Chama letu litakuwa hivi hiyo kesho....1. Yaw Berko2. Shadrack Nsajigwa 'Fuso'3. Oscar Joshua4. Chacha Marwa 'Muraa'5. Nadir Haroub 'Cannavaro'6. Juma Seif 'Kijiko'7. Godfrey Taita8. Nurudin Bakari9. Davies Mwape10. Jerry Tegete11. EDIBILY JONAS LUNYAMILA
Hapo 11 hapo!
 
Nilisikia mtangazaji wa star tv anasema Chacha Marwa ''Muraa&'' ni mnyeramba wa Singida nikachoka kabisa. Au ni yale mambo ya kununua jina kama ya mh. HK?
 
Back
Top Bottom