Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Hawa ndo wababa wenye umama ndani yao hawakawii kuesabu minofu ya nyama
Si vizuri kumlaumu yeyote kwa life style anayoishi. Maana si sahihi watu wote kuwa na jibu moja kwa hili, inategemeana na kipato cha mwanaume au wote mwanaume na mwanamke, pamoja na Aina ya mwanamke ulienae, Kama ambavyo tumeona baadhi ya wanawake kulaumiwa, wakati huo tumeambiwa tuishi na wanawake kwa akili, Basi ndo akili hiyo kuwa flexible pale unapohisi kutomwelewa mwenzio kuliko kugombana.
Hata ivo mada hii iliwahusu zaidi wanawake waeleze Ni mwanaume yupi wanamwona Bora zaidi, ingawa wachangiaji wengi nikiwemo Mimi tumechangia out of point katika kile kinachoitwa kueleza hisia zetu..
 
Kuna wanawake si wezi wakiachiwa pesa hawana wazo hata chembe la kuiba watanunua kila kitu sawa sawa, sasa wala wenye tabia ya wizi ogopa kabisa! Ukimuachia 400,000 kwa siku anawaza aibe ngapi kwa siku/mwezi ili apeleke kwenye vikoba
Mie napewa na nimeshazoea hivyo na husband anasema inamsaidia kuwaza vitu vingine
 
Mimi naacha pesa ya mboga tuu ambayo naona mimi inafaa na sio kila siku

Mtu umemfungulia biashara afu akiuza pesa anapeleka wapi? Lazima mambo yake binafsi atoe humo,mboga atoe humo ila vitu vingine vyote vya lazima nitafanya

Siwezi acha pesa ya eti mwezi kwanza haitafika na ukiacha kila siku itakuwa utumwa lazima na yeye awajibike na niliishiwa navuta pesa zake saafi maana mimi ndio natoa mtaji

Hata simba ,majike wanasaidia kuwinda au sio kusaidia ila wanazaa kulea na kuwinda
 
Kuna wanawake wengine unamwachia pesa ananunua vitu substandard , anapeleka pesa, vikoba, na kuservu pesa ya bia

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanawake ukimpa pesa anachukulia ni zawadi atafanya lolote na huna cha kumfanya hasa kama umeshikwa

Jamaa yangu alimpa mke mil.4 amalizie nyumba ,jamaa anaishi mkoani pesa ilikoenda haijulikani nyumba haijakamilika mwanamke anadaiwa vicoba na vyombo ndani baadhi vilichukuliwa,ukiuliza mwanamke hakuna majibu.

Jamaa mwenyew amebak kulia Lia na kutukana mwanamke ko unaweza ona japo jamaa mwenyew mpole yaani simuelewagi
 
Mimi kila kitu nanunua .

Na pia nitampa Pesa kwaajili ya Mambo mengine ambayo sio lazima aniambie.



Haya mambo ya kuacha Pesa mezan kila siku , yanafanya Mwanamke aweke akilin Pesa sana,kuliko kukuweka wewe akilini.
Hata mm huu utaratibu siukubali na Sikuwahi uona kwa mzee,nachofanya ni kumfungulia biashara ndogo ikifa kwa uzembe ajiandae kuwa beki 3 kwa sisi ambao wake zetu sio watumishi
 
Habari za saizi wakuu,

Poleni kwa majukumu ya kila siku moja kwa moja niende kwenye point.

Kati ya hawa ni yupi mzuri zaidi, mwanaume anaeacha pesa ya matumizi nyumbani na mwanamke ndio anaepanga matumizi au mwanaume anaenunua kila kitu cha ndani na kama kuna matumizi ya ziada yakubidi uombe pesa kwa kutolea maelezo.
Kuacha pesa au kununua na kuleta mahitaji nyumbani itategemea na akiki za mwanamke.
Kuna baadhi ya wanawake hupenda kununa vitu wanavyotaka badala ya wanavyohitaji.
 
Kuna siku wife nlimuambia kuwa hata kama hii pesa ya gesi nikikaa nayo mimi lazima niitoe tu pale ambapo gesi itaisha hivyo hakuna faida ya kukaa nayo mimi wakati ina matumizi yake ambayo lazima itumike,sasa kukaa nayo nafaidika nini ?

Ingekuwa ukikaa nayo na matumizi yanapungua hapo sawa

Alafu kitu kingine ni kuwa naona inanijazia wallet tu wakati sio yangu ile pesa.

Alafu ukikaa nazo mwanaume pesa za matumizi stress zinazidi unaona unatoa tu pesa,unatoa tu pesa,unatoa tu pesa,unatoa tu pesa,unatoa tu pesa,unatoa tu pesa unatoa tu pesa mpaka unajiuliza heee inakuwaje pesa inaenda hivi,kumbe ungemuachia wife kila kitu wala yasingekuja mawazo hayo
Kwani bajeti huijui Hadi uone shida? Tunachokwepa hapa ni kuacha pesa ya mwezi afu isifike ,hakuna rangi utaacha kuona , wanawake Wana tamaa za vitu vizuri
 
Unatoa tu pesa,unatoa tu,unatoa tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119] mwishowe zinaanza kukuuma.

Bora akae Nazo mke.

Nyie sasa ndio wanaume[emoji122]
Ukisikia huyu kama Ana roho nzuri ujue mtu kaliwa ila kinyume chake sasa hapo ni bajeti kali
 
Yaani eti mwanamke unakaa huna hata mia mbovu.
Kuna baadhi ya mapochopocho mwanaume hawezi nunua yote kama jinsi unavyotaka.

Vitu vikiisha anaanza kukununia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ena,ndagha fijo
Acheni ujinga vitu vya jikoni hakuna mwanaume ananunua,by ni vihela vidogo dogo ila items zinazohusu pesa nyingi nafanya mwenyewe
 
Mimi nanunua vitu muhim kama sukari, unga, mchele, mafuta n.k..alafu naacha kodi ya meza daily maana wakati mwingine wife akiwa pekeeyake hapiki ananunua msosi. Pia namkabidhi akiba wife incase of anything mf Siku naweza kwama.
Kwamba huwez tunza pesa unamkabidhi akiba [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] umenichekesha we jamaa
 
Mimi kipato Changu ni cha kuunga unga
Mara nyingi huwa kuna issue nasikilizia.
Kila Mwisho wa Mwezi huwa nampa 900,000/= TZS cash kwa Matumizi yafuatayo

1. Chakula cha Mwezi mzima (Mimi + Yeye + Dada wa kazi + Mtoto Mmoja)
2. Bills za Umeme
3. Maji
4. King’amuzi Azam
5. Mshahara wa Dada wa kazi
6. Vitu vya Mtoto Mdogo Diaper
7. Nguo za Mama na Mtoto
8. Vinywaji Soda na Juice
9. Vocha ya Mama
10. Nauli zake za kuzurura Nyumbani (Yeye ni Mama wa Nyumbani)

Majukumu yangu
1. Emergency za hapa na pale nahusika
2. Kodi ya kibanda tunachokaa
3. Ujenzi
4. Mafuta na Marekebisho ya Pikipiki ya Familia
5. Afya na Matibabu
7. Mambo ya ndugu , wazazi marafiki
8. Uwekezaji
9. Ukarabati wa kitu Chochote cha Nyumbani
10. Matumizi yangu Binafsi Mjini
11. Michango yote ya Mtaani, Jumuiya, Kanisani

Sasa hapo sijui niko sawa au kuna sehemu nazingua . Ushauri wenu wakuu
Umetisha Sana kwa hiyo bajeti ya kipato cha kuunga unga,uko sahihi sana
 
Kwani bajeti huijui Hadi uone shida? Tunachokwepa hapa ni kuacha pesa ya mwezi afu isifike ,hakuna rangi utaacha kuona , wanawake Wana tamaa za vitu vizuri
Mkuu kama wewe mkeo ni mfujaji mfundishe asifuje kisha ndo umpe pesa ya matumizi.

Sisi wenye wake ambao sio wafujaji wanaionea pesa ya Mume uchungu acha tuwape tu pesa ya mambo ya ndani kisha sisi tunaumiza kichwa na mambo mengine.

Sio lazima ufuate formula za wengine utaumua mkuu.
 
Back
Top Bottom