Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Screenshot_20200430-151421.png
 
Mkuu kwani Wabrazil walikuwa wangapi, si 3

Mbona unamtaja huyo Fraga peke yake ambaye naye kwenye mechi tulivyocheza na nyie alitepeta

Wale Wabrazil wa India wote ni mzigo, hivi wako wapi? Ukiacha huyo Faranga

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona wapo ila namba ngumu..ila tuongee ukweli mara ngapi Tairone da Silva anaanza kwenye defence ana anafanya vizuri!??
Hvi Yikpe kuna siku amewahi kucheza vizuri licha ya kumpa namba mara kwa mara!+?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muheshimiwa raisi kasema wanaangalia uwezekano wa kuruhusu ligi iendelee. Najiuliza kwa hali ilivyo kiuchumi,mikia fc watapata wapi hela za kununua mechi?
Usishangae na ubingwa wenyewe waukose

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NILETEENI KIUNGO WA KUNITINGISHA "TSHISHIMBI

KIUNGO wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kama kuna kitu anatamani basi ni timu yake kusajili kiungo mpya wa kushindana naye, mwenye ubora hata wa kumzidi.

Yanga katika hesabu zao za usajili wanajipanga kusajili kiungo wa kati mkabaji na kufikia sasa hesabu zinamtaja Mnyarwanda Ally Niyonzima kuwa chaguo la kocha Luc Eymael.

Akizungumza na Mwanaspoti, Tshishimbi amesema endapo Yanga itasajili kiungo mkabaji basi itakuwa akili nzuri itakayoboresha timu yao.

Amesema ana kiu kubwa ya kupambana kwa kushindana kwa ubora na kiungo mwenzake aliye na ubora mkubwa ndani ya kikosi hicho. “Mi napenda sana ushindani, nashangaa watu wanaogopa, mimi niko tofauti sana, napenda ushindani hii ndio njia sahihi ya mafanikio,” alisema Tshishimbi. “Kukiwa na ushindani mkubwa kwenye timu hapo ndipo ubora wa kikosi unakuja. Yanga wakileta kiungo mkabaji hiyo ndio safi mimi nataka sana tena aje haraka tuwanie nafasi kikosini.”
 
Back
Top Bottom