Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

HATUNA JINA LA MCHEZAJI YEYOTE WA SIMBA AMBAE TUTAMUHITAJI KWENYE USAJILI WA MSIMU UJAO "HERSI SAID"

BOSI mzito wa GSM anayeratibu usajili wa Yanga amesikia jina la Said Ndemla akihusishwa na mziki wake mpya akacheka sana huku akitikisa kichwa.

Ndemla amekuwa akihusishwa na Yanga kila inapofika wakati wa usajili, ingawa Mwanaspoti linaweza kuthibitisha kwamba Simba wameshampa mkataba mpya wiki mbili zilizopita na bado anausoma tu bado hajasaini.

Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM ambao wamepania kufanya makubwa ndani ya klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said amesisitiza kwamba wala hatasaini staa yoyote aliyeko ndani ya kikosi cha wekundu hao kwasasa.

Amesema wanaheshimu ubora wa wachezaji wa Simba pamoja na Ndemla lakini katika orodha wanayoifanyia kazi hawana jina lolote kutoka Simba kwani wanataka kusuka kikosi cha aina yake na chenye ladha ya kipekee zaidi ya klabu zote nchini. “Ndemla? Aje wapi Yanga? Hapana huo uvumi tu mdogo wangu, yule namuheshimu sana lakini mpaka sasa hatuna jina lolote kutoka Simba,” alisema Said ambaye moja ya usajili wake mkubwa ulioleta raha ni kumshusha Bernard Morrison aliyewatungua Simba bao moja lililowapa Yanga kiburi kwenye mechi iliyopita ya watani.
“Sina jina la Ndemla, niseme ukweli na sioni kama tutamchukua mtu yoyote kutoka kule kwao. Yanga tuna hesabu tofauti za usajili. Tunataka vitu vikubwa safari hii,” aliongeza na kusisitiza kwamba usajili wao wanafanya kwa kushirikiana na wataalam wakubwa wa ndani na nje ya nchi.

Akifafanua hesabu zao Hersi alisema staa yeyote mpya watakayemleta sio mtu wa kuja kusubiri benchi wala huko anakotoka hasotei nafasi kivile ya kikosi cha kwanza.
“Huku tutaleta watu wa kweli wanaokuja kuanza kikosi cha kwanza kwa sababu huko wanakotoka tumeridhika na ubora wao, hatuleti watu wa kujaribu, huo ndio mpango wetu kwa sasa. “Tunachotaka kufanya kuna watu ambao tutaachana nao hasa wale ambao wamekuwa wakikosa nafasi sana ili wale ambao watakuwa wanatoka kikosi chetu cha kwanza wajiulize.

“Hawa wapya ambao wanakuja imani yetu ni kwamba wataingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza kwahiyo kama unakosa nafasi katika timu yako huko uliko Yanga isahau kabisa, tunapotaka kujenga timu bora.
Tunashukuru kwa taarifa!!

The only thing to fear is fear itself
 
Nadhani wanaona na kuyasikia haya mapungufu na hawana budi kuyatafutia ufumbuzi mana kama App yangu tangia jana inaanza fresh tu kwamba karibu kwenye App Rasmi ya Yanga kisha naishia kuambiwa lipia hapa halafu inabaki tu kuload.
Duuu IT Technicians wetu watakuwa wana shida mahali Fulani ila naamini wanahangaika kuliweka sawa hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila GSM hata hiyo App msingeipata ........Nakukumbuka tu ligi itarejea muda sio mrefu hahahahahahahahah kila mtu atavuna alichopanda.
Haijalishi Mtani Potelea pweteee wacha GSM atuue. 😂😂😂😂

Kama mimi aisee. Huwa nawakumbuka sana tambo zenu. Lol. Ligi ianze hebu.

Natamani watupange na nyie Quarter final kwenye Kombe la FA tupate kuwanyoosha tena. 😂😂😂
 
Back
Top Bottom