Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Screenshot_20220616-131512.jpg
 
Huyu GSM anafaa kushtakiwa.!

Yaani kamchukua pep guardiola halafu kamvalisha kofia eti ndio NABI..yaani anatuonaje huyu?

Hilo kama halitoshi kubwa zaidi katuletea kdb halafu eti kamvalisha mask ndio aitwe sure boy..! Mjue ana ujanja wa kishamba sana huyu..

Kikubwa zadiz na kilicholeta maumivu nchini ni kumleta huyu benzema ambaye sote tunajua hana mzaha na goli, mtu katoka kuchukua uefa juzi tu leo tena unamleta huku yanga..hivi hajui sisi simba tunavyopata tabu, presha, kisonono,kaswende?

Guardiola vua hiyo mask hatutaki ujanja ujanja tunataka fair play wewe sio NABI..

KDB sisi tutakushtaki kwa mabosi zako unachezea team mbili wewe sio sure boy vua hiyo mask tafadhali..

Na wewe benzema hivi hata kama sisi mbumbumbu ndo unadhani hatukujui wewe hata kama umevaa mask ya mayele? Vua tafadhali matatizo uliyotusababishia yanatosha,

Umefanya tajiri yetu ashushe matofali pale bunju..

Inatosha
Yaaaniiiiiiiii.......
 
Niko poa kabisa mtani.

Unaona raha tuliyoipata ndani ya miaka 4 mfululizo. Nakutakie furaha njema ila tukutane CCL kuanzia mwezi wa nane.
Hahahaaa! Hata na sie tuliwahi pia ujue.

Haya Mtani tukutane mwezi wa nane. Tupo. 🙏
 
Back
Top Bottom