Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Umeongea pointi sana, haya vijana ambao hamjaoa pitiezi huu uzi huu ndio ukweli

Kama mkeo unampa pesa na anapanga budget inaenda vizuri sema asante Mungu

Maana wapo wanawake ni vimeo hawafai kuachia hata buku anunulie watoto mkate wa chai asubuhi utashangaa watoto anawapa chai kavu yeye anaenda kwenye vikoba
 
Vijana wa siku hizi wamekuwa wagumu kuelewa hili then
 
Kununua vitu vya mwezi mzima ndo mpango
 
UZI UMEUFUNGA WEWE! SALUTE! JABALI!
 
Nawe una kitu cha kufundisha, asante, nimeelewa na kujifunza kitu hapo
 
Ipo hivi: ukitaka kuwa na maisha marefu na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea na mkeo, pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha muache mkeo awe na jukumu la kuratibu mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi fungu husika hata kama limetokana na michango yenu wawili. Wanawake WENGI wanajua sana kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata kama utakuwa umeishiwa! Na michango ya wengine hapo juu ipo vizuri sana.
 
Dah, wotehao siku hizi hawapo, utafiti wangu wenye risachi ndogo 50% ya wanaume wetu hawa hawajui kununua ila pia wote hao wanajua kuwa wanasaidiwa!
 
Inategemea na jamii husika na mazoea ya malezi. Nimekua nikiona baba yetu anaenda sokoni na anapika akiwa na muda, nimeoa mwaka wa 8 sasa ktk familia yangu kwenda sokoni ni jukumu la baba na huwa napika nikiwa na muda.
 
[emoji109][emoji109][emoji109]
 
Kiukweli binafsi nikiwa nina bajeti nzuri huwa naomba kujua orodha ya mahitaji ya ndani. Kama nipo nanunua kila kitu,kama sipo napiga simu anaenda kwa Mangi kinanunuliwa kila kitu kama alivyohitaji yeye (sitaki lawama). Baada ya hapo namwachi ki elfu kadhaa cha Emergency.
Basi! Suala la kumuachia hela afanye yeye kila kitu cha ndani/jikoni hiyo nadhani sijafikia status hiyo. Ikifika nitafanya nione inavyoenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…