Yupo wapi siku hizi?

Yupo wapi siku hizi?

F431E0EB-EC20-4115-98CB-8BC7E8564F87.png
Ndio nyimbo zangu Siku hizi. Old school. Hawa WCB speed yao imenishinda aisee.
 
zamani ukikumbuka unaweza ukamwaga hata chozi yani hivi wako wapi sumbi na bocha,abiola, bupe na aunt seche wa kaole, yu wapi dada alieimba maprosooo
"Maprosooo nieleze ukweli wako baba" ila huyu dada sijui kapotelea wapi..waridi na Aisha wa mambo hayo nao sijui wamepotelea wapi
 
Mkuu Lushoto ni kama ulaya kule jamaa usikute mazingira safi yamemvutia halafu unaweza dhani kachacha kumbe mwana anapiga pesa za kilimo kule juuu kwa juu
Sasa kama Mkapa mwenyewe anaishi Lushoto ije kuwa huyo mshkaji

Lushoto ni pa ukweli sana
 
Kama sio juhudi zako jf mambo haya tungeyapata wapi. Udumu milele
 
OTen yupo Morogoro, Madizini Kilalala! Anakunywa mpk wanzuki
Mike T na track zake
Hali halisi ft Jay dee
Sintobadilika ft Qchief
Je utanipenda ft Mad Ice
Alikuwa bishoo flani hiv classic, namkubali sana

Oten track kali ilikuwa nicheki ninavyongara
 
Amemrudia MUNGU.... anafanya shughuli za dini na IMANI TV & RADIO - Morogoro
Tabia wa kidedea ni marehemu nadhani

Yuko wapi Frank Mtao wa channel 10 mara ya mwisho nilisikia yupo China

Na Kuna jamaa aliyekuwa anafanya hihhop base ya eatv kabla ya Saigon
 
Ni sahihi Mkuu.... Kali P anapatikana sana MARKAZ GONGO LA MBOTO... Wakati anaacha mziki ilikuwa MWEZI WA RAMADHANI na alikuwa ametoka kumalizia album yake ya 3 ambayo hakuiingiza sokoni.... Allah atujaalie mwisho mwema!
Kal p ndio huyo pembeni ya suma lee ni Sheikh na ndio kamfundisha fundisha sana suma lee mambo ya diniView attachment 1102104
 
Umechanganya Madawa mkuu..Ma-jobless ni BDP(Bigdogg Pose) waliokuwa wanafanya recording zao na Amit Bajaj Mentor.
Wapo kinondoni shamba kwa msokota nywele
Walioimba "Mke wa mtu Sumu" na "wanaokwenda jela" wanaitwa LWP (Life with Purpose) walikuwa wana record na Pfunk nadhani wapo TMK
BDP wametawanyika tawanyika but habari njema ni kwamba hapa majuzi wamesharekodi wimbo bado kuutoa tuu... Issa yupo kigamboni, drez kimara na computer pose nadhani ndio kabaki kino.
 
Back
Top Bottom