Yunus Nassoro Ali, akamatwa kwa kujifanya mtumishi wa Usalama wa Taifa "TISS"

Huyu jamaa kwa ufupi ana akili nyingi sana kwenye upande wa forgery.

Master forgery na ilitakiwa serikali imchukue imuajiri huyu anayajua matatizo ya wananchi maana inaonekana huduma yake anaitoa kwa wananchi directly halafu bila kupiteza muda.

Nadhani watu wakitaka kupita na mizigo ku jifanya ya serikali, au ya jeshi huyu anakutolea barua zina letter head na logo, anakupa plate number hata DFP, huyu akisafiri na gari njiani trafik akimsimamisha anamfinnyia kitambulisho chenye bibi na bwana anachiwa nenda mkuu.

Huyu shida ndogondogi sijui za passport, cheti cha nida, kujifanya afisa taskforce ya kujusanya ushuru na mapato, Kukusanya hela kwa niaba ya serikali toka kwa wafanyibiashara inaonekana ndio mapigo yake. Ni mtazamo tuu simjui ila mwamba inauwezekano aliwahi kuwa jeshini au chombo kingine cha usalama akaufukuzwa kazi huwa wengi wanakuwaga hivyo.
 
Kadi ya gari ya Shein kaipataje?
Original au copy?
 
Waliyomkamata ndiyo wamekutumia hii picha au wewe ni miongoni mwa mliyomkamata?
 
Wewe inaonekana hata Movie huangaliagi

TISS na POLICE ni idara mbili tofauti kimuundo, kimajukumu na kisheria, POLICE wana oparesheni zao na TISS wanaoparesheni zao

Mara nyingi watu wa TISS wakiwa kwenye oparesheni huwa hawajulikani na wanafanya kimya kimya na huwa hawataki kabisa police ijue maana ikijua wao wanaweza kubanwa na sheria

Mtu kama huyo huenda alikuwa kwenye mission ila kakamatwa na police usishangae kumkuta anadunda mtaani

Hii ni experience yangu niliyoitoa kwenye movie za kikorea
 
Huyu itakuwa kachokwa tu.yaani kadi ya gari ya rais anakaa nayo ya nini?.
Majibu ya alama za vidole kwake yeye vya kazi gani?
Is not professional kama wadau wengi wanavyodhani. Why keeping too much unnecessary necessary stuffs
 
na ndomaana hata kwenye iyo picha jamaa karilax kabisa yupo komfotable hana wasiwasi kabisa, anajua tu hapo wanajisumbua hawana pa kumpeleka wala cha kumfanya.
 

Hahahahaha movie na reality ni tofauti kabisa ingawa mengi wanatoa kwenye uhalisia ila mengi ni mambo ambayo hayawezekani in a real life

Sasa huyu mwamba vitu vyote hivyo iwe mission kivipi yaani mpaka vitu vya Rais mstaafu vya nini
Hebu angalia orodha hiyo number plates zote hizo Ina maana kila mission anabadili namba ama
Hata kama ni mkuu wa TISS hawezi kuwa ana namba zote hizo hata awe na mission za 007 hajafika huko
 
Huyo jamaa ni TISS kweli. Huwezi kuwa na documents zote hizo kwa kufoji au kufanya matukio. Huyo ni mwenzao ila namna alivyonasa ndio hawajaeleza na itaishia juu juu aachiwe

Basi inawezekana alikuwa anaziiba ofisini kwao na amekusanya kwa mda mrefu sana

Wengine huwa wanaiba vitu na kufanya kama souvenirs ila kwa huyu mwamba hizo souvenir zimevuka kiwango

Nimekumbuka kuna serial killers au rapist huwa wanabaki na vitu vya watu waliowauwa kama chupi au viatu au ID zao

Kwa huko ni ngumu sana kuweka ukweli wa huyu mwamba alikuwa ni nani haswa maana kama ni mmoja wa wapelelezi hawawezi kumsema kwani mpaka sasa polisi wana doa kubwa katika jamii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…