Yuko wapi Vengu-mchekeshaji wa comedy

Yuko wapi Vengu-mchekeshaji wa comedy

Mnisamehe tu sio wote tunaweza kuwasilisha mawazo yetu kwa kuandika
wasalaam
 
Mwaka 2013 nilikuwa taasisi fulani ya utafiti na tulikuwa na kaka yake ambaye alikuwa dereva wetu pale, ndiye aliyekuwa akiishi na Joseph Kigamboni na ndiye alikuwa akipambana na matibabu yake........kwa maelezo yake kwenye kundi lao la ze comedy ni Joti na Masanja pekee ndiyo waliokuwa wakienda kumuona.......na kipindi kile Mizengo Pinda ndiye alikuwa msaada mkubwa sana wakati ni PM,maana chakula alichokuwa anakula kwa siku ilikuwa kama elf 30 (special meal).

Ila jambo kubwa lililokuwa linaelezwa nikwamba ni issue ya ushirikina ndani ya kundi lao.........

Duu wamempiga kipapai mwenzao halafu wakaokoka!
 
Jamaa alikuwa class mate wangu huko mbozi mission kabla ajaanza kuugua nakumbuka nikitoka church maeneo ya mabibo aliinita akataka kuninulia hadi kilaji nilikuwa mda huo situmii hiyo kitu nilimshukuru tukaagana tukipeana ahadi ya kuonana tena, Mara siku si nyingi nikasikia taarifa zake za kuumwa nilijaribu kuwacheki hao wasanii wenzie kwenye mitandao yao ya kijamii nipate kujua yuko wapi nikamjulie Hali lakini sijawahi pata ushirikiano. Naimani uko aliko anaendelea vizuri namuombea kwa Mungu awe mzima kama zamani aje kuendeleza harakati zake alikuwa anafit Sana kumuigiza Mueshimiwa Mrema
 
Hivi kwanini hawasemi mahali aliko wala afya yake?
 
Salaam sana wanajamvi,

Nimeona taarifa kupitia TvE Tanzania leo asubui alikua anahojiwa mshiriki mwenza katika kipindi cha ucheshi kilichobamba kitambo kidogo ze comedy mpaka orijino komedi Mpoki akisema kwamba Bw. Joseph shamba maarufu kama Vengu ambaye tuliaminishwa amepoteza maisha kwa maradhi yalokua yakimsumbua

Je, Vengu anaishi kweli na kipi kinasababisha aishi maisha ya kivuli au kuna nafasi nyeti anaitumikia kwa sasa?

Karibuni wenye taarifa zaidi

Ana tatizo la kwenye ubongo ambalo hawezi kurudi Katika hali ya kawaida tena Katika maisha yake. Ila ni mambo ya kifamilia hayo.Hata Muhimbili waliligundua hilo na hata kwenda India ilikuwa haina maana kwasababu ni tatizo ambalo ukipata halina tiba zaidi ya palliative care tu.

Alipelekwa tu India na Serikali kwasababu wakati ule kundi lilikuwa maarufu na ilionekana kama viongozi wanapelekwa India why not Wasanii lakini kitaalam walikuwa wanaojua nothing new will be detected or diagnosed.

Yuko Kigamboni kwa Babu na baadhi ya ndugu zake wakimpa msaada pamoja kundi lao la OK likiongozwa na Masanja Mkandamizaji.

Ila inasikitisha sana.
 
Hili swali hata mimi linanipa wakati mgumu Sana sema kina salama jabir na wengine wanaondesha vipindi vya kuhoji Hawa wasanii siku wakimuhoji mmoja wa Hawa original comedy watusaidie kuuliza hili
Tafuta mahojiano ya salama jabiri na joti yapo mtandaoni na ni ya mwaka huu huu tu
 
VENGU WA ZEKOMEDI DUNIANI AU AKHERA?

Amefariki au yungali hai? na kama yu ngali hai yupo wapi na anajihusisha na nini kwa sasa?

ni maswali yalio katika vichwa vya watu wengi sana haswa mashabiki zake,
Asilimia 99 ya wapenzi wa sanaa ya maigizo Yale ya kuchekesha haswa mashabiki wa msanii vengu hawajui ni wapi alipo na wanatamani hata wangejua ni kitu gani kimejificha kwenye story ya maisha yake,
Ukweli ni kwamba Joseph Shamba ama Vengu kama wengi tumjuavyo tulianza mfahamu baada ya kujiunga na kundi la maigizo la zekomedi
Vengu alijitengenezea wigo mkubwa wa mashabiki waliokuwa wanapenda kuona jinsi alivyokuwa akimwigiza Mh.Mrema huku akibeba uhalisia wake,
Vengu alianza kuugua kidogokidogo mwaka 2009, lakini Agosti, 2011 hali yake ilikuwa mbaya, akalazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar. Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ aliwahi kwenda kumjulia hali.

Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, alipelekwa kwenye Hospitali ya Apollo nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejeshwa nchini akiaendelea kuuguzwa na familia yake huku taarifa zake zikiwa ngumu kupatikana
lakini cha kushangaza zilianza zagaa taarifa kwenye mitandao nyingi zikieleza kuwa vengu hatunae duniani yaani (AMEFARIKI DUNIA)

Taalifa hizo zikapingwa vikali na meneja wa kundi kwa wakati huo sekioni maarufu kama seki lakini pia mwigizaji mwenza masanja mkandamizaji akakemea vikali kuhusu taarifa hizo huku akitanabaisha kuwa vengu yu ngali hai ila bado anaendelea na matibabu,

Post ya mwisho ya joseph shamba katika mtandao wa Facebook ilipostiwa march 6 2015 iliandikwa hivi "Baba wasamehe maana hawajui watendalo......Poleni wote mlioshitushwa na uvumi huo"
Tokea hapo hamna post nyingine iliowahi kupostiwa kwa page hiyo ya mtandao wa facebook

maswali yanaongezeka je joseph shamba aka vengu ni nini kimemchukiza hadi asitumie mtandao tena?

lakni je vengu bado ni mgonjwa?na kama ni mgonjwa basi ni mtu maarufu mtanzania wa kwanza kuwahi kuugua kwa kipindi kirefu...
vipi kuhusu Media na wasanii wenzake kutokutoa taarifa yoyote imuhusuyo mpendwa wetu huyu wamemsusa au?????

au amedaka kitengo sasa anaishi kwenye kivuli cha Cheti na jina lingine????
Masanja, Mpoki, macregan kipara,joti ,wakuvanga na seki tunaomba majibu
 
Kwa wasio mjua au wanaochanganya sura.

images (31).jpeg

Huyo hapo. Alikua anapenda sana kumuigiza Mrema, watu wengine walikua hawapendi kinoma.

images (23).jpeg

Hapo ndio alipotembelewa na Rais Mstaafu, JK.

Kuna huu uzi ulisema Amefariki India ila ukakanusha baadae.

Vengu wa Original Komedi amefariki dunia nchini India (Si habari ya Kweli)
 
Habar ya vengu huwa ni siri sana sijui kwa nn tu huku sisi wapenz wa vichekesho tuna ham ya kujua hali yake
 
VENGU WA ZEKOMEDI DUNIANI AU AKHERA?
Amefariki au yungali hai? na kama yu ngali hai yupo wapi na anajihusisha na nini kwa sasa?
ni maswali yalio katika vichwa vya watu wengi sana haswa mashabiki zake,
Asilimia 99 ya wapenzi wa sanaa ya maigizo Yale ya kuchekesha haswa mashabiki wa msanii vengu hawajui ni wapi alipo na wanatamani hata wangejua ni kitu gani kimejificha kwenye story ya maisha yake,
Ukweli ni kwamba Joseph Shamba ama Vengu kama wengi tumjuavyo tulianza mfahamu baada ya kujiunga na kundi la maigizo la zekomedi
Vengu alijitengenezea wigo mkubwa wa mashabiki waliokuwa wanapenda kuona jinsi alivyokuwa akimwigiza Mh.Mrema huku akibeba uhalisia wake,
Vengu alianza kuugua kidogokidogo mwaka 2009, lakini Agosti, 2011 hali yake ilikuwa mbaya, akalazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar. Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ aliwahi kwenda kumjulia hali.
Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, alipelekwa kwenye Hospitali ya Apollo nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejeshwa nchini akiaendelea kuuguzwa na familia yake huku taarifa zake zikiwa ngumu kupatikana
lakini cha kushangaza zilianza zagaa taarifa kwenye mitandao nyingi zikieleza kuwa vengu hatunae duniani yaani (AMEFARIKI DUNIA)
Taalifa hizo zikapingwa vikali na meneja wa kundi kwa wakati huo sekioni maarufu kama seki lakini pia mwigizaji mwenza masanja mkandamizaji akakemea vikali kuhusu taarifa hizo huku akitanabaisha kuwa vengu yu ngali hai ila bado anaendelea na matibabu,
Post ya mwisho ya joseph shamba katika mtandao wa Facebook ilipostiwa march 6 2015 iliandikwa hivi "Baba wasamehe maana hawajui watendalo......Poleni wote mlioshitushwa na uvumi huo"
Tokea hapo hamna post nyingine iliowahi kupostiwa kwa page hiyo ya mtandao wa facebook
maswali yanaongezeka je joseph shamba aka vengu ni nini kimemchukiza hadi asitumie mtandao tena?
lakni je vengu bado ni mgonjwa?na kama ni mgonjwa basi ni mtu maarufu mtanzania wa kwanza kuwahi kuugua kwa kipindi kirefu...
vipi kuhusu Media na wasanii wenzake kutokutoa taarifa yoyote imuhusuyo mpendwa wetu huyu wamemsusa au?????
au amedaka kitengo sasa anaishi kwenye kivuli cha Cheti na jina lingine????
Masanja, Mpoki, macregan kipara,joti ,wakuvanga na seki tunaomba majibu
Hii taarifa nimeona Twitter sasa sielew ni nan kamkop mwenzake au mhusika ndo wewe uko twitter mana siku hizi jamii forums siku hizi hakuna tena great thinkers watu wana copy kazi za watu bila ridhaa ya mhusika
 
Duh hadi FB !
 
Back
Top Bottom