Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

100% kuna mkono wa mikia
Kuumbe. Ila wanakeraga sana yaani kaona tunataka kusimama anaanza kusambaza habari za uongo. Aiseee.

Nauliza kwani hakuna hatua za kumchukulia mana nasikia ni Mwanachama.

Uongozi kuandika barua ya kukanusha pekee kwangu naona haisaidii.
Wakishirikiana na wale Yanga maslahi
 
Kuumbe. Ila wanakeraga sana yaani kaona tunataka kusimama anaanza kusambaza habari za uongo. Aiseee.

Nauliza kwani hakuna hatua za kumchukulia mana nasikia ni Mwanachama.

Uongozi kuandika barua ya kukanusha pekee kwangu naona haisaidii.
Kweli kama ni amedanganya basi achukuliwe hatua nasi tujue siyo kukanusha tu
 
Nataka kumwaga mchele humu, picha na jina la striker ambae ,timu za kariakoo zinataka kupiga hodi Congo ,inakataa
 
Haya haya ,naona timu za kariakoo mnataka kuipasua tp Mazembe na fc lupopo ,pamoja na As Vita Club

Leteni Makuta hayo ,mchukue Sentahafu huyo na striker
IMG-20200127-WA0026.jpeg
 
Kweli kama ni amedanganya basi achukuliwe hatua nasi tujue siyo kukanusha tu
Hakika usemalo.

Ila huu uongozi bana majuzi tu hapo kuna barua ilitembea ikimshutumu Bashite anahusika kuihujumu Timu ya Wananchi basi haikupita siku tayari uongozi ukakanusha tena kutokuhusika na hiyo barua.

Hivyo kama usemavyo kukanusha haisaidi kama hawatatafuta dawa kwa hao wachawi wetu.
 
MORRISON AWAAHIDI MAKUBWA WANA YANGA

Nyota wa Yanga ambaye kwa sasa ameiteka mioyo ya mashabiki, Bernard Morrison, amesema anafurahi kuona 'amekubalika' mapema ndani ya klabu hiyo na hali hiyo inampa nguvu ya kujipanga kufanya makubwa zaidi.

Wiki iliyopita Morrison alisaini mkataba mpya ambao utamuweka Jangwani kwa miaka miwili. Awali Morrison alikuwa akiwindwa na klabu ya Simba.

Morrison amesema ataongoza mapambano kuhakikisha wanashinda mechi zao za ligi zilizobakia na mashindano ya Kombe la FA.

Aidha, Mshambuliaji huyo amesema kuwa 'mapenzi' wanayopata wachezaji wa timu hiyo kutoka kwa mashabiki wa Yanga ni sababu inayowafanya wajitume katika kila mechi wanayocheza na kusahau changamoto zinazowakabili. "Ningependa kuwashukuru mashabiki kwa kunikubali, nimekuwa na wakati mzuri, nimekuwa nikipata zawadi mbalimbali kutokana na uchezaji wangu, hii inanifanya nijipange zaidi kuisaidia timu yangu, nimejifunza vitu vingi nilipokuwa Orlando Pirates," amesema Morrison. "Ninaheshimu ajira yangu ndani ya Yanga, nitaitumikia kwa nidhamu, mipango yangu ni kutimiza malengo yangu, lakini huu ni mpira, kwa sasa nitaelekeza nguvu na akili zangu Yanga".

20200316_151541.jpg

@Yangafulldozz
 
NINA MKATABA NA YANGA 'MAXIME

Kocha wa Kagera Sugar , Mecky Mexime amefichua kuwa anao mkataba na Yanga lakini bado hajasaini.

Mexime amebainisha kuwa alifanya mazungumzo na uongozi wa Yanga mwishoni mwa mwaka jana lakini kuna baadhi ya vipengele havikuwa vimewekwa sawa hivyo bado hajasaini mkataba huo wala kuurudisha.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa amesema haoni shida kuwa kocha msaidizi wa Yanga kama mambo yote yatawekwa sawa "Mimi kuwa kocha msaidizi wala sio kikubwa Maslahi ndio jambo kubwa na zuri kwangu,naangalia ninachopata Kagera na watakachonipa Yanga," amesema.

Kwa sasa Yanga inanolewa na Luc Eymael akiwa kocha Mkuu na Charles Mkwasa akiwa kocha msaidizi.

Mpango uliokuwepo awali Mexime angechukua nafasi ya Mkwasa ambaye angepandishwa cheo kuwa Mkurugenzi wa ufundi.

@Yangafulldozz
 
BARUA YA GSM KWENDA YANGA.

MWENYEKITI,
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB,
P.O.BOX 15202,
DAR ES SALAAM.

Ndugu. YAH:MKATABA WA YOUNG AFRICANS SPORTA CLUB NA GSM TANZANIA LIMITED.

Husika na kichwa cha habari hapo juu. Kwa heshima na taadhima nachukua fursa hii kuushukuru uongozi mzima wa Klabu yetu ya YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB "YANGA" TIMU YA WANANCHI kwa ushirika wenu kwenye mambo kadha wa kadha kwenye kuirudishia heshima na kutatua changamoto nyingi zilizokua zinaikabili Klabu yetu.

Ikumbukwe kuwa changamoto nyingi ziliikumba na kuendelea kuikabili timu yetu na sisi tulijitahidi kuzitatua ingawa hazikua sehemu ya mkataba wetu.
NAZO NI
1.Kumrudisha LAMINE baada ya kutukatiza mkataba wake.
2.Kusajili wachezaji katika kuiongezea nguvu klabu yetu. I.Bernad Morisson. II.Ditram Nchimbi III.Haruna Niyonzima IV.Adeyum Saleh
3.Kuwaleta na kulipa gharama zote za KOCHA MKUU,KOCHA WA MAZOEZI NA VIUNGO (FITNESS COACH na PHYSIO)gharama hizo ni pamoja na mishahara, nusafiri wa ndani,nyumba na ticket za kwenda na kurudi makwao(BELGIUM & SOUTH AFRICA). 4.Kulipa Mishahara.
5.Kulipa Bonas za ushindi ktk mechi zote timu iliposhinda kuanzia Mwezi Desemba 2019.Pamoja na ahadi kubwa ya ushindi kwa mechi dhidi ya watani wa jadi na kuitekeleza
baada ya ushindi huo.

5.Kulipa gharama zote za CAMP/HOTEL kwa timu kuanzia mwezi Desemba 2019.

6.Tiketi za ndege kwa wachezaji na viongozi.

7.Kulipa na kugharamia uwanja wa mazoezi kwa ukamilifu wake.Hii ni pamoja na ukarabati wa uwanja na ununuzi wa vifaa vya mazoezi.

8.Kulipa baadhi ya madeni ya nyuma ya usajili wa wachezaji. Aidha,yote hayo yamekua yakifanyika kwa MAPENZI MEMA kwa klabu yetu bila kujali gharama nyingi na kubwa tunazolipa.

Pia,Katika kuelekea mabadiliko ya kiundeshaji wa Klabu,GSM ilitafuta wataalam( CONSALTANT)kuja kushauri na kusaidia mabadiliko ya kimfumo pamoja na kupata TIMU kubwa barani ULAYA itakayokuja kuwa ni TIMU RAFIKI katika kukuza maendeleo ya idara zote katika Klabu yetu CONSULTANT huyo yuko tayari na TIMU hiyo pia iko tayari kuja kuanza ushirikiano kwa Gharama za GSM.

Lakini,kumekua na malalamiko mengi sana kutoka kwa baadhi ya viongozi kuwa GSM imekua na ikiingilia majukumu yao na wao ndiyo wenye mamlaka hayo waliyokabidhiwa na WANACHAMA. Kwa masikitiko makubwa kauli hizi pia zimekua zikitekelezwa kwa vitendo

Usimamizi wetu umekua tu kwa yale tunayogharamia na kamwe hatukuwahi kutaka kujua mapato wala matumizi ya chanzo chochote cha Yanga.

Ikumbukwe pia,GSM imejitolea kwa hali na mali katika kuleta YANGA yenye maendeleo yake binafsi kupitia wanachama na KAMWE GSM haina nia ya KUPOKA MADARAKA WALA TIMU kutoka kwa mtu yeyote. YANGA NI WANANCHI NA ITABAKI KUWA YA WANANCHI

Kwa barua hi I,GSM itabaki kuwa mdhamini wa Yanga kimkataba na kutekeleza yale TU yaliyo Kwenye mkataba na kuachana na yote yaliyo nje ya mkataba.

Aidha,kwa niaba ya GSM tunaomba radhi kwa yoyote aliyekwazika na ushirika wetu katika kuijenga Klabu yetu na tuliyafanya hayo kwa mapenzi mema tu.

Tunawatakia kila la heri katika mapambano na tutaendelea kuwa sehemu ya mabingwa wa kihistoria.

DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
FOR GSM GROUP OF COMPANIES
 
Back
Top Bottom