USAJILI YANGA CEDRIC KAZE AFUNGUKA
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze tayari amewasilisha mapendekezo yake ya usajili kipindi hiki cha dirisha dogo akihitaji wachezaji watatu
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema wanafanyia kazi mapendekezo hayo na watahakikisha wanawapata wachezaji waliopendekezwa na kocha huyo raia wa Burundi
Akiwa tayari amemsajili Saido Ntibazonkiza, Kaze amedokeza pia kuhitaji kiungo mshambuliaji na mlinzi
Hata hivyo amesisitiza usajili huo utafanyika kwa kuangalia mahitaji ya timu na sio kwa kufuata presha ya mashabiki kwani wakifanya hivyo wanaweza kuathiri kile ambacho kimeanza kujengeka katika kikosi chao sasa
"Hutakiwi kusajili kutokana na presha za mashabiki au viongozi, tunahitaji wachezaji ambao watasaidia timu kufikia malengo yetu, kama nilivyoeleza awali kwamba tunahitaji kupata watu ambao watakuwa msaada kwetu," alisema Kaze