Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20210104_174344.jpg
 
Leo nimeshangaa sana Kaseke na mwenzake kwenda goli la mpinzani kuanza kutikisa nyavu kama wanatafuta kitu hivi kwa chini,baadaye wakaenda hadi kwenye taulo la golikipa na kulikung'uta!Nilipigwa na butwaa kuona hivyo!Wakati huo Matokeo yakiwa Prison 1-0 Yanga na Yanga walikuwa wakishambulia sana!

Hii tabia si nzuri hasa kwa timu inayoshiriki ligi kuu na Club kubwa kama Yanga!Mnatia aibu kwakweli na hii sio mara ya kwanza ninyi kufanya hivyo!

Prison mnalingana nguvu maana kwenye mechi ya kwanza mlitoka sare tena kwenu!Sasa mnachoshangaa ni nini wao kuongoza kwa goli moja na ninyi mkiwa mnakosakosa?

Aibu kwenye michezo,mechi zinaonekana mpaka nje ya nchi halafu mnafanya ujinga!Shwain kabisa!



Siku nyingine mkagoma kuingilia lango la kuingia uwanjani,ninyi watu gani?Mbona mnaupa sana promo ushirikina?



Nawatakia kheri ya mwaka mpya!
Wewe umejuaje Mambo ya ushirikina? Bilashaka wewe ndiyo mchawi
 
Tusifadhaike,hii sare ya Leo imeonyesha ni namna gani Yanga hii iko imara. Timu imeimarika sanaaa!! Ina ari ya juu sanaaaa. Simba bila kubebwa kama walivyosaidiwa dhidi ya KMC hata sasa wasingekuwa na uwezo Wa kufunua midomo yao.

Naamini kwa ubora Wa hii timu tunakwenda kutwaa ubingwa msimu huu!
Kwa asilimia mia
 
Kwani yanga dhidi ya kmc haikubebwa? Penati fake mlipewa. Dhidi ya gwambina mlipigwa goli halali likakataliwa, dhidi ya simba faulo nje 18 mkapewa penati. Ni kujidanganya kuwa mechi zote yanga imeshinda au kudraw kwa haki.

Ubingwa labda muibe kombe.
Msimu huu Yanga hapotezi mechi hata moja,kwa raundi ya pili Simba lazima apigike.Stay tuned Ubingwa unakwenda jangwani msimu huu
 
Back
Top Bottom