Yoweri Museveni Rais wa Uganda amepiga marufuku Mitumba. Amesema ni Nguo zilizoachwa na Wafu wa Ulaya

Yoweri Museveni Rais wa Uganda amepiga marufuku Mitumba. Amesema ni Nguo zilizoachwa na Wafu wa Ulaya

Nawaza ajira za wangapi zinaenda kufa sababu ya kiburi cha mtu mmoja

Piga mahesabu ukitoa tamko kama hili vijana wangapi pale ilala,m/mmoja kkoo pekee wataathjrika
Sasa jymlisha ncgi nzima

Wakati ukitoa matamko huku umeshiba mkumbuke mwenye nhaa.

Tz haiwezi kupiga marufuku patachimbika[emoji38][emoji38][emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app

watauza zilizozalishwa nchini
 
Ingeweza kukuza soko la ndani (viwanda vya ndani kama vingekuwepo na quality ingekuwa nzuri) Unless otherwise ni shortcut ya kuvaa midabwada....

Au sababu ya supply ndogo kuliko demand bei kuwa juu zaidi..., ukizingatia watu hawana disposable income ya hata zile basic need kubwa nyingine mbili (chakula na malazi) basi watakuwa hawana budi kutembea peku au viungo vingine vikichungulia...

By the way mitumba yote sio kwamba imetumika mingine ni ex-catalogue au rejects....; kitu ambacho hata samaki zile top quality huwa zinakwenda nje na nyingine grade B zinabaki soko la ndani....

Watunga sera wasipende shortcut..., tungeni sera za watu kupata disposable income..., vitu vya ndani viwe top quality basi watu wala hawatahitaji kuambiwa pa kununua....
We mtetezi tutavaa mitumba mpaja lini ?
Mbona Africa magharibi wanavaa mavazi yao ya kipekee na wamezoea.
Hata vazi la masai likiboreshwa ni zuri sana kama kichwani tutaondoa ukoloni.
Hizo nguo za wazungu sio midabwada?
Tuliweza kwenye rambo tukaja vufingashio.
Unakumbuka watu walivyobeza upigaji marufuku wa mifuko ya rambo .
Je leo mwaka wa ngapi tunaishi bila rambo?
Tukipiga marufuku mitumba kisha sekta ya nguo inajiinua yenyewe.
Utaona uwekezaji mkubwa wa wazawa na wageni.
Kutakuwa ba ubunifu mkubwa sana wa bidhaa za nguo.
Kwa ujumla tutakuwa tumepiga hatua mbele na si kurudi nyuma
Kuanza ni bora kuliko kutoanza kabisa.
Pamba yote tunayolima tunaishia kuvaa mitumba kweli ?
Unadhani ni sawa?
 
Ila mitumba inavalisha watu wengi xnaa na pia kutoa ajira kwa vijana wengi mno.sidhani kama ni busara kuifungia
Imagine wewe , ndo umepata uongozi sasa, bila shaka utatuludisha nyuma kwa hatua za mlevi.
 
We mtetezi tutavaa mitumba mpaja lini ?
Mbona Africa magharibi wanavaa mavazi yao ya kipekee na wamezoea.
Hata vazi la masai likiboreshwa ni zuri sana kama kichwani tutaondoa ukoloni.
Hizo nguo za wazungu sio midabwada?
Tuliweza kwenye rambo tukaja vufingashio.
Unakumbuka watu walivyobeza upigaji marufuku wa mifuko ya rambo .
Je leo mwaka wa ngapi tunaishi bila rambo?
Tukipiga marufuku mitumba kisha sekta ya nguo inajiinua yenyewe.
Utaona uwekezaji mkubwa wa wazawa na wageni.
Kutakuwa ba ubunifu mkubwa sana wa bidhaa za nguo.
Kwa ujumla tutakuwa tumepiga hatua mbele na si kurudi nyuma
Kuanza ni bora kuliko kutoanza kabisa.
Pamba yote tunayolima tunaishia kuvaa mitumba kweli ?
Unadhani ni sawa?
Hao Africa Magharibi hayo mavazi wanavaa kwe occasions tu.Ila Mitumba kule ipo.
 
Hata huko majuu mitumba ipo.Si wote wanavaa Brand new.
mchina kaleta vitu vipya kwa bei yako hata hizo tumeshindwa? yote kwa yote tunalima pamba na viwana tulikuwa navyo[kwa sasa vichache] kwanini tusiwekeze kwetu tuzalishe kwaajili yetu ziada tuuze.
 
Anataka cheap popularity.....Waganda wanahitaji vingi vya muhimu kuliko kupiga marufuku mitumba. Museveni ni jinamizi ambalo Waganda wanahangaika nalo.
 
Kwa utafiti wangu mdogo tu, Watanzania wanapenda mitumba sana. Sasa hiyo kuipiga marufuku ni kuwatesa wananchi tu.
Sasa na sisi tupo kwenye kundi la watu wenye akili duniani ?
Kama tunazo je unaweza onesha jambo moja linalodhihirisha uwepo wa akili kama mataifa mengine ?
Unslima pamba hslafu unavaa mitumba?
China kuna kila aina ya mashine za bei rahisi za kuanzia kuchambua pamba. Kutengeneza, nyuzi, vitambaa mpaka nguo.
Hivi uundaji nguo nao ni mgumu kama teknolojia za kuunda injini au kompyuta.
Hivi ktk karne ya 21 kama huwezi kutengeneza hata nguo,utaweza nini?
 
Siku nyingi nchi za Afrika ya Mashariki zilikubaliana kupiga Marufuku mavazi ya mitumba lakini zikatishwa na vikwazo vya Marekani. Lakini mpaka sasa Rwanda na hivi karibuni Uganda zimejipiga kifua na kupiga marufuku mavazi ya mitumba. Njia pekee kwa nchi kukuza viwanda vyake na kutengeneza ajira ni kuzuia cheap imports kama mitumba. Hivyo ndivyo nchi zote duniani zilivyoendelea. Suala hili tumelipigia sana kelele humu.

Ni lini na sisi tutapiga marufuku mavazi ya mitumba?
 
Tutavaa nini? Hivyo viwanda vya kukuzwa viko wapi?

Si mliua Urafiki, Kilitex, Mwatex n.k mkawaachia Wahindi waje na Sunflag na A-Z na watumwa huko viwandani wa kuchanganya rangi na kuchochea moto ni watoto wenu walipwe elfu 60 kwa mwezi

Watu weusi wana Upumbavu sana
 
Kwani sisi tuna ubia na uganda?
 
Wakati kiwanda cha urafiki kilipouzwa ulikuwa wapi?

Mitumba haiwezi kupigwa marufuku ndugu, unataka watz wanyonge watembee uchi?
 
We mtetezi tutavaa mitumba mpaja lini ?
Kama kawaida yetu tunaongelea vitu kwa upeo mfupi umeona nilochosema..., Unless Otherwise Viwanda vya ndani ambavyo havipo na quality yake leaves a lot to be desired itapelekea watu kuvaa midabwada (hii sio theory tu it happened hapo nyuma) kwahio sitetei mitumba ila mimi ni muumini wa bottom up approach anza kwanza vutia watu vitu vyako; quality na taste (kuna kipindi watu walipenda kuvaa mavitenge (though they were not cheap) watu wanavaa mitumba sio sababu tu imetoka nje bali quality na uniqueness..., Leo hii dada anauza nyanya kipato chake cha kuunga unga ila akienda mnadani anatoka na kupendeza hata Beyonce haoni ndani..., Kutokana na Economy of Scale ni ngumu kwa nguo ya ndani kushindana na price ya hio mitumba....(we are not there yet) Unaweza ukasema kwanini wanunue cheap na wasinunue za gharama (swali linakuja watu wako wana- sufficient income) ?
Mbona Africa magharibi wanavaa mavazi yao ya kipekee na wamezoea.
Issue sio kuzoea tu issue / fashion ni taste na uniqueness hata huku kuna kipindi watu walikuwa wanavaa nguo saresare; au kule China kuna kipindi cha kufunga mikanda walikuwa wanavaa manguo yao fulani ya kufanana na viatu vya kamba za katani - lakini leo giving them a choice kila mtu anafanya anachofanya (To each their own)
Hata vazi la masai likiboreshwa ni zuri sana kama kichwani tutaondoa ukoloni.
Kwani hata bila kuboreshwa ni baya na unaongelea vazi material au kufunga lubega (hio sio mmasai tu ni kabila nyingi tu) ila nakuuliza hilo vazi la mmasai wakiboresha unadhani litacost kiasi gani kwenye market value kwa viwanda vyetu hivi vinavyotegemea umeme wa Makamba ?
Hizo nguo za wazungu sio midabwada?
Kumbe hujui midabwada ni nini midabwada ni viraka watu wanakosa pesa za kununua nguo hence wanashona na kuweka viraka..., mafundi viatu watarudi kushona viatu sababu ukinunua kimoja unakibembeleza kisiishe au wote kuvaa Bata na Bora / Sare Sare usiongelee Nike na Adidas au Puma hao wakija huku hakuna pesa (pesa zako za madafu kwao ni hasara)
Tuliweza kwenye rambo tukaja vufingashio.
Unajua hata kabla ya Rambo na vifugashio tulikuwa tunaishi na mifuko ya karatasi (ila ukweli ndio huo hizo plastics ni cheaper) kwahio wakiacha rambo sio kwamba watu wanatumia mifuko mingine ambayo ni expensive ila inawafundisha Reuse (katika ile 3Rs)
Unakumbuka watu walivyobeza upigaji marufuku wa mifuko ya rambo .
Je leo mwaka wa ngapi tunaishi bila rambo?
Nimekujibu hapo juu mifuko / plastics ni cheaper ndio maana imesambaa sana ila inaharibu mazingira balaa...., ndio maana hata ulaya wanataka kufanya hivyo Ni manufaa kwa mazingira ila ni kipigo kwa mifuko ya watu / Pesa
Tukipiga marufuku mitumba kisha sekta ya nguo inajiinua yenyewe.
Usingoje mitumba ipigwe marufuku kuza sekta ya nguo za ndani zikiwa nzuri watu watanunua ni utamaduni..., Uganda watu wanapenda kuvaa nguo za kushona huku nguo za kushona sio kivile (pia quality ni mbovu unavaa nguo mara moja inapauka ikipigwa upepo) hio sio huku tu hata original za China unadhani kwanini kuna watu wanachukua kiatu dukani wanasugua soli chini ionekane ni mtumba, ili wakuuzie kama mtumba ?
Utaona uwekezaji mkubwa wa wazawa na wageni.
Mgeni aje awekeze ili alipwe nini wakati watu wamepigika ? Hivi ushajiuliza kwanini wawekezaji wengi wa vitu ambavyo ni fashion hawaji kuwekeza huku ? Jibu watu hawana buying power.....
Kutakuwa ba ubunifu mkubwa sana wa bidhaa za nguo.
Huo ubunifu unasubiri nini . Si wabuni waende kuwauzia diaspora waliopo ulaya ?
Kwa ujumla tutakuwa tumepiga hatua mbele na si kurudi nyuma
Kuanza ni bora kuliko kutoanza kabisa.
Anza ila kuanza sio kwa kupiga siasa anza kwa kuzalisha quality kutoka viwanda vya ndani promote nguo zako ili kina mama Aisha na Mwajuma na Neema wapende kuvaa kitu kutoka Mwatex na sio Mombasa hio ndio njia sahihi sio kulazimisha watu
Pamba yote tunayolima tunaishia kuvaa mitumba kweli ?
Unadhani ni sawa?
Unadhani hio pamba yako ukishamaliza kuitengeneza na kuwa-refined kwa umeme huu wa Makamba na ukatoa nguo itakuwa bei gani ? Ushajiuliza kwanini kuna vitu vinatoka ulaya vinakuwa na bei ndogo kuliko vitu vya ndani ? Jibu ni Economy of Scale - Pile it High.., Sell it Cheap.......; Na kama soko lako ni la kuokoteleza volume unazotoa hazitafanya bei iwe chini - Anza kidogo waambie watoto wa shule, wanajeshi n.k. wavae nguo made in Tanzania (ila utashangaa mzazi itabidi atoe mara tatu ya bei aliyokuwa anatoa jana)
 
Tutavaa nini? Hivyo viwanda vya kukuzwa viko wapi?

Si mliua Urafiki, Kilitex, Mwatex n.k mkawaachia Wahindi waje na Sunflag na A-Z na watumwa huko viwandani wa kuchanganya rangi na kuchochea moto ni watoto wenu walipwe elfu 60 kwa mwezi

Watu weusi wana Upumbavu sana
Kuvaa nguo za wafu zinazoweza kuwa na magonjwa siyo upumbavu, ila kiwanda imaginary cha wachochea kuni wanaolipwa 60K!!!!? Watu wako nchi hii!!?
 
Back
Top Bottom