Yule bibi wa Ngende aliyekuwa akigawa vyeo na utajiri amekufa

Yule bibi wa Ngende aliyekuwa akigawa vyeo na utajiri amekufa

ndio zao, unaweza ona sharti linasema

Huruhusiwi kuwa na Wanawake zaidi ya watatu.

Haraka haraka unaona wanawake watatu tena wazuri niwapendao,wanantosha sanaaa.

Kimbembe kinakuja ukishawapata hao watatu uliojiridhisha ndio wazuri, Hawa wazee wanakuletea PISI WALIZOZIUMBA WAO WENYEWE SASA, unapitishiwa viumbe ambavyo ukifananisha na wake zako unaona ni kumdhihaki muumbaji.

Tena Pisi zenyewe unazoletewa zinajirahisisha kwako yani ni kugusa tu, Sasa Jichanganye Usahau Masharti yako.
Unamuacha mke mmoja unachukua pisi nyingine..hesabu inarudi kwenye tatu palepale
 
Kitu ambacho wengi hawajui ni kwamba hayo masharti huwa hayawezi kutimizwa kwakuwa yana roho ya miujiza ndani yake mfano; wanaume wengi kuchepuka ni kawaida lakini ikumbukwe kuwa wapo wasio chepuka na wanasababu, sasa mtu kama huyu asiyechepuka akipewa sharti la kutochepuka na mganga tayari roho ya kuchepuka humwingia na hakika atachepuka alimradi tu sharti livunjwe ili aharibikiwe yaani arudi nyumbani umasikinini.
Kuna ndugu yangu alichukua hilo sharti la kujisaidia popote lakini siyo nyumbani anakoishi kuna siku aliamka tumbo limemkamata ile anapiga hatua moja ya pili aliharisha karibu nusu kindoo kila kitu kikaishia hapo yupo kijijini anachoma mkaa
 
Wanachofanya Waganga Wachawi ni kuku unganisha na ulimwengu wa Giza.
Kwa hali ya hapa kwetu Tanganyika mtu ukiwa na bidii ya kazi huwezi kukosa mahitaji muhimu.

Tuna ardhi kubwa yenye rutuba nzuri, tuna Bahari. Tuna Maziwa makubwa, tuna mito ya uhakika.

Kwanini uuze roho yako kwa Ibirisi Shetani kwa vipande thelasini vya Fedha?

Ibirisi Shetani kamwe hakupi pesa kwa kukupenda.
Mashetani na Malaika zao Majini baada ya kufukuzwa Mbinguni yanahangaika kutafuta watu ili nao waukose Ufalme wa Mbingu.
............
Surah Al-Djini Ayah 8

وَأَنَّا لَمَسۡنَا ٱلسَّمَآءَ فَوَجَدۡنَٰهَا مُلِئَتۡ حَرَسٗا شَدِيدٗا وَشُهُبٗا
Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.
...........
Itakufalia nini ukipewa mali zote za hii dunia na ukaukosa Ufalme wa Mbingu?
Duniani unapoishi kwa miaka mia moja tu tena kwa taabu nyingi sana.
 
Back
Top Bottom