Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Kama wametusikia vile Leo. Wajirekebishe sasa sehemu zote walizochemka!
20200320_180322.jpg

BRO NIMEI REPOST HII PICHA ILI NA WALE WAPENDA UZI WA TIMU YA WANANCHI WAIONE VIZURI. 😂😂😂
 
Bado kina Feisal sasa japo hawa si mpaka kipindi cha usajili kianze?

Au inawezekana kufanya nao mazungumzo kabisa?
 
KIPINDI HIKI KAMA MCHEZAJI UTAKOSA UMAKINI UBORA WAKO UNAWEZA UKAPUNGUA"NCHIMBI'

Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema atatumia kipindi hiki ambacho ligi imesimama kutokana na ugonjwa wa Corona kujiimarisha zaidi.

Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao sita kwenye ligi msimu huu, amesema pamoja na kutekeleza program ya mazoezi aliyoachiwa na kocha wake, ataongeza mazoezi binafsi ili kuhakikisha anakuwa timamu ligi itakaporejea.

Nchimbi amesema kama mchezaji mapumziko ya muda mrefu yanaweza kusababisha hata ukaongezeka uzito na baadae unaweza kushindwa kutimiza majukumu yako "Hiki kipindi kinaweza kutuharibu wachezaji wengi kwa sababu kwanza hatupo kambini kwa maana hata kama tutaenda mazoezini tutakuwa tunatokea katika familia zetu, huku aina ya vyakula tunavyokula vinaweza kuja kutuletea madhara pale ligi itakapoendelea. "Kama mchezaji asipokuwa makini kipindi hiki cha mwezi mzima, lazima atapata kitambi na kuongezeka uzito," alisema Nchimbi.
 
Inawezekana kufanya nao mazungumzo kabisa na hata kusaini kwa sababu ni mchezaji Wa ndani. Ila kasheshe ni viongozi kujiongeza. Kwa haya mambo ya kusubiri hadi mchezaji amalize mkataba wake tumepoteza wachezaji kama Gadiel Michael, Maka Edward dogo anacheza Serbia huko kama sikosei, Frank Domayo, Chirwa, Ninja, Haruna kipindi kile anaenda simba free n.k
 
KIPINDI HIKI KAMA MCHEZAJI UTAKOSA UMAKINI UBORA WAKO UNAWEZA UKAPUNGUA"NCHIMBI'

Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema atatumia kipindi hiki ambacho ligi imesimama kutokana na ugonjwa wa Corona kujiimarisha zaidi.

Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao sita kwenye ligi msimu huu, amesema pamoja na kutekeleza program ya mazoezi aliyoachiwa na kocha wake, ataongeza mazoezi binafsi ili kuhakikisha anakuwa timamu ligi itakaporejea.

Nchimbi amesema kama mchezaji mapumziko ya muda mrefu yanaweza kusababisha hata ukaongezeka uzito na baadae unaweza kushindwa kutimiza majukumu yako "Hiki kipindi kinaweza kutuharibu wachezaji wengi kwa sababu kwanza hatupo kambini kwa maana hata kama tutaenda mazoezini tutakuwa tunatokea katika familia zetu, huku aina ya vyakula tunavyokula vinaweza kuja kutuletea madhara pale ligi itakapoendelea. "Kama mchezaji asipokuwa makini kipindi hiki cha mwezi mzima, lazima atapata kitambi na kuongezeka uzito," alisema Nchimbi.
Angalau anajielewa kwa kutambua hili
 
NAFASI TULINAYO KWA SASA NI KOMBE LA ASF

Uongozi wa klabu ya Yanga jana ulikuwa na kikao cha kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu klabu hiyo

Pamoja na mambo mengine, mabosi hao wa Yanga waliandaa mkakati wa kuhakikisha timu inaweza kupata ushiriki wa michuano ya Kimataifa kwa kutwaa taji la FA timu ikiwa imetinga robo fainali.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wameweka malengo hayo baada ya kupoteza nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Msimu ujao ni timu mbili tu kutoka Tanzania zitashiriki michuano ya CAF baada ya Libya kuiondoa Tanzania nafasi ya 12 kwenye viwango vya CAF.

Aidha mabosi hao walijadili mpango mkakati wa usajili pamoja na kuwajadili nyota walioagizwa kuandika barua wakituhuma na makosa ya utovu wa nidhamu hasa baada ya kukosa safari Lindi.

Mwakalebela amesema kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael ametoa msamaha kwa wachezaji wote.
 
Hili kombe ni muhimu sana sana tena mno!!
 
Kwa nini tusiweze?
Timu yenu inasambaratika. Mnaanza kushikana uchawi wenyewe kwa wenyewe. Nni kamleta mchezaji gani, nani aachwe kwenye timu, mchezaji gani sijui anahujumu timu, basi vurugu moja kwa moja. Mtashinda vipi kwenye mazingira kama hayo?
 
Sasa tumefikaje hapo tulipo sasa?
 
Back
Top Bottom