Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Hahahaaa. Anajitoa ufahamu tu huyo.

Uzi una miaka zaidi ya 11 ndio anauona leo si visa hivyo.
Ndio nimeuona Leo mkuu Kwa hiyo miaka kumi na moja mnasoma tu mnapita!?Rage kuja huku lile jina ulikosea kubatiza,wa kubatizwa alikuwa mwingine!?
 
Team yetu kiukwel tukiweza kucheza kwa speed ambayo huwa tunacheza kipindi cha kwanza hakika wapinzani watakunywa sana sparleta bar ila na mastriker wetu nao wanatakiwa wajitafakari zile nafas wanazoshindwa kuzitumia kikamilifu
 
20200211_070105.jpg

HAPPY BIRTHDAY YOUNG AFRICANS SC ..... 85 yrs

February 11, 1935 - February 11, 2020


Vikombe 27 ligi kuu Tanzania bara.
Vikombe 5 Kagame.
1998 kufuzu hatua ya makundi klabu bingwa Afrika.
1970 Robo fainali CAF Champions league.
2016 hatua ya makundi Shirikisho Afrika.
2018 hatua ya makundi Shirikisho Afrika.
1995 Robo fainali kombe la washindi barani Afrika ( limefutwa kwa sasa )

Records za kukumbukwa .
Ushindi mfululizo wa miaka mitano ligi daraja la kwanza Tanzania ( sasa ligi kuu Tanzania bara ) 1968, 1969 , 1970 , 1971 na 1972 .

Yanga SC ilipanda rasmi ligi daraja la kwanza ( sasa ligi kuu ) mwaka 1936 hivyo ina miaka 84 kwenye ligi husika bila kushuka .


Young_Africans_SC_(logo).png
 
muda wa mwisho ilikuwa saa nne na dakika kumi na saba asubuhi ya tarehe 11.02.2020 nyie vyura mna fail wapi shadeeya mpo au jana Mbeya city alimnunua lamine moro
 
20200215_112633.jpg
NCHIMBI AFURAHIA KUCHEZA NA MOLINGA

Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi, amemtaja David Molinga kuwa ndiye anayempa raha kila wanapocheza pamoja, ikiwa ni baada ya kutengeneza pacha hatari hivi karibuni

Tangu aliposajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili mwezi uliopita, Nchimbi ameonekana kuelewana vilivyo na straika Mkongo, Molinga, wakiisaidia timu yao hiyo kuendelea kukusanya pointi msimu huu.

Kombinesheni yao ilianza kuonekana katika mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga na Mtibwa Sugar, Nchimbi akitoa asisti tamu kwa Molinga, pia, alikuja kufanya hivyo tena Wanajangwani walipomenyana na Ruvu Shooting.

Nchimbi maarufu kama Duma, amesema baada ya kucheza michezo michache sambamba na Molinga ameanza kuielewa mikimbio ya mshambuliaji mwenzake huyo na jinsi gani ya kumpenyezea pasi za kufunga mabao. "Nafurahi mno ninapocheza na Molinga. Sasa nafahamu ni aina gani ya pasi za kumpenyezea na katika mazingira yapi ili aweze kufunga mabao. "Uzuri ni kwamba Molinga ana uelewa mkubwa wa mchezo wa soka, hata kama hana kasi, lakini anajua aina ya pasi ninazomletea njiani kutokana na mimi pia nimeshafahamu nimchezeshe vipi"

Tangu ajiunge na Yanga, Nchimbi bado hajafanikiwa kuifungia bao, lakini uwezo wake wa kukaba na kukokota mpira unaonekana kuwa na faida ndani ya timu hiyo kupitia kwa wachezaji wenzake

Leo Jumamosi Yanga itashuka dimba la Taifa kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu mzunguuko wa 22

Yanga ilishinda bao 1-0 katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliopigwa mkoani Iringa

Baadae ikashinda 2-0 kwenye mchezo wa kombe la FA hatua ya 32 bora

Bila shaka Molinga na Nchimbi watajumuishwa kwenye kikosi kitakachoshuka dimbani
 
20200215_112754.jpg
NATAKA KUIRUDISHA NAMBA YANGU 'YONDANI'

Beki mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani amesema kuwa anafahamu alipoteza namba katika kikosi cha kwanza katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu Bara na sasa amerudi upya huku akiwataka mashabiki wa timu hiyo kupata soka safi kutoka kwake.

Awali, beki huyo alikuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mbelgiji Luc Eymael kwa kile kilichoelezwa kuonyesha nidhamu mbaya kwa kutoonekana mazoezini kwa siku tatu huku simu yake ikiwa imezimwa na baadaye kurejea kikosini na kuondolewa.

Beki huyo baadaye alirejeshwa kikosini, lakini hakuwa anapata nafasi ya kucheza huku nafasi yake ikichezwa na Juma Makapu, kabla ya juzi kurejea uwanjani katika mchezo wa ligi walipocheza na Mbeya City na kutoka sare ya 1-1.

Yondani alisema: “Nikwambie tu ili timu iwe bora lazima kila nafasi iwe na ushindani, hii ni funzo kwangu kuendelea kujituma na kuhakikisha napata nafasi yakucheza mara kwa mara kwani ndicho kilichonileta Yanga. “Katika nafasi hii ninayocheza wachezaji wote waliokuwepo wana uwezo wa kucheza, kikubwa kinachotakiwa kwangu ni kutimiza majukumu nitakayopewa ya kuokoa na kupunguza hatari golini kwetu,” alisema Yondani.

@Yangafulldozz
 
Back
Top Bottom