Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Huyu Fundi kama anaweza kuupanda mpira namna hii huku akifanya movement akikutana na vijitu kama viwawa na vinyoni na vyenyewe si atavipanda tu!?
 

Attachments

  • VID-20200123-WA0033.mp4
    516.9 KB
YANGA KUREJEA DAR KUIWINDA PRISON.

Jumapili ya Januari 26 2020 kwenye uwanja wa Uhuru, kikosi cha Yanga kitashuka dimbani kuikaribisha Tanzania Prisons katika mchezo wa raundi ya nne kombe la FA (ASFC).

Timu hizo zinakutana kwa mara ya pili msimu huu, Yanga ikishinda kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu uliozikutanisha timu hizo mkoani Iringa.

Wakati kikosi cha Tanzania Prisons kikiwa hakina mabadiliko, hali itakuwa tofauti kwa Yanga iliyosukwa upya katika usajili wa dirisha dogo.

Wachezaji wapya saba wameongezwa Yanga huku wengine sita wakionyeshwa mlango wa kutokea.

Maboresho hayo yameiongezea Yanga makali, sasa ikicheza kandanda la kushambulia muda mwingi tangu ujio wa kocha Luc Eymael.

Yanga inatokea mkoani Singida ambako jana ilipata ushindi wa mabao 3-1 huku kiungo wake mshambuliaji Bernard Morrison aliyetua wiki iliyopita akiwaongezea makali mabingwa hao wa kihistoria.

Baada ya kukosa taji lolote kwa misimu miwili, Yanga imedhamiria kuondoka na taji msimu huu hesabu kali zikipigwa kwa taji hili la FA na ligi kuu.

Ushindi katika mchezo huo utawahakikishia kutinga hatua ya 16 bora mchezo mmoja kuelekea hatua ya robo fainali.

@Yangafulldozz
 
Huyu Fundi kama anaweza kuupanda mpira namna hii huku akifanya movement akikutana na vijitu kama viwawa na vinyoni na vyenyewe si atavipanda tu!?
Yaani huyu jamaa sio siri majuzi alinisurprise kwani sikutarajia kile kiwango.

Hata zile kona alizokuwa anapiga nyingi zilikuwa na macho.
 
MAZOEZI YA TIMU YA WANANCHI JANA KUJIANDAA NA PRISONS HAPO JUMAPILI KOMBE LA ASFC.

20200125_065908.jpg
 
Nimeangalia video youtube huyu jamaa ni balaa sana,nawapa heko viongozi waliofanikisha kumleta ni rahis kuongeza morale kwenye timu ukiwa na mtu kama huyu ,

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida ni kwamba je tutaweza kuendeleza uwezo wake, au ndo tutashindwa kumhendo mwishowe aanze kuanguka kama Feisal na makame? Mana hawa wachezaji huwa naamini wana uwezo Mkubwa sana ila wamekosa watu sahihi Wa kuwaendeleza uwezo walionao
 
Back
Top Bottom