Yule aliyesema watu wahame mjini warudi Shamba hakudhamiria, hawa ndio wamedhamiria. Akufukuzaye...

Yule aliyesema watu wahame mjini warudi Shamba hakudhamiria, hawa ndio wamedhamiria. Akufukuzaye...

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Yule wa ñyuma alisema atakayebaki Mjini mpaka Mwezi July ni mwanaume akiwa amelenga watu warudi vijijini hasa wasio na shughuli Rasmi, nakiri Leo hakuwa amedhamiria. Aliongea tuu. Pengine alisema lakini baadaye akaingiwa na Imani akahairisha.

Anyway,
Huyu wa Leo sasa naona hajasema lakini ndio hivyo, akufukuzaye hakuambii toka!

Mtajaza wenyewe.

Ukitaka kumfukuza mtu Mjini, nazungumzia kwenye jiji kubwa utapaswa ufanye mambo Yafuatayo Kwa ufanisi mkubwa;

1. Pandisha bidhaa bei kadiri uwezavyo
Hasa bidhaa nyeti zinazogusa watu moja Kwa moja uliowalenga, nikusaidie kuzitaja, pandiaja bei ya Unga na Mchele ambao wengi hutumia, pandisha Mafuta ya Kula, pandisha Sabuni ili washindwe kununua wawe wachafu wafubae. Pandisha viungo kama Karoti, hoho na vitunguu usisahau nyanya. Hawa watu watadhoofu tu nakuambia.

2. Pandisha bei ya Vifurushi vya mawasiliano na makato kwenye miamala ya simu.
Unajua wengi hawaweki pesa Benki si unajua hawana Account huko, pandisha vifurushi wasiwasiliane, alafu wasitumiane pesa Kwa sababu ni gharama.

3. Fukuza na ondoa shughuli zisizo Rasmi
Watu wasio Rasmi wengi wao ndio hufanya shughuli zisizo Rasmi.
Kuondoa shughuli zisizorasmi automatic utawaondoa kwenye mchezo watu wa chini na kuwawekea mazingira Magumu ya ku-survive Mjini. Wasiowavumilivu wataondoka mjini na kurudi shambani au kusogea miji mingine ya jirani.

Hivyo namna Bora ya uhakika ya kuwafukuza watu Mijini ni kuwatengenezea Mazingira magumu ya kimapato.

Anyway!
Ongeza shughuli za michezo ya kubahatisha ili waishi Kama Kunguru wakibahatisha maisha yao.

Ongeza watu mashuhuri wanaofanya vitu vya kipuuzi ili wawafanya bize hao watu.

Acha kwanza!

Watahama wasiowavumilivu, na waliowavumilivu watamenyeka kisawasawa.
Wao ni Kama Mbuzi Acha Wale urefu wa kamba zao. Wakati wachungaji wao wakiwa wamesimama Kivulini.

Ama vipi!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
 
Wao ni kula kulala KILA kitu bure wanaletewa mezani hawaoni tabu kuongeza figures tu
 
Kilicho baki
07405392bc7a31a8be5ea495aae63b9a.jpg
 
Teh teh teh mzee umetupa kitaulo ukakimbia uwanja. Kama wewe mwanaume kweli ungebaki mjini tukuone. Nasikia unashindia furu huko Chato!!
Nipo mjini!

Sijakimbilia kwa mabeberu kama wewe
 
Yaani huyu kiumbe ndiyo anachemshamsha kabisa.😥
 
Back
Top Bottom