Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Yupi bora, mwanaume anayeacha pesa au anayenunua mahitaji yote mwenyewe?

Ukwelinasema

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2021
Posts
454
Reaction score
542
Habari za saa hizi wakuu,

Poleni kwa majukumu ya kila siku moja kwa moja niende kwenye point.

Kati ya hawa ni yupi mzuri zaidi, mwanaume anaeacha pesa ya matumizi nyumbani na mwanamke ndio anaepanga matumizi au mwanaume anaenunua kila kitu cha ndani na kama kuna matumizi ya ziada yakubidi uombe pesa kwa kutolea maelezo.
 
Binafsi ingawa sina mke lakini naona ni bora mke awe na uhuru na sehemu yake.

Pangeni budget, ukishajua matumizi yote ya chakula nyumbani ni kiasi gani unatenga fungu unampa. Mwanamume kuanza kudeal na mambo ya jikoni directly ni kukosa kazi.

Mwanamume unapaswa kuwaza mambo makubwa kama ujenzi, kodi ya nyumba, ada za WATOTO, kuongeza kipato n.k

Ikitokea emergency mnakaa mnajadili mtatatua vipi.

Hakuna kitu sikipendi kama uko busy umekaa tena sometimes na mgeni unaanza tena kuambiwa mboga ya jana iliisha, au kiberiti kiliisha.
 
Back
Top Bottom