Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Labda kwa sababu Mo katengeneza Sanitizers na kuziuza ktk janga hili la Corona. Kwa maana nyingine kama Mo amechukulia Corona ni fursa basi hawezi omba ugonjwa huu uondoke mapema!
Kwani Moo yeye hataathirika na Covid 19? Mikia wao hawatakimbiwa na wachezaji? Bilioni 20 zenyewe za kununua mikia bado hajaitoa

Mnyero Fc watulie tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
YANGA YATAKIWA KUTUMIA MAWAKALA WAZOEFU KUFANYA USAJILI

Aliyewahi kuwa kocha wa Yanga Hans van Pluijm amesema utaratibu mbovu wa usajili ndio sababu inayopelekea mabingwa hao wa kihistoria wasajili wachezaji wenye viwango vya kawaida.

Pluijm ambaye aliisaidia Yanga kutwaa mataji mawili mfululizo ya ligi kuu misimu ya 2014-15 na 2015-16, amesema ili kupata wachezaji wazuri sokoni, Yanga inapaswa kurudi kwenye utaratibu wa kutumia Mawakala wazoefu.

Pluijm aliyewahi kupita vilabu vya Singida United na Azam Fc, amewataka mabosi wake hao wa zamani kuacha kusajili wachezaji kwa kutumia taarifa za mitandaoni kwani mara nyingi taarifa hizo hasa video zinazowekwa Youtube kuwahusu wachezaji hao ni zile ambazo wameonekana kufanya vizuri "Nimeifuatilia Yanga na nimegundua wanakosea kwenye usajili, kwani wanasajili wachezaji kutoka nje wa kiwango cha chini na kushindwa kuonesha ushindani, lakini hawajachelewa, kama wanahitaji wachezaji wazuri wanatakiwa kutumia mawakala wazoefu," amesema.

Pluijm alisema kama Yanga wanahitaji kuchukua ubingwa unaoshikiliwa na watani wao Simba, wanatakiwa kuacha kusajili wachezaji kimazoea kama miaka iliyopita, kwani mambo yamebadilika na ikiwa wanahitaji mchezaji mzuri lazima wakubali kupita njia sahihi kwa kutumia Mawakala "Unajua siku za hivi karibuni kumeibuka mazoea watu kusajili wachezaji kupitia mitandao, lakini wengi wao wamekuwa wakidanganya na mwisho unapata mchezaji anayekuja kukalia benchi badala ya kuwa msaada kwenye timu".

Pluijm ni mmoja wa makocha ambao wameacha historia nzuri kunako klabu ya Yanga katika muda ambao aliinoa timu hiyo.

@Yangafulldozz.
Ukweli mtupu. Naona hajaongelea suala la 10% nalo inabidi tuache, japo hili hata mikiani huwa wanafanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hapo kasahau tu kitu kingine kikubwa cha wale kamati ya usajili kupambania 10%. Ila tukitumia mawakala wazoefu kweli huko mbele hatutokuwa na kina Yirpe + Molinga
kidunula1 na Chikwuemeka naona kama Pluijm yuko sahihi.

Kwani na sisi tulizidi kusajili wachezaji ilimradi tu mwishowe wakawa watazamaji tu huku wanakula mshahara wetu pasi kuisaidia timu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wizara ya michezo imepanga kuanzia msimu ujao timu zote za ligi kuu Tz bara kuwa na wachezaji Wa kigeni wasiozidi watano tu. Ikiwa hivyo mi naona tutapaswa kuwatema Molinga, Eric Kabamba, Sibomana na Yirpe fasta. Kasheshe itabaki hapa sasa; Shikalo,Lamine,Haruna, Tshishimbi, Morrison. Nani achomolewe ili aletwe Mshambuliaji matata ili timu iwe na idadi ya wachezaji watano Wa kigeni!? Mana piga ua garagaza ni lazima atafutwe mshambuliaji Wa kati japo na winga matata namba 7 nae anahitajika sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hapo kasahau tu kitu kingine kikubwa cha wale kamati ya usajili kupambania 10%. Ila tukitumia mawakala wazoefu kweli huko mbele hatutokuwa na kina Yirpe + Molinga

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ilishakuwa jipu. Japo nadhani tuwe na subira tu mabadiliko yakishaingia Yanga basi hapo ndio itakuwa mwisho wa hii kitu.
 
Wizara ya michezo imepanga kuanzia msimu ujao timu zote za ligi kuu Tz bara kuwa na wachezaji Wa kigeni wasiozidi watano tu. Ikiwa hivyo mi naona tutapaswa kuwatema Molinga, Eric Kabamba, Sibomana na Yirpe fasta. Kasheshe itabaki hapa sasa; Shikalo,Lamine,Haruna, Tshishimbi, Morrison. Nani achomolewe ili aletwe Mshambuliaji matata ili timu iwe na idadi ya wachezaji watano Wa kigeni!? Mana piga ua garagaza ni lazima atafutwe mshambuliaji Wa kati japo na winga matata namba 7 nae anahitajika sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwiii!! Hapo itakuwa changamoto aisee.

Wameshapitisha tayari au ni wazo wameliwasilisha?
 
Screenshot_20200430-150849.png

Kuna APP yetu jamani tuidownload ipo play store,Ina mengi ya Yanga na hutojuta kuwa nayo.

Daima mbele
 
Back
Top Bottom