Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Majibu sahihi anayo mwanamke kwa swali lako kama unavyotaka wajibu.

Mimi kama mimi ni bora kununua vitu na kuviweka ndani maana uzuri umewazidi nguvu wanawake na kupelekea baadhi ni bora akanunue carolight kuliko unga wa kula na watoto.
Huyu atakua si mzima wa akili
 
Mm nanunua mahitaji ya mwezi kama mchele, unga ngano/mahidi, maharage, mafuta ya kula, chunvi, na sukari baada ya hapo nampa kiasi cha pesa ya mboga ya mwezi mzima, pia ni jukumu langu kuleta kuleta nyanya na mboga mboga kila jmosi, haya ndio makubaliano yetu na imenisaidia sana huu mwaka wa nne kwenye familia.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Mimi kila kitu nanunua .

Na pia nitampa Pesa kwaajili ya Mambo mengine ambayo sio lazima aniambie.



Haya mambo ya kuacha Pesa mezan kila siku , yanafanya Mwanamke aweke akilin Pesa sana,kuliko kukuweka wewe akilini.
 
Kama mwanamke ni mswahili swahili atapenda kuachiwa cash kila siku.
 
Una mawazo ya kizamani sana, sikushauri uoe mchagga au uje uishi huku ughaibuni.
 
Mimi ninachofanya naenda sokoni nanunua mchele unga na kila kitu cha ndani kiwemo kisha naacha na pesa ya kununua chipsi pale anapotamani au vitu vidogo vidogo hivi.

Lakini sitokuja kukaa n pesa ya matumizi ya ndani hata siku moja,pesa inayohusu mambo ya kula namuachia wife.

Nikikaa nazo mara natumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…