Ukiona mwafrika yoyote hasa mtanzania anamsifia Mandela basi huyo hajui lolote kuhusu historia ya kweli kuhusu shujaa na jasiri aliye shiriki kuwakomboa mataifa mengi ya Kiafrika dhidi ya wakoloni, wanajeshi wa Tanzania wakapigana na kumwaga damu wakati wa harakati za kuwakomboa Waafrika wenzao, Nyerere (RIP) aliwapatia fedha chungu nzima,silaha,mafunzo ya kijeshi wapigania uhuru, kaanzisha vyuo vya kuwafundisha vijana kutoka kwenye mataifa yaliyo kuwa chini ya wakoloni wa magharibi - nani kama Mwalimu Nyerere Duniani kote? hakuna kabisa.
Mandela anakuzwa tu na vyombo ya habari vya magharibi lakini ukweli wa mambo Mandela hawezi kuvaa viatu vya Kambarage hata siku moja ie Mandela hamwingii kwa lolote lile Nyerere zaidi ya kukaa gerezani zaidi ya miaka ishirini - ni hilo tu,personally umuchukulia Mandela kama binadamu aliye waangusha/wasariti Waafrika wenzake Afrika kusini, hakuna kitu chochote cha maana alicho wasaidia Waafrika wenzake Afrika kusini zaidi ya kuendelea kushirikiana/kumbatia makaburu na rangi nyeupe wengine - I am sorry kusema Mandela hakuwa riziki kwa waafrika wa Afrika kusini na Dunia, kusema kweli mkewe Winnie Mandela ndiye alikuwa mwanamke jasiri na mwenye msimamo thabiti - ndio maana alikuwa anagombana na mumewe mara kwa mara kwamba anawa aibisha Waafrika wenzake kwa kushindwa kuwaondoa kwenye lindi la umaskini,bado wanendelea kulala kwenye shanks,hawana maji wala umeme, arable land yote Afrika kusini bado inaendelea kushikiliwa na Makaburu na watu weupe, wafrika wanakuwa mashamba boy tu as if walipata uhuru wa bendera tu!! Halafu watu wanakuja hapa na kusema eti Mandela ni HERO, hii wapi na wapi??