Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Wamepita Makocha weengi hapo Chura FC tena wengine kwa mbwembwe nyiiingi lakini mwisho wake mnawafungashia virago waondoke zao. Mwambieni aje taratibu, aje kwa heshima na adabu zote akijua kabisa kuna Mzee wa Pori, Lunyasi ambae hakawii kukitia mchanga kitumbua chake cha ajira hapo Bonde la kulimia mpunga
Mikia fc.
 
Cc Shadeeya @Kidunula ,watani naona Head Coach kawasili
IMG_20201016_071932_599.jpg
 
KOCHA WA YANGA ASIPIMWE KWA PIRA BIRIANI, AACHWE AFANYE KAZI

Anaandika @exaud_msaka_habari

Cedric Kaze amesaini mkataba wa miaka Miwili yani atakuwa jangwani mpaka 2022. Ni mkataba mzuri utakaompa nafasi ya Kuijenga timu ya Ushindani.

Katika Mahojiano yake leo amesema amekuja kuifanya Yanga irudi kwenye hadhi yake, amekuja kurudisha Heshima ya Yanga nadhani hii ndio kiu ya Kila mwanajangwani kwa sasa.

Ila sasa Kazi ya kuifanya Yanga Irejee kwenye heshima yake sio nyepesi kama tunavyodhani na kocha anajua na Viongozi wa Yanga wanajua ndio maana wamempa mkataba Wa miaka Miwili.

Kama Yanga wanaitaka Yanga bora basi wavumilie Wapande milima na kushuka wampe Muda kocha afanye kazi yake kikamilifu.

Yanga waache haraka waliyonayo kichwani kwamba Watalala leo waamke kesho wakute timu yao imekuwa hatari sana, inahitaji Muda inahitaji Mipango na inahitaji Uvumilivu.

Waachane na kulifikiria Pira biriani wanalotamba nalo majirani zao, waache kuwaza mambo makubwa kwa kipindi kifupi, wakianza kumharakisha kocha awafikishe wanakotaka watamfukuza Soon. Wamuache afanyie kazi mipango yake.

Malengo ya Yanga ni Ubingwa msimu huu ila wapo ligi Moja na Simba na Azam wasije wakakosa Ubingwa wakamtimua Kocha, watakuwa wanamuonea Bure, waheshimu Muda utatoa majibu.

ALL IN ALL KUMBE TUNISIA WANAVAA JEZI NYEKUNDU SASA ITAKUAJE
 
Back
Top Bottom