Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20200129_161343.jpg

YANGA YAPELEKA MALALAMIKO BODI YA LIGI JUU YA FAINI WALIZOPIGWA

Uongozi wa klabu ya Yanga umepeleka malalamiko Bodi ya ligi (TPLB) juu ya faini walizopewa katika mechi zao zilizochezwa mwezi uliopita kutokana na kutoridhishwa na jinsi hatua hizo zilivyo chukuliwa dhidi yao.

Ofisa habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli amesema kuhusu kupigwa faini ya shilingi laki tano kutokana na kuto wasilisha majina ya wachezaji katika kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons msemaji huyo amebainisha kuwa walipeleka kwa kuchelewa kwakua mechi ilihamishwa ghafla kutoka uwanja Sokoine kwenda Samora, Iringa baada ya kutokuwa tayari kuchezewa baada ya mvua kunyesha.

Kuhusu faini ya shilingi laki mbili kwa kutoingia kwenye vyumba rasmi katika mchezo dhidi ya Simba msemaji huyo alisema walipeleka malalamiko Bodi ya ligi kuwa vyumba vyao havikuwa salama na wakaruhusiwa kuingia katika vyumba vya timu B lakini wameshangaa kuona wamepigwa faini hiyo.

Pia kuhusu mashabiki wao kurusha chupa za maji katika mchezo huo ni kutokana na wao kupeleka malalamiko Bodi ya juu ya mambo mbalimbali ambayo wanaona wanaonewa.

Bumbuli ameongeza kuwa wanashangaa Bodi hiyo kuzuia pesa kutoka kwa mdhamini Vodacom bila kufanya majadiliano na klabu hiyo kitu ambacho ni kinyume na kanuni ambazo wameziweka wenyewe.

@Yangasoccer
 
Sasa kanuni mnazijua maana toka ligi inaanza ndio zinazotumika, na vilabu vinashirikishwa katika utungaji wake. Mkifanya makosa zikiwabana mnalalamika tena!!!! Chura FC bana, kama watoto wadogo vile😀😀😀
 
BODI YA LIGI YAONYA WAAMUZI

Bodi ya ligi (TPLB) imetoa onyo kwa waamuzi watatu kutokana na kushindwa kufuata sheria 17 za mpira wa miguu katika mechi walizo chezesha.

Mwamuzi Florentina Zablon aliyechezesha mchezo namba 17 kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga katika uwanja wa Sokoine amepewa onyo kali kutokana na kushindwa kutafsiri sheria licha ya uwanja kujaa maji kutokana na mvua kubwa kunyesha jijini Mbeya.

Mwanamama huyo pia ndiye aliyechezesha mchezo wa jana wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Namungo Fc

Mwamuzi Jonesi Rukya na msaidizi wake Soud Lilla nao wamepewa onyo kali baada ya kushindwa kuona baadhi ya matukio katika mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Taifa, Januari 4.

Maamuzi hayo yametangazwa mbele ya vyombo vya habari na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya ligi, Ibrahim Mwanyela katika ofisi za Shirikisho la soka Tanzania (TFF) zilizopo Karume, Dar es Salaam.

@Yangafulldozz
 
SAA NYINGINE HIVI TUNAVIITA VICHEKESHO. INAKUWAJE KUPITIWA. 🤔🤔

👇👇👇

BODI YA LIGI YAKIRI KUPITIWA KUTOIPANGIA YANGA MECHI

Mwenyekiti wa Bodi ya ligi Steven Mguto amekiri kuwa vijana wake walijisahau kutoipangia Yanga mechi katikati ya wiki hii baada ya kucheza na Prisons mchezo wa kombe la FA Jumapili.

Akihojiwa na eFM radio mapema leo, Mguto amesema Yanga walipaswa kucheza mechi katikati ya wiki kama zilivyo timu nyingine

Hata hivyo amewalaumu viongozi wa Yanga kuwa nao walipaswa kuwakumbusha !
Pamoja na kuwa na michezo pungufu kuliko timu nyingine, Yanga haikupangiwa mechi mpaka Jumapili ijayo watakapocheza na Mtibwa Sugar ambayo leo iko uwanjani kuumana na Azam Fc.

@Yangafulldozz.
 
SAA NYINGINE HIVI TUNAVIITA VICHEKESHO. INAKUWAJE KUPITIWA. [emoji848][emoji848]

[emoji116][emoji116][emoji116]

BODI YA LIGI YAKIRI KUPITIWA KUTOIPANGIA YANGA MECHI

Mwenyekiti wa Bodi ya ligi Steven Mguto amekiri kuwa vijana wake walijisahau kutoipangia Yanga mechi katikati ya wiki hii baada ya kucheza na Prisons mchezo wa kombe la FA Jumapili.

Akihojiwa na eFM radio mapema leo, Mguto amesema Yanga walipaswa kucheza mechi katikati ya wiki kama zilivyo timu nyingine

Hata hivyo amewalaumu viongozi wa Yanga kuwa nao walipaswa kuwakumbusha !
Pamoja na kuwa na michezo pungufu kuliko timu nyingine, Yanga haikupangiwa mechi mpaka Jumapili ijayo watakapocheza na Mtibwa Sugar ambayo leo iko uwanjani kuumana na Azam Fc.

@Yangafulldozz.
Huyo m/kiti na yeye hana akili, kosa lao wenyewe halafu lawama zinakua kwetu, kwani wakati anachukua mshahara wake hua anasubiri yanga tumkumbushe kuuchukua, bwege kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si ndio hapo Mkuu. Yaani eti hujapangwa halafu ukumbushe. Aiseee. Taratibu za wapi hizo.

Na kwa ukubwa wa timu ya Yanga sio ya kusahaulika. Wana yao tu hao sio bure.
 
Kusema kweli kwa kauli hiyo ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi ilitakiwa amaliziea kwa kauli ya kuachia ngazi!
 
Hii ndiyo Tanzania

"Kiukweli mimi na vijana wangu tulipitiwa (kuwasahau) kuwapangia Yanga SC mchezo toka wacheze mchezo wa FA dhidi ya Prisons, Yanga nao walipaswa kutukumbusha kupangiwa mechi"

Steven Mguto (Mwenyekiti bodi ya ligi)
FB_IMG_1580404148356.jpg
 
Hii ndiyo Tanzania

"Kiukweli mimi na vijana wangu tulipitiwa (kuwasahau) kuwapangia Yanga SC mchezo toka wacheze mchezo wa FA dhidi ya Prisons, Yanga nao walipaswa kutukumbusha kupangiwa mechi"

Steven Mguto (Mwenyekiti bodi ya ligi)View attachment 1341422
Wana lao tu waliwekage wazi sababu kwa hali hii tutakuja jikuta leo tunacheza Arusha kesho kutwa Iringa. Ili mradi tu huku wakidai muda hautoshi.
 
Hii ndiyo Tanzania

"Kiukweli mimi na vijana wangu tulipitiwa (kuwasahau) kuwapangia Yanga SC mchezo toka wacheze mchezo wa FA dhidi ya Prisons, Yanga nao walipaswa kutukumbusha kupangiwa mechi"

Steven Mguto (Mwenyekiti bodi ya ligi)View attachment 1341422
Halafu niliwahi kusikia yule Mwenyekiti wetu Msola kwamba kawa mmoja wa Wanakamati za huko TFF ni ipi vile? 🤔🤔🤔

Au nimechanganya madawa?
 
Hii ndiyo Tanzania

"Kiukweli mimi na vijana wangu tulipitiwa (kuwasahau) kuwapangia Yanga SC mchezo toka wacheze mchezo wa FA dhidi ya Prisons, Yanga nao walipaswa kutukumbusha kupangiwa mechi"

Steven Mguto (Mwenyekiti bodi ya ligi)View attachment 1341422
Ki ukweli ni kwamba Kuna kaupendeleo fulani ka kupendelea timu fulani hivi, ili tu yanga ionekane hakuna kitu pale, Lakini ukweli utajulikana tu, huwezi kusema yanga waikumbushe TFF, Hayo ni masihara kabisa.

Sent from my Infinix-X551 using Tapatalk
 
Kauli tu hiyo ilifaa ajiuzulu Ila Karia anambeba wanatoka Tanga wote na ndiyo maana alimteua kuwa makamu mwenyekiti na wote ni Simba lialia
 
20200201_070618.jpg

MAHADHI TAYARI KURUDI DIMBANI

Baada ya kuwa nje ya dimba kwa zaidi ya miezi 18 kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti, kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi ataanza kuonekana kikosini siku sio nyingi

Mahadhi amepona majeraha na tayari ameanza mazoezi mepesi

Ni baada ya jitihada kubwa kufanyika kumrejesha dimbani tangu alipopata majeraha Agost 18 2018

Mahadhi alifanyiwa upasuaji wa goti mara mbili, akianza kutibiwa Hospitali ya Muhimbili na baadae kupelekwa nchini India

Karibu tena Mahadhi...!

@Yangafulldozz
 
20200201_071836.jpg

NI YANGA SC VS MTIBWA SUGAR, JUMAPILI HII UWANJA WA TAIFA

Baada ya kusahauliwa kupangiwa mechi na Bodi ya Ligi, hatimaye kikosi cha Yanga kitashuka dimbani siku ya Jumapili Februari 02 kuikaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Taifa.

Hii ni siku nyingine kwa mashabiki wa Yanga kupata burudani kutoka kwa vijana wao wakiongozwa na Bernard Morrison ambaye ni habari ya mjini kwa sasa.

Mtibwa Sugar wamecheza na Azam Fc juzi na kufanikiwa kupata sare ya bao 1-1

Viingilio vya mchezo wa Jumapili, VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- wakati Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
 
Back
Top Bottom