Huyu hapa kwetu ni Kiongozi, lakini amapotea zaidi ya wiki nne na jibu jepesi ni kuwa yuko Likizo.
Wapi na kwa kanuni gani maana kaajiriwa juzi tuu nafasi hiyo.
Jee yanataka kuwa kama yale ya kijana Ben Saanane aliyepotea (potezwa kiutani utani) zaidi ya miaka saba iliyopita na wazazi na ndugu wanashindwa kufanya matanga maana hawajui kafa au yuko hai?
Sasa kama inafika mahali hata kiongozi hajulikani alipo na hakuna taarifa rasmi?
Hata kama ni ugonjwa, nini kinashindikana kututaarifu?
Mbona serikali hii inapenda kulea majungu?
Mtuambie tuu hata kama zile dua za wazee wa Kinyaturu kule Ikungi zinafanya kazi! Twaweza kumuombea msamaha au kumshawishi aombe mwenyewe!
Kuweni wazi KONDAKTA yuko wapi?