Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

*MAISHA YANA KWENDA KASI SANA YANI SIMBA LEO ETI ANA TAMANI ANGEKUA NDO KMC🤣🤣🤣*
 
LUC EYMAEL AMEANZA KUPIGA HESABU ZA MSIMU UJAO

Mabadiliko ya kikosi na benchi la ufundi, inaweza kuwa sababu ya kuifanya Yanga isiwe na mwendelezo mzuri.

Tangu mwezi Juni mwaka jana, Yanga imesajili wachezaji 22 na kubadilisha benchi la ufundi mara tatu.

Sasa ili kuhakikisha msimu ujao timu inakuwa imara, uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wadhamini wao GSM, wamempa kocha Luc Eymael ruhusa ya kuanza kusaka wachezaji anaotaka wasajiliwe.

Kocha huyo ametakiwa kuangalia maeneo yenye mapungufu na sio kusajili timu nzima na bila mpango kama ilivyokuwa kwa Mwinyi Zahera.

Moja ya maeneo ambayo wanayanga watarajie kuona mabadiliko ni safu ya ushambuliaji. Washambuliaji David Molinga na Yikpe Gnamien wana uwezekano mdogo wa kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao.

Molinga alisajiliwa kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Renaissance, anatarajiwa kurejea kwenye klabu hiyo inayoshika nafasi ya tano Ligi Kuu ya DRC.

Kwa Gnamien mabosi wa Yanga watalazimika kuvunja mkataba wake kwani alisaini miaka miwili.

Eymael ameahidi kuwa ataleta washambuliaji ambao wataifanya safu ya ushambuliaji iwe moto wa kuotea mbali msimu ujao.

Amesema anawafahamu wachezaji wazuri ambao watain'garisha safu hiyo kwa kushirikiana na Bernard Morrison na washambuliaji wazawa.

Usajili wa Morrison ni pendekezo la Eymael Yanga ikimnasa Januari 15, siku ambayo dirisha dogo la usajili lilifungwa.

Habari njema ni kuwa Yanga inakaribia kubadili mfumo wake wa uendeshaji na pengine msimu ujao itakuwa mikononi mwa wawekezaji hivyo suala la kusajili wachezaji wakali halitakuwa tatizo kwani fedha itakuwepo.

Kuna uwezekano mkubwa GSM wakajitosa 'mazima' kuwekeza Yanga.

@Yangafulldozz
Kiukweli yule kocha Mimi nina imani nae sana labda uongozi tu wakati mwingine nauona kama umezubaa sana sijui nini kimetokea
 
WACHEZAJI HAWAKUJITUMA TANGU MAZOEZINI EYMAEL

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema alikuwa na hofu timu yake isingefanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya KMC jana baada ya kutoridhishwa na morali ya wachezaji mazoezini.

Akizungumza na wanahabari baada ya mchezo huo uliomalizka kwa Yanga kufungwa bao 1-0 na KMC, Eymael amesema wachezaji wake walijisahau baada ya ushindi dhidi ya Simba "Nilikuwa na wasiwasi kuelekea mchezo huu kwani sikuridhishwa na kile nilichokuwa nikikiona mazoezini," alisema Luc "Bahati mbaya kwa hapa Tanzania, timu ikishinda dabi wachezaji wanaona kama wametwaa kombe la dunia. Niliwatahadharisha wachezaji wangu kuhusu umuhimu wa kujituma ili kupta ushindi kwani mechi ya Simba haina tofauti na mechi nyingine zote tunasaka alama tatu" "Ni jambo baya sana kupoteza mchezo lakini wakati mwingine mambo haya hutokea, tunajipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata".

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea mkoani Lindi kesho tayari kwa mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumapili.
Jana wachezaji walinikera sana sana tena mno!
 
Jana wachezaji walinikera sana sana tena mno!
Yaani wacha tuitwage Utoporo tu, mi mwenyewe walinikera mbaya wenzao tulitaka tuendeleze furaha wao wanaleta masikhara. 😔

Kama Molinga kuna nafasi ya wazi aliipoteza kizembe sa sijui mawazo yake yalikuwa wapi sababu yale maamuzi ya haraka aliyakosa kabisa.
 
Yaani wacha tuitwage Utoporo tu, mi mwenyewe walinikera mbaya wenzao tulitaka tuendeleze furaha wao wanaleta masikhara. [emoji17]

Kama Molinga kuna nafasi ya wazi aliipoteza kizembe sa sijui mawazo yake yalikuwa wapi sababu yale maamuzi ya haraka aliyakosa kabisa.
Molinga uwezo Mdogo sana,hao ni aina ya wachezaji tunaopaswa kutemana nao siku ligi tu inapoisha
 
20200315_085856.jpg
 
Back
Top Bottom