Yupo wapi dereva teksi alyefichua njama za kumpindua Nyerere mwaka 1982? Je, alilipwa chochote kama ‘asante’?

Yupo wapi dereva teksi alyefichua njama za kumpindua Nyerere mwaka 1982? Je, alilipwa chochote kama ‘asante’?

Mkuu hii ndio principle kwenye intelligence kwamba haondolewi mtu mpaka ijulikane ombwe litazibwa na nani?

Uganda walimtoa Amin wakapita Marais kama 10, Same to Burundi waliompindua Rwagasore wakapita Marais kibao hapo kati nao ikawa mchezo kupinduana. Na hii ni case kwa nchi nyingi tu stability ilipotea baada ya mapinduzi.

So hapa sipingi serikali kubadilika ila sio kwa mapinduzi maana ombwe linabaki wazi so inakua gombania goli
Waliopo ni matokeo ya imani.
Waliaminiwa ndio maana wakawepo.

Pia wanaokuja ni matokeo ya imani.
"The only thing that never change is changes."
Mabadiliko hayazuiliki iwe ni mazuri au mabaya.
 
Chanzo:
Code:
(1) HATIBU GANDHI and OTHERS v REPUBLIC ( ) [1987] TZCA 18; (14 December .... https://old.tanzlii.org/tz/judgment/court-appeal-tanzania/1987/18.
(2) Tanzania coup plot uncovered - UPI Archives. https://www.upi.com/Archives/1983/01/22/Tanzania-coup-plot-uncovered/8958412059600/.
(3) Zacharia Hans Poppe: The untold story of a Kagera war veteran. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/national/zacharia-hans-poppe-the-untold-story-of-a-kagera-war-veteran-3551376.
Naijua hii ila nimesema kuwa hata mahakamani vitu vinavyopelekwa vinakuwa vimechujwa sana ili kulinda implication zake. Kwenye hiki sakata kuna jamaa mmoja nilikuwa namfahamu na alishiriki kwenye patashika la kuua yule jamaa pale Kinondoni.
 
Waliopo ni matokeo ya imani.
Waliaminiwa ndio maana wakawepo.

Pia wanaokuja ni matokeo ya imani.
"The only thing that never change is changes."
Mabadiliko hayazuiliki iwe ni mazuri au mabaya.
Ni kweli but blind faith is bound to fail.... Mabadiliko bila ya kujua atakua Bora kuliko aliyepita Haina maana yoyote Ile.
 
Nilishangaa hata Patrobas Katambi alikuwa mwenyekiti BAVICHA Taifa kumbe ni usalama. Leo hii Naibu waziri na yupo CCM. Hii nchi hii.
Sio huyo tu wapo wengi sana hata kiongozi wetu pale kinondoni ni mmoja wao. It's normal hta mdhamini wa CHADEMA kata nayoishi ni JWTZ!!

Sema wapo kwa kazi nyingi not necessarily kuzuia wasichukue dola. Wanataka tu kuwa ahead of the information which is fine.
 
Haukuwepo Dar ulikuwepo kijijini ndio maana haukuwahi kusikia

Hapa ndio tunapataa maana ya lile neno MJINI SHULE Yani ukiwa mjini Kuna vitu unavijua bila ya kuenda shule
Aisee..!!! Kwa technolojia ilivyo sasa, kuna uwezekano wa Dar asijue jambo fulani lakini aliyeko Kilando akalijua.
 
Unasema hayo ni maneno tu wakati yametamkwa na Rais na mwenyekiti wa chama kinacho ongoza nchi ?

Wapumbavu wamezidi humu ni kupoteza muda tu
Sasa Rais ndio anaamua Nini kwenye katiba mpya? Mfano Kenya huwa kitu kikionekana kina madhaifu wanaenda mahakamani Wala hawasubir kauli ya Rais.

Mfano suala la BBI mahakama ilipinga ingawa Rais Kenyatta alitaka liendelee ila hakuna alichoweza lazimisha. Unaweza ona jinsi katiba mpya inampoka Rais madaraka mengi mnoo so aseme kitabu sio kitabu ataona tu utekelezaji wake mbaya zaidi Jaji mkuu huwezi mbadilisha Wala kamtimua.
 
Subiri kwanza.

Una miaka mingapi dogo ? Na kichwani kupo timamu kweli ?

Isiwe tuna poteza muda bure kwa kufanya michezo ya kijinga hapa
 
Hatukuwepo....

Ila yameandikwa vitabuni na magazetini....

Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa najisomea nakala ya gazeti la RAI kila wiki....nikapata kuwajua akina LUTENI LUGAKINGIRA ,EUGENE MAGANGA ,UNCLE TOM ,TAMIMU ,HATTY MC GHEE na wengineo.....

Tupende kujisomea....

Maarifa hupatikana humo....

#SiempreJMT[emoji120]
Nashukuru umenikumbusha Hatty McGhee. Tulisafiri pamoja kwa ndege ya jeshi kwenda Uganda kikazi mwaka 1980 baada ya Idd Amin kutolewa. Mimi nikiwa raia kwenye hiyo Tume. Alikuwa askari mrefu, aliyesoma kiasi chake, mwenye bashasha, kijana wa Tanga. Nilishtuka baadaye niliposikia alikuwemo kwenye kundi hilo. Mapinduzi haya yalipangwa baada ya Tanzania kuanza kupata matatizo ya kiuchumi ambayo hayakuwa makubwa kiasi kile kabla ya vita ya kumng'oa Idd Amin. Matatizo ya mfumuko wa bei, mishahara kutokidhi mahitaji hatukuwahi tena kuyamudu mpaka leo!
 
Historia ya serikali ya nchi hii ina Mengi na Mengi hayo hatuyajui.

Kina Hanspope, Maganga, Tamimu na wengine wengi walipanga kumuua na kuipundua serikali ya Mwl Nyerere.

Inadaiwa dereva teksi aliyekuwa akiwasafarisha wapanga mapinduzi kuhudhuria vikao vyao vya Siri alibaini mpango wao na kuripoti kwa vyombo vya usalama.

Muda umeenda Sasa, huyu dereva teksi ni nani? Yupo wapi Sasa? Alilipwa nini na serikali Kama shukurani ya kuinusuru nchi?
... amelipwa mishahara yake yote na marupurupu ya ustaafu!
😎
 
Huyo alikuwa mtu wa usalama alifanya kazi ya teksi driver, na hata Leo bado wapo na wengine ni shoe shiners, fundi viatu mjini
Alikuwa tax driver tu, sema wale jamaa walikuwa wajinga, kalewa kaanza kusema siri kwenye tax. Actually aliyefikisha kwa Mahiga alikuwa Paul Sozigwa ambaye naye alikuwa mteja wa huyo dereva
 
Nduo maana Bas jk alimpeleka akalime bamia huko mtera sio!!?

KWAMBA akachungulie kaburi si ndio!!!
Eeh,alipohitajika 2015 kukata watu,maana anasifika kwa ukauzu,akamrudisha,akapiga panga watu wakanuna,wengine wakaenda kufunga nyuki na kulima zabibu,nasikia alisema 'wenye miaka 60 na zaidi mn astaafu na jakaya'..ikaisha hiyo
 
Nani alisema TISS haitakiwi kuwepo upinzani? Nachofahamu kitengo chochote makini lazima kiwe ahead sio sababu ya chama tawala ila kwamba hata nchi ikienda upinzani basi kuwepo regulated.

Nyie ndio mnafanya TISS ionekane ni CCM ila kikawaida ni halali tu usalama kuwepo makanisani, Yanga, CHADEMA etc ku regulate usalama. Hata Mbowe anafahamu hilo na mara nyingi huwa anasema "najua mpo humu, mfikishieni mama...."
Marando na mrema chama kilikua Chao kabisa,pengine chadema nayo 'yao'
 
Historia ya serikali ya nchi hii ina Mengi na Mengi hayo hatuyajui.

Kina Hanspope, Maganga, Tamimu na wengine wengi walipanga kumuua na kuipundua serikali ya Mwl Nyerere.

Inadaiwa dereva teksi aliyekuwa akiwasafarisha wapanga mapinduzi kuhudhuria vikao vyao vya Siri alibaini mpango wao na kuripoti kwa vyombo vya usalama.

Muda umeenda Sasa, huyu dereva teksi ni nani? Yupo wapi Sasa? Alilipwa nini na serikali Kama shukurani ya kuinusuru nchi?
Kumbe usalama Bado huujui! Huwezi kufichua Siri kubwa ukabaki hai!
 
Back
Top Bottom