Yule Mzee aliharibu maisha ya Mabinti wengi Ila yangu aliyaharibu na kuyatengeneza mwenyewe

Yule Mzee aliharibu maisha ya Mabinti wengi Ila yangu aliyaharibu na kuyatengeneza mwenyewe

tiny and tempting to use as a whistle 😬😬

huge ukasukumie chapati🤣 I can see how many ideas you have

Beaty and Beast Clepatina 😊
Mkuu Gily you have bn a blessing.
You really make me happy,😂😂.
Long may you live ndugu yangu🙏
 
Maisha ni mafupi sana. Juzi tulikuwa na rafiki yetu leadermoe leo hayupo. Unatakiwa uishi na ukiisha kwenye ulimwengu wa past hiwezi ona future. Put everything behind and start living. .
Amen mkuu.
Kuacha mizigo ya jana ibaki jana na kuitazama kesho ktk mwanga chanya wa matumaini.
Pole sana kwakuondokewa na rfiki yako.
Japo sikumzoea ila iliniuma.
 
Amen mkuu.
Kuacha mizigo ya jana ibaki jana na kuitazama kesho ktk mwanga chanya wa matumaini.
Pole sana kwakuondokewa na rfiki yako.
Japo sikumzoea ila iliniuma.
Maisha ya mwanadamu ni hadithi. Nataka nisimulie na mimi ya kwangu nikumbukwe kwa mazuri pia...
bado machungu ni mabichi sana tuombe mwisho mwema. .
 
EP. 4

Kwa mliosoma story yangu ya Mzee Kipipa Ep. 3 kuna mahali nilieleza kuwa nilimsumbua sana mzee Kipipa mpaka akataka kukimbia nchi.

Nitakuja kueleza kwa kirefu ila kwa kifupi ni kwamba kuna siku chuki dhidi ya mzee Kipipa na uncle ikawaka na kiu ya kisasi ikawa kali kiasi nikatamani nione wakilipa kwa waliyonifanyia.Kuna nurse fulani wa hospital ya mission aliyenitibu wakati nimepata ile infection na mmoja wa aliyekua akinibembeleza nitaje anayeniingilia ila kama mnakumbuka nilikataa kutaja lkn siku hii roho ya kulipa kisasi ikanijaa na mbio nikaenda hadi pale hospitali kumtafuta yule nurse.

Nilipofika kwa nurse nikamwambia niko tayari kutaja watu wanaoniingilia ila nikamuomba aniambie kwanza kama nikiwataja watafanywa nini?

Nurse akanitizama kwa muda akinisoma kujua lengo la swali langu kisha badala ya kunijibu akaniuliza"Wakipewa adhabu kali utawaonea huruma au utafurahi?".
Nikajibu nitafurahi kisha akasema"Ikidhibitika kuwa ni kweli wanakufanyia hivyo watafungwa jela"
.Nikajikuta naropoka "Hata wakifungwa jela bado sitakua na furaha".
Nurse:Wakifungwa jela hawataweza kukubaka tena wewe au watoto wengine
Mimi:Sawa lakini natamani wapate adhabu ambayo itanifanya niwe na furaha!
Nurse:Kwa hiyo Clepatina mwanangu unafikiri adhabu gani itakufurahisha wakiipata mbali ya jela.

Baada ya yule Nurse kuniuliza lile swali nilisimama nikatizama chini kwa muda kisha nikanyanyua kichwa kumtizama na kwa upole nikamjibu"Kusema ukweli sista kwa sasa sijui adhabu inayowafaa ila ninachokijua kwa hakika ni kuwa adhabu ya jela haiwatoshi" kisha nikapiga alama ya msalaba kisha nikageukia mlango nikaanza kutoka kuelekea nyumbani kwetu.

Sista yule alinikimbilia,akanishika na kunibembeleza niwataje wanaonibaka na kuniahidi mambo mengi mazuri iwapo nitawataja ila nikagoma na kurudi zangu home.

Nilipofika home nikaenda hadi kitandani kwangu nikajitupa nikaliaaa kisha nikajifuta machozi nikakaa nakuwaza ni nini kikifanyika kwa mzee Kipipa kitanifurahisha.

Nilitamani niwafungie sehemu halafu kila siku nikiboreka niwe naenda kuwatesaaa waumiee walieeee waniombe msamaha halafu siwasamehi.Nilitamani wapate wapate mateso hadi watamani kufa ila wasife.

Niliwaza na kuwazua mpaka usiku ukaingia na kukacha ila sikupata jibu la adhabu ipi ni kali kuliko jela ila moyoni mwangu kuna sauti (nina hakika ni ya shetani) ilikua inanipa moyo kuwa nisijali adhabu ya kuwafaa itapatikana tu cha msingi nisiwasamehe,nisikate tamaa na nihakikishe hawaendi jela.

Hakuna siku iliyopita bila kufikiria adhabu ya kumpa mzee kipipa na siku moja nikiwa naangalia filamu ya kimarekani kuhusu mafian cartel of mexico kwenye tv aliyonunua step maza kwa pesa za mzee Kipipa na pamoja na kuwa sikua najua kiingereza ila kwa vitendo tu nilipata wazo la nini cha kumfanyia mzee Kipipa.

Hawa Mexican mafian cartel waliku a wanafanya maasi kujipatia pesa zisizohesabika kiasi kwamba hata serikali haikuweza kuwagusa.

That movie Inspired me to be a mafia.I wanted money too sababu niliamini kama sio umasikini nisingepitia niliyopitia na niliamini nisipokua na pesa nitaendelea kunyanyasika maisha yangu yote na moyo wangu haukua tayari kuendelea kuteseka zaidi ya nilivyoteseka.

I hated umasikini sbb huo ndio uliosababisha nipitie niliyopitia.Hivyo nilitaka umafia wangu niutumie kumuadhibu mzee Kipipa kwa style itakayonitoa kwenye umasikini.

Hapa nilikiwa na kama 14 yrs hivi na tayari nilikua nawaza vitu ambavyo watu wengi mpaka wanazeeka wanakufa hawaviwazi na mawazo yangu mengi yalikua ya kishetani.Nilikua mtoto wa shetani.Nilikua na roho ngumu na mbaya.Sikua na huruma wala roho ya kusamehe.

Mara nyingi nilikua nakaa peke yangu na ikitokea unanikuta naongea na mtu basi atakua ni mtu mzima na itakua kuna jambo namdadisi.

Nilitaka kumfanya mzee Kipipa awe anaishi kwa kufuata amri zangu mpaka siku kifo kinamuondoa mmoja wetu.Nilitaka kila akinifikiria aogope.Nilitaka akiota ndoto mbaya jina au sura yangu viwepo kwenye hiyo ndoto.Nilitaka kila anapopumua ajutie kosa la kunibaka.Nilitaka alilaani dushe lake lililomponza kuniingilia.

Pamoja na u teenager wangu nilijua bila pesa kisasi kwa mzee Kipipa kitabaki kuwa matamanio daima hivyo nilipanga niwe na pesa na watu wazito nyuma yangu.

Tajiri pekee niliyemjua na niliyetaka kumfanyia umafia ili nijipatie pesa alikua ni mzee Kipipa.

Mtaji pekee niliokua nao katika project yangu ya umafia ilikua ni urembo na akili na mpango wangu wa mwanzo ilikua ni kum seduce mzee Kipipa kimapenzi lakini niligonga mwamba.Kwanza kabisa Mzee Kipipa hakua bwege,alishajua simpendi na hata chakula alikua anapata kutoka nyumba nyingine kwani nilikataa kuendeleza hiyo huduma na kwa mkwara niliomcjimba siku anarudi tena kijijin vilifanya kujisogeza kwangu kwake anione nyoka.

Mbali ya hivyo pamoja na miaka yangu 14 mzee yule alishanikinai na kuniona mbibi na alikua na katoto kengine ka miaka 9 hivi kanakompelekeaga chakula.

Mpango wangu huo ukafeli na nikawa sijui cha kufanya ila ile sauti ya kunitia moyo wa kutokata tamaa juu ya kulipa kisasi ikaendelea.

Kitendo cha mzee Kipipa kuniona simfai tena baada ya kunichezea
kiliongeza kiu ya kisasi na siku moja kwenye uzinduzi wa ile shule yake akiwa mgeni rasmi ni mzito mmoja serikalini huku waandishi wa habari,wafanyabiashara wakubwa wa Dar na vigogo mbalimbali wakiwa ni wageni waliohudhuria nilipata Plan B ya mpango wangu.

Viongozi wa wilaya,kata na kijiji walikuwepo kushuhudia ufunguzi wa shule kubwa ya boarding ya wasichana.Mzee Kipipa na mkewe na watoto wao walikuwepo.

Yule mjukuu wa ulaya niliyeambiwa nimefanana nae alikuwepo na nilimtambua baada ya kila aliyekuwa karibu yangu kusema tumefanana sana sura kasoro umbo yeye ni flat screen.

Kabla ya kukaribishwa mgeni rasmi mzee Kipipa alitoa hotuba fupi iliyonichefua sana.Alikemea vikali na kuiomba serikali itunge sheria kali dhidi ya watu wanaowanyanyasa watoto kingono.Nilikasirika hadi nikaapa huyu mzee pumzi yake ya mwisho lazima niikatishe mimi.

Katika mkusanyiko ule mimi ndio nilipendeza kuliko ke wote waliokuwepo pale.Wanawake wa Dar waliniangalia kwa wivu huku wanaume zao wakiniangalia kwa uchu na mpaka ule uzinduzi unaisha nilijipatia namba nne za watu wazito kutoka Dar mmoja wao akiwa rafiki na connection nzito ya mzee Kipipa.

Miezi mitatu baadae nilienda Dar kwa kwa ufadhili wa wanaume hao ila kwa kutumia hela zao nilijitafutia makazi na kisha kuwadanganya kuwa nimefikia kwa mjomba na nilifanya hivi kwani nilijua wananiita wanitumie kingono nami sikutaka kutumika.

Kila mmoja bila kujua kuwa kuna wenzie alifadhili maisha yangu mapya ya Dar na kwa vile nilijua wakishanivua nguo sitakua tena na nguvu juu yao nikawa nawachezea mchezo wa sitaki nataka mara nisamehe nimeshindwa kuja mjomba kanikataza nisitoke mara kesho vile mradi tu nilinde mbususu yangu huku nikipanga mipango ya kumuadhibu Kipipa.

Kupitia kigogo na rafiki ya mzee Kipipa nilifanikiwa kumjua mzee Kipipa vizuri.Niliujua uimara na udhaifu wake ulipo na kikubwa nilifanikiwa kujua njia zao za kupiga deal chafu.Nilichofanya ni kuwagombanisha yeye na rafiki yake Kipipa.Devide and rule thing kisha taratibu nikajitoa kwenye hali ya kuonekana ninafaa kwa ngono tu na kujipatia nafasi ya kuwa kwenye business lunches and teas na kupata heshima ya beauty with brain.

Pamoja na kuishia la nne nilipata ofa ya ajira ila nilikataa.Nishaona kuna pesa nzuri zaidi ya mshahara na ndizo nilizozitaka.

Kupitia huyu mzee Kigogo nilipata connection nyingi kubwa na kupitia uadui kati ya huyu mzee nikaanza rasmi kumuadhibu Kipipa.

Baada ya kumsumbua sana Kipipa akaona suluhisho ni kuniua na alifanya jaribio la kuniua mara mbili ila akashindwa.Aliposhindwa kuniua akajaribu kuhamishia miradi yake nchi jirani ila haikua rahisi na mwishowe akanifata tukae mezani tuyaongee.

Akaniomba nihamie nchi za nje na akaniahidi kufadhili kila kitu cha hiyo safari.Kwa ushamba wangu nikadhani ulaya ukishafika tu kule na kuvuta ile hewa yao unakua tajiri.Na pia nilikubali kwenda kuishi ulaya nikiamini kwamba siku nikimuua sitakuwepo nchini kukamatwa.Nikakubali na akanipeleka Sweden katika mji uutwao Göteborg.

Hata hivyo baada ya kukaa kule kwa miezi minne na kuelekezwa mchakato mzima wa maisha ya pale ikiwa ni kutafuta kibabu kinioe ili nipate uppehåltillstånd(resident permitt) au nijipe ukimbizi na pia kwenda kufanya kazi za usafi na kusambaza magazeti asubuhi asubuhi nukaona huyu mbabu Kipipa kaniingiza cha Kike.

Nikawaza deal za hela ndefu wanazopiga kina mzee Kigogo na mzee Kipipa halafu nikalinganisha na future yangu pale Göteborg nikasema huu ni ungese.Narudi bongo.

Mzee Kipipa baada ya kujua nimepanda ndege hakutaka kunijua kwa heri wala kwa shari wakati na mara chache alizopokea simu yangu alinijibu shit.Nikasema hiiiiiiii kwani huyu mbabu anazani hapo bongo ni ahera siwezi kwenda.?

Siku ya siku mzee Kipipa alikua kwenye conference fulani kwenye hotel moja kubwa yuko mbele pale anaongea.Nikamuingilia pale huku natembea kisela natafuna big g nimepiga cape ya cardet ya kijani,miwani mikubwa,jeans tight,shati na chini safari buti.

Ma gentle men wale walikua wakishangaa hili lisichana lihuni lihuni kama livuta bangi limefata nini hapa lakini mzee Kipipa yeye alionekana akiniangalia akiwa ameishiwa nguvu asiamini kama jipu lake la kwapa limeeudi tena.

Mi sikuwajali wale wavaa suti pale ila nilienda mpaka kama hatua sita na alipo mzee Kipipa kisha nikamwambia kwa sauti ya juu " We gat to talk" akaniambia kanisubiri kule restaurant ila nikamuonyeshea saa then nikamwambia "Kama huna muda naweza hata kuongelea hapa" then nikavuta capelo karibu ya pua then nikaweka mikono mfukoni nikawa namuangalia.

Bila kusema chochote mzee Kipipa alitoka na mie nikamfuata kwa nyuma.Tulivyofika rastaurant kabla hajasema chochote nikamwambia "Hivi wee mzee mbona unapenda sana kucheza na maisha yangu?"
Akatikisa kichwa kisha akasema"Kwanini umerudi Tanzania mapema hivi?".

Nikamwambia"Nikae ulaya kufagia barabara za wazungu halafu kazi ya kukuua nimuachie nani?,

Hakunijibu kitu bali akanitizama tu kisha nikamwambia "Kesho nakuja ofisini kwako kuna kazi nataka mimi na wewe tufanye na sitegemei usumbufu wala janja janja".

Akasema"Niambie unataka kiasi gani cha fedha nikulipe haya mambo yaishe niwe na amani".

Mimi:Huna uwezo wa kunilipa mimi wewe mzee!Hapa ni tufanye kazi tupate
hela hayo ya kukosa amani uliyataka mwenyewe ulivyokua ukinibaka".

Nikasepa zangu na kumuacha pale akiwa anakuna kuna kidevu chake kipana ka sahani ya mama lishe.

NB:Mbali ya kusoma historia yangu ili uburudike nataka ujifundishe kitu hasa wewe mwenye tamaa ya utajiri wa haraka.Ukisikia mtu anakwambia umlipe akuunge freemason huyo ni tapeli.Wanachama wa freemason ni watu ambao tayari ni wazito kwenye jamii.Wanasiasa wakubwa,wana michezo wakubwa,wanamuziki n.k.Hayo mabango ya freemason ni utapeli,hata mimi ukinifata DM kuhusu freemason nitakutapeli.Freemason is by connection na uwe mzito.
Nimejisikka tu kutoa somo ila usitake kujua ni kwa nini wewe jifunze tu usitapeliwe.

Sisy Joannah darling bro Half american wifi ake Leejay49 big broh Gily bestie Equation x Analyse cocastic Dr. Mariposa mshamba_hachekwi Depal Dejane Lucha Darlin Shunie To yeye Glenn Mad Max Lovie Lady an alpha male Unique Flower Chizi Maarifa Palina mshamba_hachekwi dronedrake




My daddy .....
Daah! [emoji848]

Sent from my SOV37 using JamiiForums mobile app
 
nimeishia kwenye masifa ya verse ya kwanza sipendi mtu mwenye masifa.
 
Back
Top Bottom