Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20200107_065440.jpg
 
MWAMUZI JONESIA: Ile ya Kagere haikuwa cheni

Mwamuzi Jonesia Rukyaa aliyechezesha pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga amesema kile alichokichukua kwa mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere hakikuwa cheni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam siku moja baada ya mchezo huo Jonesia alisema alielezwa na wachezaji wa Yanga kwamba Kagere ana kitu kisichoruhusiwa kimichezo na alipomfuata akakichukua na kukitoa nje kwa Kamisaa. "Ile haikuwa cheni kwa sababu cheni nazijua. Wengine wanasema eti ilikuwa hirizi. Mimi sizijui hirizi kwa hiyo sio rahisi kukiri kwamba ilikuwa hirizi", alisema Jonesia. "Mimi sipendi maswali mengi, labda mkamuulize mwenyewe Kagere. Kwanza hata sikuwa na muda wa kukichunguza. Alivyonipa tu nilikimbilia kukitoa nje haraka ili tuendelee na mchezo.", alisema.

Kumekuwa na mjadala mrefu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kifaa alichokutwa nacho Meddie Kagere ambacho kilitolewa nje na mwamuzi wengi wakisema ni hirizi wengine wakisema ni cheni.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), huenda likatoa ufafanuzi juu ya kifaa hicho kwa sababu kilikabidhiwa kwa Kamisaa na kwa vyovyote vile, kwa taratibu za mpira wa miguu, kitakuwa ni sehemu ya ripoti ya Kamisaa kuhusu mchezo huo.
 
Back
Top Bottom