Yule aliyesema watu wahame mjini warudi Shamba hakudhamiria, hawa ndio wamedhamiria. Akufukuzaye...

Yule aliyesema watu wahame mjini warudi Shamba hakudhamiria, hawa ndio wamedhamiria. Akufukuzaye...

Ataondoka yeye atatuacha

kulikuwa na hali ya ukapa yuko wapi
kila nyumba lazima ipande muarubaini nje ? yu wapi
hata mle nyasi itanunuliwa tuu
mpaka maji ya viroba yakapewa jina lake
nyumba kwa nyumba wanaume kupima tezi dume
wataishi kama mashetani

tumesurvive mapito mengi na still tunadunda na furaha tele
RAHA jipe mwenyewe ukisubilia matamko ya wanasiasa utasubiri sana

hvyo hata huyo atapita tu

Acha jeuri KIJANA

😀😀😀
 
Kaka mjini hatufugi fisi, Magufuli alisema watu wote watahama mjini na watakaobaki basi wao ni wanaume, sasa ukiona umebaki jipige kifua wewe ni mwanaume na ukiona hapakufai nenda kafuge bundi.

Kuna mapori mengi tu unaenda kulima asali, fuga nyuki mpaka wakuzoee wakikuona wanakushangilia.

Mie nilikuwa najiuliza hii influx ya watu kukimbilia mjini inatokana na nini na kwa nini matajiri wakarudi mashambani na wameshanunua maeneo makubwa kule Sasa sijui wale malaika wa Magufuli mtaishi wapi maana mjini pa moto na vijijini mlipakimbia mkiaminishwa matajiri wanakimbia mjini basi ndio wale walioitwa wanyonge wakawa wanaimba ule wimbo kwamba Sasa ni wakati wao (kipindi kile).

Hivi sasa kilimo kimeshikwa na wale walioitwa mashetani kipindi kile sasa masikini wamehama vijijini na wameuza maeneo yao, wale mashetani sasa wameshika kilimo na mjini wameshika masoko ni mwendo wa kula za uso tu.

Kiukweli wakati mwingine usifurahie mateso ya mwanadamu mwenzio maana nawe hujui siku yako inakuja lini.
Watu walikimbia vijijini baada ya kugundua huduma muhimu zipo mijini.
Vijiji vingi vilisahauliwa kupata hudumu za msingi,wakakimbilia mijini hasa miji mikubwa,matokeo yake na huko mjini kukafurika, kazi zikayeyuka na huduma zikawa shida.
Bei ya mazao au bidhaa itokayo vijijini huku mjini bei yake imepanda sana yaweza ikafika mara 10 wakati mwingine kuliko bei ya anayouza mkulima sababu inapitia kwa middle men zaidi ya watano.Kwa hali ilivyo ukishindwa kupata hata mlo mmoja kwa siku utakimbia mji.
Tuseme tu kuhamia mjini sio solution ya kila kitu wakati mwingine ni kuhamisha matatizo.
 
Ht hiyo bado bei ni ndogo, mnajua gharama za kilimo au mko mjini mnapiga tu kelele. Mchele kihalali unatakiwa uuzwe 2500 kwa kilo

Ili uwauzie Watanzania wapi hao ambao kipato Chao wengi wao hakifiki elfu 3 Kwa siku?

Na wengi familia zinaanzia watu watano...

Unachukulia mambo kirahisi Boss
 
Kuna jamaa yangu alikua round about kkoo kama miaka 8 hivi ... sasa hivi anatembeza bidhaa zake BAGAMOYO... dah mama samia sio mchezo
 
Kwema Wakuu!

Yule wa ñyuma alisema atakayebaki Mjini mpaka Mwezi July ni mwanaume akiwa amelenga watu warudi vijijini hasa wasio na shughuli Rasmi, nakiri Leo hakuwa amedhamiria. Aliongea tuu. Pengine alisema lakini baadaye akaingiwa na Imani akahairisha.

Anyway,
Huyu wa Leo sasa naona hajasema lakini ndio hivyo, akufukuzaye hakuambii toka!

Mtajaza wenyewe.

Ukitaka kumfukuza mtu Mjini, nazungumzia kwenye jiji kubwa utapaswa ufanye mambo Yafuatayo Kwa ufanisi mkubwa;

1. Pandisha bidhaa bei kadiri uwezavyo
Hasa bidhaa nyeti zinazogusa watu moja Kwa moja uliowalenga, nikusaidie kuzitaja, pandiaja bei ya Unga na Mchele ambao wengi hutumia, pandisha Mafuta ya Kula, pandisha Sabuni ili washindwe kununua wawe wachafu wafubae. Pandisha viungo kama Karoti, hoho na vitunguu usisahau nyanya. Hawa watu watadhoofu tu nakuambia.

2. Pandisha bei ya Vifurushi vya mawasiliano na makato kwenye miamala ya simu.
Unajua wengi hawaweki pesa Benki si unajua hawana Account huko, pandisha vifurushi wasiwasiliane, alafu wasitumiane pesa Kwa sababu ni gharama.

3. Fukuza na ondoa shughuli zisizo Rasmi
Watu wasio Rasmi wengi wao ndio hufanya shughuli zisizo Rasmi.
Kuondoa shughuli zisizorasmi automatic utawaondoa kwenye mchezo watu wa chini na kuwawekea mazingira Magumu ya ku-survive Mjini. Wasiowavumilivu wataondoka mjini na kurudi shambani au kusogea miji mingine ya jirani.

Hivyo namna Bora ya uhakika ya kuwafukuza watu Mijini ni kuwatengenezea Mazingira magumu ya kimapato.

Anyway!
Ongeza shughuli za michezo ya kubahatisha ili waishi Kama Kunguru wakibahatisha maisha yao.

Ongeza watu mashuhuri wanaofanya vitu vya kipuuzi ili wawafanya bize hao watu.

Acha kwanza!

Watahama wasiowavumilivu, na waliowavumilivu watamenyeka kisawasawa.
Wao ni Kama Mbuzi Acha Wale urefu wa kamba zao. Wakati wachungaji wao wakiwa wamesimama Kivulini.

Ama vipi!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Ni ukweli mchungu
 
[emoji769]Mh?
ROBERT HERIEL
 
Yaani huyu kiumbe ndiyo anachemshamsha kabisa.😥
Watu walimshauri akaange au aoke, akadai mafuta ^yata-two-me-car^ mengi. Ndiyo hivyo tena, ngoja ^key-la m-two^ ale kulingana na urefu wa kamba yake. Ila wasisahau kuna possibility ya kamba kukatika na kuvamia viunga vya wengine!
 
Ili uwauzie Watanzania wapi hao ambao kipato Chao wengi wao hakifiki elfu 3 Kwa siku?

Na wengi familia zinaanzia watu watano...

Unachukulia mambo kirahisi Boss
Kwahyo watu walime kwa hasara ili nyie wa mjini mle tu kwa bei mnayoitaka. Bado bei ya mazao ipo chini huo ndio ukweli
 
Back
Top Bottom