Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

View attachment 1342913

MAHADHI TAYARI KURUDI DIMBANI

Baada ya kuwa nje ya dimba kwa zaidi ya miezi 18 kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti, kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi ataanza kuonekana kikosini siku sio nyingi

Mahadhi amepona majeraha na tayari ameanza mazoezi mepesi

Ni baada ya jitihada kubwa kufanyika kumrejesha dimbani tangu alipopata majeraha Agost 18 2018

Mahadhi alifanyiwa upasuaji wa goti mara mbili, akianza kutibiwa Hospitali ya Muhimbili na baadae kupelekwa nchini India

Karibu tena Mahadhi...!

@Yangafulldozz
Ila goti likishaguswa maisha ya kucheza soka yanakua mashakani. Wengi waliopatwa na changamoto hiyo wakirudi dimbani wanakua hawachezi kwa viwango vyao vya awali na pia ni rahisi kujitonesha tena. Tunamuombea kila la heri na afya njema
 
HAKUNA MCHEZAJI MKUBWA KULIKO YANGA - EYMAEL

“ Yondani alisema hawezi kucheza dhidi ya Azam, alidai anasumbuliwa na tumbo, baada ya hapo sijui nini kilitokea. Kwa siku sita siku simu yake ilikuwa imezimwa. Tulishindwa kuwasiliana naye kumpa taarifa za kwenda Singida. Baadaye alirejea klabuni na kusema anajisikia vizuri”

“Lazima watu wakubali kuwa tunatakiwa kwenda kwa mstari mmoja, sipangi jina, nachezesha timu. Hakuna aliye mkubwa kuliko timu. Sote tutapita hapa, Yanga itabaki hapa.”

Kocha wa Yanga, Luc Eymael akisisitiza hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya Yanga baada ya Yondani ‘kupotea’ klabuni kwa siku sita na kulazimika kumtumia Juma Makapu kama beki wa kati katika mechi dhidi ya Singida na Prisons.

@Yangadaima
Kama kweli kelvin alifanya hivyo mwalimu yupo sahihi,kazi kwa mazoea inabidi zife. Labda kama anadai kama zamani
 
Ni kweli yanaweza yakaisha juu juu ila binafsi siamini kama tuhuma ni za kweli.

Hahaha jina linasomeka hivi 'twaiziem' hicho ni kifaransa
Troisième Ceil = Third Eye
Simba kama alichosema kabwili ni uongo wamfungulie mashitaka ili uchunguzi uanze. Mana kawachafua sana. Na simba isipomshitaki kabwili tutajua ni kweli
 
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison amesema anapofanya mbwembwe uwanjani halengi kuwadhihaki timu pinzani bali ni mahsusi kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki ambao wamelipa viingilio kuingia uwanjani

Aidha Bernard ameongeza kuwa hatafanya matukio hayo wakati wote, isipokuwa pale ambapo timu iko kwenye mazingira ya uhakika wa kuondoka na ushindi

Morrison ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kocha Luc Eymael kueleza kutofurahishwa na matukio hayo ambayo aliyafananisha na dhihaka kwa timu pinzani "Mashabiki wanakuja uwanjani kuona timu yao inashinda, ndio maana wanalipa viingilio, lakini ninapoona timu inaongoza vizuri huwa naona ni bora kufanya kitu ambacho kitawapa burudani zaidi mashabiki wakienda nyumbani wapate cha kusimulia zaidi," amefafanua Morrison. "Nafikiri kocha yeyote hawezi kukubali hilo moja kwa moja, namheshimu kocha wangu (Eymael) kwa alichoniambia, lakini kwangu nafikiri kuna kitu cha ziada natakiwa kukifanya kama mchezaji, sidhani kama naweza kuacha lakini nitakuwa makini wakati gani nafanya hivyo"

@Yangadaima
Sawa,ila tutakapowafunga simba kwenye game ya pili apige tu mbwembwe kuanzia sekunde yabkwanza hadi mwisho. Na ikibidi atembee juu ya vichwa vya kina nyoni na wawa, ha ha ha
 
NI YANGA SC VS MTIBWA SUGAR, JUMAPILI HII UWANJA WA TAIFA

Baada ya kusahauliwa kupangiwa mechi na Bodi ya Ligi, hatimaye kikosi cha Yanga kitashuka dimbani siku ya Jumapili Februari 02 kuikaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Taifa.

Hii ni siku nyingine kwa mashabiki wa Yanga kupata burudani kutoka kwa vijana wao wakiongozwa na Bernard Morrison ambaye ni habari ya mjini kwa sasa.

Mtibwa Sugar wamecheza na Azam Fc juzi na kufanikiwa kupata sare ya bao 1-1

Viingilio vya mchezo wa Jumapili, VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- wakati Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Ilipo tupo......
 
HAKUNA MCHEZAJI MKUBWA KULIKO YANGA - EYMAEL

“ Yondani alisema hawezi kucheza dhidi ya Azam, alidai anasumbuliwa na tumbo, baada ya hapo sijui nini kilitokea. Kwa siku sita siku simu yake ilikuwa imezimwa. Tulishindwa kuwasiliana naye kumpa taarifa za kwenda Singida. Baadaye alirejea klabuni na kusema anajisikia vizuri”

“Lazima watu wakubali kuwa tunatakiwa kwenda kwa mstari mmoja, sipangi jina, nachezesha timu. Hakuna aliye mkubwa kuliko timu. Sote tutapita hapa, Yanga itabaki hapa.”

Kocha wa Yanga, Luc Eymael akisisitiza hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya Yanga baada ya Yondani ‘kupotea’ klabuni kwa siku sita na kulazimika kumtumia Juma Makapu kama beki wa kati katika mechi dhidi ya Singida na Prisons.

@Yangadaima
Ila Yondani amezidi sasa, sijui viongozi wanamchekea mana kila kocha lazima alalamike kuhusu tabia zake mbovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana lao tu waliwekage wazi sababu kwa hali hii tutakuja jikuta leo tunacheza Arusha kesho kutwa Iringa. Ili mradi tu huku wakidai muda hautoshi.
YANGA, MWEZI 1 MECHI 9

**RATIBA YA YANGA FEBRUARY**

1) 02/02/2020 Yanga SC vs Mtibwa Sugar-National Stadium 1600hrs;

2) 05/02/2020 Yanga SC vs Lipuli FC- National Stadium 1600 hrs;

3) 08/02/2020 Ruvu Shooting vs Yanga SC National Stadium 1900hrs;

4) 11/02/2020 Yanga SC vs Mbeya City- National Stadium 19:00hrs

5) 15/02/2020 Young vs Tanzania Prisons National Stadium 1900hrs;

6) 18/02/2020 Police Tanzania vs Yanga SC- Ushirika Stadium, Kilimanjaro, 1600hrs;

7) 23/02/2020 Coastal Union vs Yanga Mkwakwani Stadium, Tanga 16:00hrs

8) 25 or 26/02/2020 Yanga SC vs Gwambina FC (FA);

9) 29/02/2020 Yanga SC vs Alliance FC, National Stadium, 1600hrs;

Mwezi February una jumla ya Mechi tisa, Sita-Mwenyeji, Tatu-Ugenini

HATIMAYE BODI IMEWAKUMBUKA

*Nlitaka nishangae yani tff waisahau yanga kwenye ratiba kweli!? Wamejifanya kutusahau kumbe wanajua mkakati walopanga wa kuimaliza Yanga. Pumbavu zao na tutatoboa tu.* *Hiyo timu yao pendwa wanayoibeba itawaumbua tu!*
 
Ila goti likishaguswa maisha ya kucheza soka yanakua mashakani. Wengi waliopatwa na changamoto hiyo wakirudi dimbani wanakua hawachezi kwa viwango vyao vya awali na pia ni rahisi kujitonesha tena. Tunamuombea kila la heri na afya njema
Kweli usemalo ila kama usemavyo tumuombee sababu ndio ajira yake ile.
 
Back
Top Bottom