Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Nilikua naacha pesa nikalishwa sana maharage na majani kama mbuzi wakati mimi siwezi kula mlo usiokua na nyama au samaki nikaona usinitanie..jpil najaza friji vitu navyopendelea halafu namwachia vichenji chenji ya kununua tu viungo viungo...
Still bado unafanya vyema
 
Wanawake kwa asilimia kubwa ni wazuri katika kupanga matumizi hasa ya nyumbani na inawapa fahari fulani ukimpa madaraka ya nyumbani anakuwa anajisikia kuwajibika kwa kiasi fulani. Mimi huwa na mpa mke wangu pesa za matumizi yeye ndio boss wa mambo ya ndani mimi na deal na mambo ya nje. Tunagawana madaraka ila wanawake kwa ujumla ni wazuri katika kusimamia budget ya nyumbani.
 
Mimi nanunua vitu muhim kama sukari, unga, mchele, mafuta n.k..alafu naacha kodi ya meza daily maana wakati mwingine wife akiwa pekeeyake hapiki ananunua msosi. Pia namkabidhi akiba wife incase of anything mf Siku naweza kwama.
 
Back
Top Bottom