Shadeeya
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 49,759
- 118,798
Juma Mahadhi ametaja sababu za kuto onekana Morogoro
.
.
Winga Juma Mahadhi ni miongoni mwa wachezaji watakaoendelea kukipiga Jangwani baada ya uongozi wa Yanga kumuongeza mkataba
Hata hivyo 'kiberenge' huyo bado hajaonekana uwanjani wakati wenzie wanaendelea kujifua mkoani Morogoro
Msimu mzima uliopita Mahadhi hakupiga kabisa 'gozi la ng'ombe' baada ya kuvunjika mguu kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger
Mahadhi amefichua kuwa sio muda mrefu ataonekana dimbani baada ya kupona majeraha hayo "Kwa sasa nimepona kwa kiasi kikubwa, wanayanga wawe na subira kidogo siku sio nyingi wataniona uwanjani" amesema
Licha ya kutoonekana uwanjani kwa muda mrefu, kocha Mwinyi Zahera ameonyesha kuwa na imani nae na kupendekeza aongezwe mkataba
Mahadhi alitua Yanga misimu mitatu iliyopita akitokea klabu ya Coastal Union .