Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Ukipata mwanamke mwenye financial discpline hamna shida. Kuna wengine unamwambia piga budget ya mwezi,anapiga unampa. Hata nusu mwezi bado anakwambia hela ya chakula imeisha,ukifuatilia vzr ametumia kwa mambo ya kipuuzi. Kuna baadhi ya wanawake ukishawapa hela wanapata uchizi,mpaka iishe ndio wanakaa sawa.
Umeongea pointi sana, haya vijana ambao hamjaoa pitiezi huu uzi huu ndio ukweli

Kama mkeo unampa pesa na anapanga budget inaenda vizuri sema asante Mungu

Maana wapo wanawake ni vimeo hawafai kuachia hata buku anunulie watoto mkate wa chai asubuhi utashangaa watoto anawapa chai kavu yeye anaenda kwenye vikoba
 
Sikilizeni nyie vijana... mwanaume jabali na wa kweli kama sisi wakongwe hufanya yote. Unanunua mahitaji yote muhimu kwa jumla unavibwaga ndani hapo. Afu kuna vitu vingine havinunuliki kea jumla. Unatoa bulungutu unamrushia wife kitandani... unampa busu moja mwanana na kauli ya kiumeni "tutaonana tena tarehe kama ya leo mwezi ujao"
Hata urudi umeelewa saa saba usiku, utaambiwa pole kwa majukumu mume wangu
Vijana wa siku hizi wamekuwa wagumu kuelewa hili then
 
Kutoka kwangu mpaka dukani kuna umbali wa 1.5 Km wife hajui kudrive, mwanzo wa mwezi inabidi niende kununua vitu vya jumla vya mwezi mzima!

Kila Jumamosi naenda gulioni namnunulia vitu vya wiki nzima kutokana hivyo hata nikimuachia hela hawezi kudrive kwenda sokoni! Je nakosea!??
Kununua vitu vya mwezi mzima ndo mpango
 
Sikilizeni nyie vijana... mwanaume jabali na wa kweli kama sisi wakongwe hufanya yote. Unanunua mahitaji yote muhimu kwa jumla unavibwaga ndani hapo. Afu kuna vitu vingine havinunuliki kea jumla. Unatoa bulungutu unamrushia wife kitandani... unampa busu moja mwanana na kauli ya kiumeni "tutaonana tena tarehe kama ya leo mwezi ujao"
Hata urudi umeelewa saa saba usiku, utaambiwa pole kwa majukumu mume wangu
UZI UMEUFUNGA WEWE! SALUTE! JABALI!
 
Mimi kipato Changu ni cha kuunga unga
Mara nyingi huwa kuna issue nasikilizia.
Kila Mwisho wa Mwezi huwa nampa 900,000/= TZS cash kwa Matumizi yafuatayo

1. Chakula cha Mwezi mzima (Mimi + Yeye + Dada wa kazi + Mtoto Mmoja)
2. Bills za Umeme
3. Maji
4. King’amuzi Azam
5. Mshahara wa Dada wa kazi
6. Vitu vya Mtoto Mdogo Diaper
7. Nguo za Mama na Mtoto
8. Vinywaji Soda na Juice
9. Vocha ya Mama
10. Nauli zake za kuzurura Nyumbani (Yeye ni Mama wa Nyumbani)

Majukumu yangu
1. Emergency za hapa na pale nahusika
2. Kodi ya kibanda tunachokaa
3. Ujenzi
4. Mafuta na Marekebisho ya Pikipiki ya Familia
5. Afya na Matibabu
7. Mambo ya ndugu , wazazi marafiki
8. Uwekezaji
9. Ukarabati wa kitu Chochote cha Nyumbani
10. Matumizi yangu Binafsi Mjini
11. Michango yote ya Mtaani, Jumuiya, Kanisani

Sasa hapo sijui niko sawa au kuna sehemu nazingua . Ushauri wenu wakuu
Nawe una kitu cha kufundisha, asante, nimeelewa na kujifunza kitu hapo
 
Ipo hivi: ukitaka kuwa na maisha marefu na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea na mkeo, pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha muache mkeo awe na jukumu la kuratibu mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi fungu husika hata kama limetokana na michango yenu wawili. Wanawake WENGI wanajua sana kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata kama utakuwa umeishiwa! Na michango ya wengine hapo juu ipo vizuri sana.
 
Dah, wotehao siku hizi hawapo, utafiti wangu wenye risachi ndogo 50% ya wanaume wetu hawa hawajui kununua ila pia wote hao wanajua kuwa wanasaidiwa!
Habari za saizi wakuu,

Poleni kwa majukumu ya kila siku moja kwa moja niende kwenye point.

Kati ya hawa ni yupi mzuri zaidi, mwanaume anaeacha pesa ya matumizi nyumbani na mwanamke ndio anaepanga matumizi au mwanaume anaenunua kila kitu cha ndani na kama kuna matumizi ya ziada yakubidi uombe pesa kwa kutolea maelezo.
 
Inategemea na jamii husika na mazoea ya malezi. Nimekua nikiona baba yetu anaenda sokoni na anapika akiwa na muda, nimeoa mwaka wa 8 sasa ktk familia yangu kwenda sokoni ni jukumu la baba na huwa napika nikiwa na muda.
 
Mimi kipato Changu ni cha kuunga unga
Mara nyingi huwa kuna issue nasikilizia.
Kila Mwisho wa Mwezi huwa nampa 900,000/= TZS cash kwa Matumizi yafuatayo

1. Chakula cha Mwezi mzima (Mimi + Yeye + Dada wa kazi + Mtoto Mmoja)
2. Bills za Umeme
3. Maji
4. King’amuzi Azam
5. Mshahara wa Dada wa kazi
6. Vitu vya Mtoto Mdogo Diaper
7. Nguo za Mama na Mtoto
8. Vinywaji Soda na Juice
9. Vocha ya Mama
10. Nauli zake za kuzurura Nyumbani (Yeye ni Mama wa Nyumbani)

Majukumu yangu
1. Emergency za hapa na pale nahusika
2. Kodi ya kibanda tunachokaa
3. Ujenzi
4. Mafuta na Marekebisho ya Pikipiki ya Familia
5. Afya na Matibabu
7. Mambo ya ndugu , wazazi marafiki
8. Uwekezaji
9. Ukarabati wa kitu Chochote cha Nyumbani
10. Matumizi yangu Binafsi Mjini
11. Michango yote ya Mtaani, Jumuiya, Kanisani

Sasa hapo sijui niko sawa au kuna sehemu nazingua . Ushauri wenu wakuu
[emoji109][emoji109][emoji109]
 
Kiukweli binafsi nikiwa nina bajeti nzuri huwa naomba kujua orodha ya mahitaji ya ndani. Kama nipo nanunua kila kitu,kama sipo napiga simu anaenda kwa Mangi kinanunuliwa kila kitu kama alivyohitaji yeye (sitaki lawama). Baada ya hapo namwachi ki elfu kadhaa cha Emergency.
Basi! Suala la kumuachia hela afanye yeye kila kitu cha ndani/jikoni hiyo nadhani sijafikia status hiyo. Ikifika nitafanya nione inavyoenda.
 
Back
Top Bottom