Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

"Kikubwa nnachoweza kusema nawaomba wana Yanga tuwe watulivu, klabu kupitia Msola tutatoa tamko rasmi. . uongozi kwa pamoja tutafuatilia na taarifa rasmi kama klabu tutatoa baadaye ila wana Yanga wawe na amani kila kitu kinaenda sawa. . Yanga tuna utaratibu wetu wa kutoa taarifa na tutatolea ufafanuzi wa sintofahamu zote ikiwemo swala la wachezaji ambao sauti zao zimevuja. . swala la mikataba ni too personal hatutoweza kuweka wazi ila tuna wachezaji ambao wamemaliza mkataba na majadiliano yanaendelea kumjadili mchezaji mmoja mmoja ni kama kumpa kiki, hatuwezi kujadili mchezaji mmoja mmoja tutakuja na taarifa ya wachezaji wote. . ni kawaida wachezaji kuibua sintofahamu kipindi cha usajili ili kuongeza thamani yao sisi hatutishwi na hilo" David Luhago ( Katibu Mkuu - Yanga SC)

Sidhani toka Yanga izaliwe kama imewahi kuwa nankatibu poyoyo na asiye na uwezo hata Wa kueleza mambo kama huyu. Yaani anaongea utadhani anasutana na mtu au watu. Kwa kifupi anavyoongea anaudhi badala ya kushawishi
Mkuu hizi timu mbili bado zinategemea donation, subscription, Loyality na ada za wanachama,,..

Huwa hazina profit kabisa,,

Sasa hao wadhamini mwanzo wanakuja na kauli tamu kuwa tunasaidia club ilihali kwa upande mwingine wa sarafu wako kimaslai zaidi,, baada ya ile mechi ya watani nadhani walichota mapesa,, sasa wanachama wanapohoji ndio kinakuja hicho sintofahamu,, lazima wahoji mapato na matumizi ili ktk vile vikao na wanachama wapate cha kusema.

Si Yanga wala sisiSimba[emoji23]

Itachukua mda mrefu kuja kuelewana 100% baina ya wadhamini na clab.

Bado tuko na matongotongo gharama za kuendesha clab ni kubwa mno kulinganisha na kinachoingia.

Azam nadhani wanaweza kufika mbali vile wakiacha Usimba+Uyanga,, walianza vizuri ila kuna dhambi kwanza inawatafuna[emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wameanza kuondoka mmoja mmoja....
[emoji468][emoji468][emoji468][emoji468][emoji468]

Mjumbe wa kamati ya utendaji Yanga SC Richard Shija amejiuzulu nafasi yake.

....
"Nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi zote za uongozi katika klabu yangu ya Yanga.

Yanga ni kubwa kuliko mimi na kuliko mtu yeyote. Yamezungumzwa mengi lakini mimi sitazungumza chochote. Wakati utaongea.

Ukweli hata usipousema, huwa una tabia ya kujitokeza wenyewe japo taratibu lakini huwa unadumu milele"

*YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO*

*Shija Richard Shija*View attachment 1401106
Shinikizo kutoka upande flani[emoji16]

Nugaz vepe? Mtoto wa kitanga yule anavojua kupangua maneno mdomoni,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hizi timu mbili bado zinategemea donation, subscription, Loyality na ada za wanachama,,..

Huwa hazina profit kabisa,,

Sasa hao wadhamini mwanzo wanakuja na kauli tamu kuwa tunasaidia club ilihali kwa upande mwingine wa sarafu wako kimaslai zaidi,, baada ya ile mechi ya watani nadhani walichota mapesa,, sasa wanachama wanapohoji ndio kinakuja hicho sintofahamu,, lazima wahoji mapato na matumizi ili ktk vile vikao na wanachama wapate cha kusema.

Si Yanga wala sisiSimba[emoji23]

Itachukua mda mrefu kuja kuelewana 100% baina ya wadhamini na clab.

Bado tuko na matongotongo gharama za kuendesha clab ni kubwa mno kulinganisha na kinachoingia.

Azam nadhani wanaweza kufika mbali vile wakiacha Usimba+Uyanga,, walianza vizuri ila kuna dhambi kwanza inawatafuna[emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
Sahihi asee, Azam wakiacha kufuata uswahili ni rahisi sana kwao kitoboa na kufika malengo kwa sababu wao inajulikana ni timu ya mtu binafsi. Hawa jamaa sijui wanakwamia wapi ila nadhani na shirikisho la soka kujaa viongozi Wa simba na yanga ni tatizo kubwa sana kwa maendeleo ya vilabu vingine na mpira wetu kwa ujumla. Sisi timu zetu hizi zinazoendeshwa kwa makomandoo na wazee Wa klabu si rahisi kusawazisha mambo. Mifumo ya uendeshaji klabu zetu kupitia wadhamini au muwekezaji bado ni tatizo kubwa sana! Muwekezaji anakuwa na asilimia zake tena nyingi na bado unakuta na wanachama wana asilimia nyingi zaidi ila klabu inaendeshwa kwa kumtegemea muwekezaji mwisho Wa siku ni kama hivi Sasa wakikohoa tu wote tunatetemeka. Kwa kifupi tunahitaji elimu kubwa na kiundani sana kuhusiana na uendeshaji hizi klabu kisasa kabla ya kuingia huko, mana naona tunaendesha hivi vilabu kupitia wadhamini tukiwa hatujui mambo kiundani kuhusiana na mfumo huu na tunaingia ktk mfumo Wa uwekezaji tukiwa hatuna elimu ya kutosha pia kuhusu mfumo huu.
 
HABARI mpya ni kwamba bado bilionea anayeipa kiburi Yanga, Ghalib Said Mohamed ameshikilia msimamo wake kutojihusisha na baadhi ya mambo ndani ya klabu hiyo huku akisisitiza kwamba amechoshwa na majungu.
Lakini ishu nzito zaidi ni kwamba kikao cha siku mbili cha Kamati ya Utendaji ya Yanga kilichokutana Masaki Jijini Dar es Salaam, kilikuwa na mzozo wa aina yake na baadhi ya wajumbe wametishia kujiuzulu ili kumrejesha GSM ndani ya Yanga baada ya kuonekana kwamba wao ni tatizo.
Ingawa viongozi wamekuwa wagumu kutoa tamko kwa yaliyojiri ndani, lakini Mwanaspoti limebaini kwamba kuna vigogo watatu ambao jana wajiweka pembeni kwani wamekuwa wakituhumiwa kwamba wao ndio walioibua ishu hiyo na kumtibua tajiri ambaye ameonekana kuleta furaha kwa mashabiki Jangwani.

MANNE YANAYOMNG’OA YANGA
Uchunguzi wa kina wa Mwanaspoti umebaini kwamba kuna mambo matano ambayo yamemkera GSM na kuamua kujiondoa Yanga.

KULIPA WACHEZAJI
Kitendo cha GSM kumtumia mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz kuwagawia wachezaji posho mbalimbali za hamasa na vifuta jasho inasemekana imewakera baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao walitaka ishu hiyo ikabidhiwe kwa viongozi wafanye utaratibu wenyewe. Lakini tajiri akasema ule mkwanja anatoa kwa mapenzi yake na wala haipo kwenye makubaliano ndio maana anamtumia mtu wake na utaratibu wake.

USAJILI
Kitendo cha GSM kumalizana na mastaa kwa kuwasajili juu kwa juu na yenyewe imeleta maneno.
Baadhi ya wajumbe wanataka apeleke fungu klabuni wao wamalizane na wachezaji hao ingawa tajiri huyo uchunguzi unaonyesha kwamba hupewa muongozo na viongozi wa juu na anachofanya ni kuwaita wachezaji kuelewana nao na kuwapa fungu lao.
Baadhi ya wachezaji aliowasajili kwenye dirisha dogo ni Morrison, Haruna Niyonzima, Adeyun Saleh na Ditram Nchimbi pamoja na makocha wote. Lakini vilevile hawafurahishi kuona wachezaji wapya wakitambulishiwa ofisini kwa mdhamini huyo badala ya klabuni. Lakini tajiri akajibu kwamba alikuwa anatoa fedha wakati fulani lakini mambo yakawa yanaenda tofauti na matarajio yake.

BIASHARA YA JEZI
Habari zinasema kwamba kuna baadhi ya wadau ambao ishu ya GSM kushinda tenda ya kuuza jezi za Yanga iligusa masilahi yao ya kiuchumi, hivyo hawakufurahishwa kwa vile walishatengeneza mzigo wao ndio maana wakaanza maneno ya chinichini lakini yakafika kwa tajiri.
KUINGILIWA MAJUKUMU
Hoja nyingine ya wanaompinga GSM ni kwamba ameonekana kuwa mbele zaidi kuliko viongozi wa wanachama na anaingilia majukumu mengi ambayo walipaswa kufanya wao kama kuandaa timu mpaka ishu za mechi huku wao wakiwa hawaonekani kabisa.

UONGOZI UNASEMAJE?
Mwenyekiti Dk. Mshindo Msolla alitangaza jana kwamba tayari uongozi wao umeijibu barua ya GSM ya Machi 24, hii ikiwa ni baada ya maamuzi ya pamoja ya kikao cha Kamati ya Utendaji, ambacho kiliwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya wajumbe wake.

Rudi Nyumbani Kumenoga.
 
Yataisha haya
 
Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kuwa timu hiyo itasajili nyota wanne wa kigeni yakiwa ni mapendekezo ya kocha Luck Eymaela.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbulia amesema Eymael amewasilisha ripoti ya maboresho ya kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.

Mwalimu ametuachia ripoti yake ya usajili ambayo tayari wadhamini wetu kampuni ya GSM wameanza kuifanyia kazi, amesema Bumbuli.

Mwalimu amehitaji wachezaji wanne wa kigeni ambao ni beki, kiungo, winga na mshambuliaji.

Pia amependekeza wachezaji ambao mikataba yao imemalizika lakini anahitaji kuwa nao msimu ujao".

Tunaendelea na mazungumzo na wachezaji nane ambao mikataba yao iko ukiongoni.
 
Hahahaha, naona hali imekua shwari sasa , mtulie ktk usajiri , isije ikawa km ya zahera , na mpunguze kusajiri kwa,mihemko
 
Imeshakuwa shwari kiasi Mtani.

Kabisa usemalo inabidi utulivu wa hali ya juu mana yale ya mwaka jana ni kichefu chefu kwani kuna siku niliona sehemu eti tulisajili wachezaji 22 nikabaki kuduwaa tu.
 
Hahahaha, si timu ya wananchi kila mwana kamati anasajiri
 
Mtoto yake peremende

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji2] [emoji2] mwanzo lilikuja vuvuvugu la kufurahia ujio wa tshishimbi huko mpaka ajibu na Manara kwenye page zao za akaunti walikuwa wanapost ishu za huyu mkongo kiasi Manara akasema yeye anatamani tshishimbi aje simba,je kwa nafasi anayocheza na umri wake ni kweli tshishimbi ni hitaji haswa la kikosi chenu?
 
Unajua mm siku hizi nimechoka na fununu,,

Hizi timu zetu mbili bado kuna shida kubwa tena sana tu.

Nliskia hizo mambo ila naangalia tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom