Huyu Waziri wa Ardhi naona kama ni mnafiki tu, Kama KWELI yuko serious kabisa katika kutatua Migogoro ya Ardhi hapa nchini Tanzania, basi aanze kuifanyia marekebisho Wizara yake anayoiongoza kwa sababu hiyo ndio kinara wa kusababisha Migogoro ya Ardhi.
Awasulubu kwanza Watendaji wabovu wa Ardhi wanaohusika kwenye kusababisha Migogoro ya Ardhi, bila kusahau KUPELEKA MAANGAMIZI MAKUBWA KWA WENYEVITI WA MABARAZA YA ARDHI YA WILAYA (Mahakama za Ardhi) ambazo karibia zote kabisa zilizopo zimetekwa mateka na Matapeli na/au Waporaji wa Ardhi. Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya ni janga kubwa Sana kwa Wamiliki wa Ardhi hapa Tanzania, yamegubikwa kabisa na VITENDO VYA RUSHWA. Watu Wananchi maskini wamekuwa wahanga wakubwa wa kuporwa Ardhi zao na Matapeli wa Ardhi au Watu matajiri, Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya yamekuwa yakibariki Utapeli au uporaji huo. Awashughulikie kwanza hao Mahakimu wa Mabaraza hayo, kwani nao ni Waajiriwa wa Wizara yake ya Ardhi.