NYOTA WA ZAMANI YANGA KUONGEZA NGUVU .
.
.
Nyota waliowahi kutamba na kikosi cha Yanga miaka ya nyuma wanatarajiwa kukutana na wachezaji wa timu hiyo kuwapa hamasa kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United
Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam mwanzoni mwa wiki ijayo kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Septemba 28 uwaja wa Levy Mwanawasa, Ndola, Zambia
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa Sam Mwaitenda alisema wachezaji hao watawaongezea morali ya kufanya vizuri huko Zambia
Yanga pia imetoa fursa kwa mashabiki wake kuongozana na timu nchini Zambia kuhakikisha kikosi kinapata sapoti ya kutosha siku ya mchezo
Katibu wa kamati ya Hamasa Deo Mutta alisema safari ya mashabiki hao kuelekea Ndola itakuwa na sura tofauti kwa makundi ambayo yataanzia ya yale ya Nyanda za juu Kusini Iringa, Songwe, Njombe na Mbeya ambao safari yao itanzia Tunduma kuelekea Ndola huku gharama ikiwa Sh 110,000 kwa kwenda na kurudi.
Mutta alisema kwa mikoa mingine ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani gharama za safari itakuwa ni Sh 200000 kwa kila kitu kasoro chakula na malazi.
Alisema kwa wanachama wenye hati ya kusafiria,hati ya chanjo gharama yao itakuwa ni Sh 150,000 ambapo wote watakaohitaji kwenda wanatakiwa kukamilisha malipo kabla ya Septemba 22,2019 huku safari ilitarajiwa kuanza Septemba 25.